Na Amina Athumani
TIMU za mpira wa kikapu za Unguja zimeanza vyema michuano ya ligi ya Taifa 'Taifa Cup', katika mechi za ufunguzi zilizochezwa jana katika viwanja vya
Donbosco, Dar es Salaam.
Katika michuano hiyo timu ya wanaume ya Unguja, iliifunga Mwanza kwa vikapu 56-55 mchezo uliokuwa mkali huku zikishambuliana kwa zamu.
Unguja Queens, nao walionesha umwamba na kudhihirisha kuwa wamekuja kutwaa ubingwa na si kutalii, kama zilivyo timu nyingi zinavyofanya.
Timu hiyo iliichapa Iringa kwa pointi 61-58, katika mchezo uliopigwa pia kwenye viwanja vya Donbosco.
Katika michezo mingine, iliyochezwa katika viwanja vya Leaders, Kilimanjaro wanaume waliicharaza Iringa kwa pointi 38-33 na Morogoro, wakiifunga Mbeya kwa pointi 60-56.
Michuano hiyo, imeandaliwa na Shirikisho la Mpira wa kikapu nchini (TBF) na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Mashindano hayo yataendelea hadi Jumamosi. Kauli mbiu ya michuano hiyo ni mpira wa kikapu na miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment