Na Mwali Ibrahim
KLABU zitakazoshiriki mashindano ya mpira wa wavu ya Kombe la Nyerere, zinatarajia kuwasili leo mjini Moshi kwa ajili ya michuano hiyo.Mashindano hayo yanatarajia
kuanza kesho kutwa, hadi Jumapili katika viwanja vya Hindumandal mjini humo.
Michuano hiyo imeandaliwa na Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA).
Jumla ya klabu 21, zitawasili kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo ambazo ni KAVC, KCC za Uganda na NCC, KPLC, KBC, STIMA na Youth za Kenya.
Nyingine ni Jeshi Stars, Magereza, JKT, Shule za Sekondari za Makongo na Loard Baden Powel, Kijichi, Tanga Central, Rukwa, Moshi University, KCMC University. Nyingine ni Mafunzo, Nyuki na Polisi za Zanzibar.
Akizungumza kwa simu akiwa Tanga jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya TAVA Tanzania, Alfred Selengia alisema, maandalizi ya mashindano hayo yamefikia hatua za mwisho.
Alisema mashindano hayo yatachezeshwa na waamuzi 12 kutoka katika nchi zote tatu za Kenya, Uganda na Tanzania.
Selengia alisema, wanatarajia mshindi atapatikana kihalali kwa kuwa usimamizi wa kutosha utakuwepo.
No comments:
Post a Comment