Na Zahoro Mlanzi
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limepitisha majina ya makocha 40 akiwemo Raisi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Leodegar Tenga kushiriki katika kozi ya ukocha ya leseni B ya shirikisho hilo.
Kozi hiyo inatarajia kuanza Dar es Salaam kuanzia Desemba 19 mpaka 22, mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF Biniface Wambura, alisema makocha wote waliopitishwa wana cheti cha ukocha cha ngazi pevu, ambapo kozi hiyo awali ilikuwa inachukuliwa na makocha wowote bila kujali elimu zao.
Aliwataja makocha hao na mikoa wanayotoka kwenye mabano ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Kassim Majaliwa (Dar es Salaam), Michael Bundala (Dar es Salaam), George Komba (Dodoma), John Simkoko (Morogoro), Juma Mwambusi (Mbeya), Samson Mkisi (Mbeya) na Sylvester Marsh (Mwanza).
Wengine ni Salum Madadi (Dar es Salaam), Mohamed Nyange (Dodoma), Madaraka Bendera (Arusha), Ally Mtumwa (Arusha), Charles Mkwasa, Idd Mshangama, Hassan Mlwilo na Leopard Tasso (Dar es Salaam), Mohamed Msomali (Morogoro), Mbarouk Nyenga (Tanga).
“Pia wamo Mohamed Tall, Dkt. Mshindo Msolla, Fred Minziro na Eugene Mwasamaki (Dar es Salaam), Abdallah Hussein (Kilimanjaro), Oscar Korosso (Mbeya), Charles Kilinda (Pwani), Salum Mayanga (Kagera), Hamimi Mawazo (Mtwara), Rogasian Kaijage (Kagera), Eugene wana Mohamed Mozi (Tabora),” alisema Wambura.
Makocha wengine ni Charles Matoke, Abdul Mingange, Jamhuri Kihweli na Mohamed Rishard (Dar es Salaam), Peter Magomba (Singida), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, Juma Nsanya (Tabora), Gilbert Mahinya (Tabora), Juma Mzigila (Morogoro), Joseph Sehaba na Charles Mngodo (Dodoma).
No comments:
Post a Comment