Na Heri Shaaban
MWIMBAJI wa nyimbo za injili Christina Shusho, anatarajia kuzindua albamu yake ya tatu ya Nipe macho katika Desemba 23 mwaka
huu katika Ukumbi wa Daimond Jublee, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Msemaji wa uzinduzi huo, Samwel Hilay alisema siku hiyo pia kutakuwepo wasanii mbalimbali wa injili wa ndani na nje ya nchi kwa ajili kumsindikiza mwimbaji huyo.
Aliwataja baadhi ya wasanii watakaosindikiza uzinduzi huo wa hapa nchini kuwa ni Rose Muhando, Bahati Bukuku na kutoka nje ya nchi ni Ruben Kigame.
"Tunazindua albam yetu ya tatu, sambamba na kusherekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara siku hiyo, ambapo tunawaomba Watanzania wajitokeza kwa wingi.
"Mgeni rasmi anatarajia kuwa Askofu wa Tanzania Asembels of God(TAG), Banabas Mtokambali," alisema.
Kwa upande wake Shusho, aliwataka Watanzania kumkumbuka Mungu na kumsifu kila wakati.
Alisema baada uzidunzi huo, atawasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na pia atawatembelea wagonjwa hospitani kuwapa pole.
No comments:
Post a Comment