MABONDIA Ramadhani Nasibu na Antony Kairuki wa Kenya, wanatarajia kupima uzito kesho kwa ajili ya pambano lao la maadhimisho ya miaka 50
ya Uhuru wa Tanzania Bara, litakalofanyika kesho kutwa katika Ukumbi wa DDC Keko, Dar es Salaam.
Pamabno hilo lisilo la ubingwa litakuwa la uzito kg. 51 la raundi nane.
Akizungumza Dar es salaam jana, Mratibu wa pambano hilo Pius Agaton, alisema lengo lao kutoa burudani kwa wapenzi ngumi katika kusheherekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Alisema maandalizi ya pambano hilo, yamekamilika na mabondia wote wanaendelea na mazoezi na tayari Kairuki yupo nchini.
Naye Nasibu alisema, amezingatia mafunzo ya kocha wake ambapo pia ataendelea kujifua hadi siku ya mwisho, ili kujiweka vizuri kumshinda mpinzani wake.
No comments:
Post a Comment