Nchi imetumbukia Baharini- Dkt.Slaa
*Atamani zitumike kulipa madai ya walimu
*Alilia watoto wa maskini kukosa mikopo
Na Rehema Maigala
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Wilbroad Slaa, amelaani vikali kitendo cha Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda, kukiri na kutetea uamuzi wa ofisi yake kupandisha posho za wabunge huku Watanzania wakitaabika na hali ngumu ya maisha.
Kwa mujibu wa Spika Makinda posho hizo za wabunge zimepandishwa kutoka sh. 70,000 hadi 200,000 kwa siku na tayari wameanza
kulipwa.
Akizungumza na gazeti hili jana, Dkt. Slaa alisema kitendo cha spika kuridhia na kutetea kuwapandishia posho wabunge ni kielelezo tosha kuwa nchi imetumbukia baharini na hakuna msaada wa kuiokoa kwa sasa.
Dkt. Slaa aliyezungumza huku akionesha masikitiko alisema, hakutarajia kama spika angetoa kauli hiyo hasa kwa kuzingatia kuwa bunge ni kioo cha nchi na kwamba jukumu lake ni kusimamia serikali na vyombo vyake vyote kwa masilahi ya wanyonge.
Alisema kauli ya Spika Makinda kukiri kuwapandishia wabunge posho ni sawa na kuwavunja matumaini Watanzania na kwamba wanapaswa kujiuliza ni nani wa kuwasaidia ikiwa wabunge wanajisaidia wenyewe.
“Watanzania wengi wanaishi katika hali ngumu kwa sababu ya maisha kupanda, kipato cha Mtanzania kwa siku ni kidogo ambacho hakiwezi kukidhi matumizi yake ya kila siku.
Lakini Mtanzania huyo hana wa kumsemea wala wa kumpunguzia mzigo mzito ili awe na unafuu wa maisha, hana wa kumsaidia ili awe na maisha mazuri hata kidogo,” alisema Dkt.Slaa na kuongeza.
“Watoto wa kimaskini wengi hawaendelei na masomo ya elimu ya juu kwa sababu ya kukosa mikopo kutoka serikalini, kwa nini hizo pesa zilizoongezwa kwa wabunge zisingepelekwa kwa wanafunzi?
Au tunaithibisha ile kauli inayosema kuwa mwenye nacho anazidi kuongezewa?” Alihoji Dkt.Slaa.Alisema wabunge wamekuwa na posho nyingi za kila aina ambazo zingine hata hazistahili kulipwa huku wakiwaacha Watanzania wakiwa na hali ngumu ya maisha.
Alisema kitendo cha Spika Makinda kutetea posho hizo bila kujali maisha ya Watanzania walio wengi ni dalili ya chombo hicho kuwakandamiza wananchi hivyo kwenda kinyume na kazi ya bunge ya kuwatetea wananchi.
Alisema ni aibu kwa wabunge kuongezewa posho bila hata kuwajali wafanyakazi ambao wengi wao wanalipwa mshahara mdogo na kuwataka Watanzania kwa ujumla kutafakari wanatembea katika mstari upi.
Alisema sehemu kubwa ya umaskini wa Watanzania unatokana na viongozi wa serikali kujigawia posho nyingi ambazo hazina maana yeyote kwa taifa.
“Mpaka hivi sasa walimu bado hawajalipwa madeni wanayoidai serikali, wanatishia kugoma ni vyema posho hiyo ingepelekwa kwa walimu ili waweze kutoa elimu bora kwa watoto wetu,” alishauri Dkt.Slaa.
Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari juzi wakati akizindua ripoti ya Maendeleo ya Wanawake Duniani kuhusu haki kwa mwaka 2011, Spika Makinda alikiri nyongeza ya posho za vikao vya wabunge kupanda kutoka sh.70,000 hadi 200,000 kwa siku.
Alisema wamefikia hatua hiyo kutokana na kupanda kwa gharama za maisha mjini Dodoma na kwamba wabunge walianza kupokea posho hiyo mpya Novemba 8, mwaka huu.
Akisisitiza umuhimu wa posho hizo alisema sh.70,000 isingemsaidia mbunge kumudu gharama hata za chumba kwa madai kuwa zimekuwa juu kutokana na mji wa Dodoma kuwa kitovu cha elimu ya vyuo vikuu kwa sasa.
“Kila kitu kimepanda bei na kwa bahati mbaya nyumba zile za CDA (Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu) zilizokuwa nafuu zilichukuliwa na wabunge wa bunge la tisa kwa mikataba binafsi na wengi hawajazirudisha hadi sasa ili kuwezesha wapya kuzipangisha,” alinukuliwa akisema Spika Makinda akitetea posho hizo juzi.
Mkurugenzi naye awashangaa wabunge
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti na Utetezi wa Haki za Ardhi, Bw. Yefred Myenzi, amesikitishwa na kitendo cha Spika Makinda kutete posho hizo na kuwataka wabunge kutambua kuwa hali ngumu ya maisha ipo kwa kila Mtanzania na si kwao pekee.
Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana, Bw. Myenzi alisema hali halisi ya Mtanzania hairuhusu mbunge kupandishiwa posho kutoka sh. 70,000 hadi 200,000 kwa siku na kwamba hizo ni anasa .
Alisema wabunge wanavyanzo vingi vya mapato mbali na mishahara yao hivyo hawakustahili kuongezewa posho kiasi hicho huku Watanzania wakizidi kulilia hali ngumu ya maisha.
“Hali hii inaonesha ni kwa jinsi gani wabunge walivyo wabinafsi, wanajali masilahi yao wenyewe na kuacha wananchi wakiumia,” alisema.
Katibu wa Bunge akanusha
Hata hivyo hivi karibuni Katibu wa Bunge, Dkt.Thomas Kashililah, alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akikanusha kuwepo kwa nyongeza hiyo.
Katika taarifa hiyo Katibu huyo wa bunge alikiri kuwa wabunge wanataka waongezewe posho za vikao lakini mapendekezo hayo hayajaanza kutekelezwa.
Alisema mapendekezo ya nyongezo hiyo yaliibuka katika mkutano wa wabunge mjini Dodoma, Novemba 8, mwaka huu walipoiomba serikali iangalie upya suala hilo kwa lengo la kuboroshewa.
Dkt. Kashililah alisema serikali ilikuwa haijatoa taarifa iwapo posho hiyo imeongezeka kutoka sh.70,000 hadi 200,000.
Balozi Seif atetea posho Wakati huohuo, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amesema wabunge kuongezwa posho za vikao ni halali kwa kuwa gharama za maisha katika Mkoa wa Dodoma zimepanda.
Alisema ongezeko hilo litalinda heshima za wabunge pindi wanapokuwa wakiendelea na vikao vya bunge.
“Nafikiri siyo heshima kwa mbunge baada ya kumaliza vikao anakwenda kulala kwenye gesti ya sh. 5000 hii ni aibu, ni sawa posho zilivyopandishwa,” alisema.
Alisema anakubaliana na uamuzi wa serikali kuwa ni mzuri na utampa nafasi nzuri mbunge ya kuishi wakati wa vikao.
Hukumu kwa wabunge wa CCM ipo 2015 Kuongezwa kwa Posho hizi wamelipwa kama fadhila ya kupitisha muswada mbovu wa sheria ya uanzishaji wa katiba.
ReplyDeleteWizi mtupu!
ReplyDeleteHizi ni hujuma kwa nchi kama Tanzania kuweza kuweka posho kubwa kiasi hicho yaani "sitting Allowance" kwani majukumu yao si yanaeleweka kuwa ni kutunga sheria na kuwasilisha matatizo ya wananchi kwa serikali na ninacho fahamu mostly wabunge wengi wanaishi Dar, na hayo mawazo wanayosema wanawakirisha wananchi mara nyingi yanakuwa na kwao ndiyo maana wanaweza hata kuongeza posho bila kujari maslahi ya wananchi wanao wawakilsha lakin waangalie 2015 si mbali sana wale wote wanao fanya vizuri watachaguliwa.
ReplyDeleteCRY THE BELOVED COUNTRY
ReplyDeletePosho za wabunge zinapatikana mara moja.. lakini waalimu hawajalipwa mishahara mpaka leo,ndio tueleweje hapo???
ReplyDeleteHIVI MNATEGEMEA KWELI WAALIMU WATAENDENDELEA KUFUNDISHA BILA MALIPO?Watu wanaishi kwa taabu, maji na umeme wa shida, matibabu ya shida,lakini wenzetu wanazidi kuongezana posho tu.
WAKATI UTAFIKA WATU WATASEMA SASA INATOSHA!
nchi yetu isije ikabadilika kuwa Uwanja wa mapambano.
TUMEJIONEA lIBYA; MISRI;TUNISIA...Ulafi huo utakutokeeni puani jamani!
Hiki ndicho tulichotaka watanzania kupitia kula zetu mwaka jana acheni waheshimiwa waendelee kula hata hivyo mimi bado hawajaanza kula vizuri. haya ni matokeo ya dhambi ya kumnyima kula Dr Slaa na kuwapa wezi waongoze nchi. tuvumilie tu.
ReplyDeleteHiki ndicho tulichotaka watanzania kupitia kura zetu mwaka jana acheni waheshimiwa waendelee kula hata hivyo mimi naona bado hawajaanza kula vizuri. haya ni matokeo ya dhambi ya kumnyima kura Dr Slaa na kuwapa wezi waongoze nchi. tuvumilie tu.
ReplyDeletewabunge tunaomba muwakilishe mawazo yetu sisi wananchi bungeni na siyo muwakilishe matumbo yenu. Mbunge wetu wa jimbo la Manyovu Bw. Albert Ntabaliba chondechonde kipindi cha kampeni ulitumia fedha nyingi sana jimboni ikiwa ni pamoja kununulia watu pombe, kununua mabati kama sehemu wa kuwashawishi wapiga kura wakuchague sidhani kama posho ni njia sahihi ya kurudisha fedha zako kumbuka ulituahidi kuwa huendi bungeni kwenda kula bali kutetea maslahi ya wananchi. Please sisi wananchi wa jimbo lako tunahitaji visima vya maji kumbuka sisi akina mama tunateseka sana tunapohitaji maji , pia tunahitaji zahanati na kuwa na miundombinu sahihi. tusaidie hilo na si vinginevyo
ReplyDeleteIkiwa tunafurahia na kusherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania, kuongezeka kwa Posho za Wabunge ni doa katika maazimisho haya.Kuna Watnzania wengi wanalia na njaa, afya, ajira elimu mbaya hivi tunaelekea wapi? Haiwezi kueleweka kwa watu eti wapepandishiwa posho sababu gharama za maisha zimepanda Dodoma ila wakumbuke kama zimepanda n awao ikawa ndio njia pekee ya kujinasua, Walimu, Madaktari Raia wa kawaida watafanyaje? Tufikilie kwa umakini sana Na said T. Mulisa
ReplyDeleteWewe Mzee Slaa wacha unafiki wako,wabunge wa chama chako wanatafuna pia hizo pesa ila mkija kwa wananchi mnageuza maneno kwa kuwadanganya. Mmeona ni kaa la moto hilo kwenu wanasiasa sasa mnaanza kugeukana, hata wewe mwenyewe unatafuna pesa nyingi tu za chama chako ambazo ni zetu pia. Mtalaanika kwa unafiki wenu. Tuambie wabunge wa chama chako walichukua posho au hawakuchukua?
ReplyDeleteSawa kabisa hapo juu. Tayari mbunge wake Shibuda amesema wanaozipinga hizo posho ni wanafiki akiwepo yeye Slaa.
ReplyDeleteBinafsi naona wabunge wote wawe wa upinzani au chama tawala wameacha kupigania maslai ya wananchi na kupigania maslai yao. Suala la kujiongezea posho ni mfano tu wa namna ambavyo wanavyoshughulikia maslai yao. Tofauti yao ni moja tu wengine ni wanafiki pindi wanapoona ukweli kuhusu namna wanavyojipendelea umefichuka basi wanajiosha kwa kupinga. Kama posho hizo walizidai na kuzipokea kimya kimya iweje leo wanazipinga kwenye vyombo vya habari na kuzibali bungeni?
ReplyDeletekila mtu anawania tumbo lake ktk karne hii, dr slaa , utatuambia nini? wadanganye watu wengine , hakuna cha CHADEMA , CCM wala CUF wote wanapigania maslahi yao kibinafsi kwa kuwatumia wananchi wajinga masikini ,
ReplyDeleteHuo ndio ukweli kila mtu anawania watoto wake waende choo (washibe)
ReplyDeleteNYIE WATU WATANO HAPO JUU HAMNA UPEO,NA NI WANAFIKI SANA MSIOJUA SIASA NA MWENENDO WA NCHI YETU,NENDENI MASHAMBANI MKALIME.SISI TUNAZUNGUMZIA BUNGE,HATUZUNGUMZII CCM,CUF ,CHADEMA AU SLAA HAPA.TUNAUNGANA KUPINGA ONGEZEKO LA POSHO MBUMBUMBU NYIE.HUKU KWENYE MTANDAO HATUTAKI WATU WAJINGA.
ReplyDeletehuu ni upuuzi mmtupu kwa Ana makinda huku anajua wanachi maisha ni magumu na kusapoti posho zawabunge ziongezewe huyu mama kanikera mpaka basi, sitaki hata kusikia Taarifa zake from this tyme.
ReplyDeleteHUYU MAMA MAKINDA AMEKUA MTU MBAYA SANA NA ANALETA HOFU KATIKA TAIFA KWASABABU HANA MUELEKEO MZURI KATIKA MAAMUZI.TULITARAJIA ATUPE MOYO KUCHAGUA VIONGOZI WANAWAKE.SURA YAKE TU UKIMTAZAMA LAZIMA UPATE MASWALI MENGI JUU YA ROHO YAKE.YOU ARE SO UGLY MAMA MAKINDA,GO TO THE HELL...........
ReplyDeleteKUNA MIJITU MIJINGA SANA HUMU. HUYU SLAA ANALAANI POSHO ZA WABUNGE HUKU WABUNGE WA CHAMA CHAKE WAKICHUKUA,WANATUFANYIA USANII. WEWE KAMA UNAZUNGUMZIA BUNGE MLE NDANI YA BUNGE KUNA MTU ASIYETOKA NDANI YA CHAMA CHA SIASA? NADHANI WEWE LIMBUKENI TUTAWATAJA VIONGOZI NA VYAMA VYAO NA WABUNGE WAO HAO NDIO WENYE KUTULIZA
ReplyDeleteSasa nimemkubali kwa moyo wote Dr. Slaa. Kweli ni mtetetezi wa wanyonge.
ReplyDeleteNaapa kwa Dini yangu, nawachukia sana Wabunge wanao pewa hizo pesa na kutunisha mifuko yao kwa kutunyanyasa sisi tulio wachagua na kuwapigia kura za KULA.
Watoto wetu wame rudishwa majumbani kwa kukosa Karo za Universities, Anna hajaongea lolote maana anajua wabunge watahoji safari zake za nje kila siku tangu alipo ukwaa Uspika, alikuwa anamuonea husda Mh. Sita. Na wala hao walafi wabunge hawajasema wala kuwatetea hawa watoto wa wakulima wanao kosa mikopo ili waendelee na vyuo, wao Wabunge wana KULA NA KUNYWA NA KULALA WAMETUNISHA MIFUKO YAO KWA KODI ZETU WAKULIMA??? Mungu atawalaani. nimeamini, CHUKUA CHAKO MAPEMA ndiyo mwendo wa nchi hii. KWA JINA LA MUNGU, HATUFIKI.
Walisema kwenye Primary school, watoto wapatiwe mlo wa mchana, HAIKUTEKELEZWA, Vyuo vikuu watoto wapatiwe MIKOPO, HAIKUTEKELEZWA, lakini leo wabunge waongezewe POSHO, IMETEKELEZWA HARAKA KINYEMELA KABLA HATA YA KUTANGAZWA.. Ilipo tangazwa, ilikuwa just a formality???!!!ee Mungu, 2015, ikifika, wengine wawe wamefutika kwenye uongozi huenda Chadema itatuokoa, tumechoka sasa na huu uonevu.
TUNAZUNGUMZIA BUNGE SIO CHAMA KWASABABU ZITO KABWE ALIKATAA LAKINI AKALAZIMISHWA KUPOKEA PESA,WAPO WALIOKATAA GARI,JANUARY MAKAMBA ALIKATAA KUSAINI PESA YA KIKAO JUZI TU NA MAGAZETI YAMETOA ILE DOCUMENTI JINA LA JANUARY LIMEKATWA.WEWE NDIO LIMBUKENI UNAVAMIA MAMBO YA SIASA BILA FACTS.DONT BE FOOL AGAIN.
ReplyDelete>>>>>>TUSI SPELLING ZAKE HIZI HAPA>>>>>>>KUNA MIJITU MIJINGA SANA HUMU.>>>>>>>
ReplyDeleteHUYU SLAA ANALAANI POSHO ZA WABUNGE HUKU WABUNGE WA CHAMA CHAKE WAKICHUKUA,WANATUFANYIA USANII.
>>>>>>MATUSI KATIKA JAMBO AMBALO LINAHITAJI LOGIC HUASHIRIA UFINYU WA MAWAZO. ANONYMOUS ALIYETOA TAMKO HILO ACHUNGE MDOMO WAKE--OOOPS. ACHUNGE MANENO YAKE. TUNAWEZA KUTRACE IP ADDRESS YA MESSAGE HIYO NA KUFUNGUA JINAI. WATCH WHAT YOU SAY. CHADEMA INA WENYEWE...
NAKIRI KUWA WABUNGE WANATAKIWA KULALA PAZURI, NA PENGINE POSHO HIZO ZINA NIA NZURI. LAKINI PIA WAZO LA KUPUNGUZA GHARAMA ZA SERIKALI NI WAZO LANYE NIA NZURI. JE HATUWEZI KUKUTANA HAPO KATIKATI, YAANI KUWALAZA WABUNGE PAZURI NA KUPUNGUZA MATUMIZI KWA KUPUNGUZA MUDA WA KUKAA DODOMA WAKATI POSHO ZIKIWA JUU?
Huu ni ushenzi wanaotufanyia hawa wanasiasa wenye idadi kubwa bungeni hawajui kama hali zetu ni za maisha ni ngumu? wanafikiri ugumu wa maisha uko kwao tu hapo Dodoma. Hebu fikirini kwa makini ni idadi ngapi ya walimu waliopo mitaani wamesubuli ajira mlizowaahidi mwezi wa nane achilia mbali wanaodai madai yao ya miaka mingi?
ReplyDeleteMNAFAGILIA TU POSHO ZENU WANAFIKI WAKUBWA NGOJENI TUNAWASUBIRI MAIMBONI 2015.
Tasmini ya kauli biu ya kuadhimisha Miaka Hamsini (50) ya UHURU; "TUMESUBUTU,TUMEWEZA NA TUNAZIDI KUSONGA MBERE" kwa mantiki za msingi inaashiria namna serikali yetu TUKUFU alivyo kosa dira katika kusimamia mifumo sahihi ya uongozi na utungaji wa sera bora za kufufua pamoja na kuimarisha UCHUMI wa TAIFA letu; WAMESUBUTU-Kutuongezea gharama za maisha katika nyanja zote za kiuchumi na kupandisha posho za Wabunge kwa kushibisha matumbo yao; WAMEWEZA-kukusanyia kodi mifukoni mwao na kufanya hata serikali kukosa pesa za kulipa mishahara wafanyakazi wake;NA WANASONGA MBERE-Kuhakikisha rasrimali zote za Taifa wanazimiliki wao na ndungu zao.
ReplyDeleteSawa wabunge wetu kweli kudai posho kubwa, kwani kura nyigi mlizopata wengi wenu mmenunua kwa kanga na kofia!
ReplyDeleteMtanzania kura yako ni muhimu sana kwa mstakabali wa ustawi wa Tanzania yetu!Bunge la Tanzania bajeti ya kuongeza posho imetoka wapi?Spika Anne Makinda ana mfuko maalum wa posho? 'MUNGU IBARIKI TANZANIA'
Ni aibu kubwa kwa wabunge kuendelea kutetea matumbo yenu, tuwaangalie vimbelembele wa posho ni akina na kisha 2015 piga chini wote. Kwa nini mnatudanganya namna hii wakati wa kuomba kura! na kama watanzania hatutabadilika, walahi nasema tutaendelea kuteseka! Kwani najua wakati wa uchaguzi tunadanganyika kwa vitu vidogo na matokeo yake ndio hayoo.... Ushabiki wa vyama matokeo yake ni hayo... rushwa na wizi wa kura matokeo yake ndio hayoo.... na bado tutaendelea kuburuzwa na kuibiwa na hawa jamaa!!! tubadilike!!
ReplyDeletehawa wabunge hawasomi alama za nyakati Watanzania tunayaona wafanyayo fainali 2015,CCM ilipata asilimia 80 mwaka 2005 wakapata asilimia 60 kwashida mwaka 2010.wamepoteza asiliimia 20.tutawakamata na kuwatia gerezani mafisadi wote.Nyerere alisema hukuna dhulma isiyo na mwisho,ole wenu
ReplyDeleteNYERER, KARUME, MANDELA, NKULUMA NA WENGINE WALIKOMBOA NCHI ZAO TOKA KWA MKOLONI MWEUPE HIVYO BASI NA SISI TUUNGANE PAMOJA KWA UMOJA BILA KUJALI ITIKADI ZA DINI WALA KABILA WALA CHAMA KUMPINDUA MKOLONI MWEUSI KATILI WANAONYONYA WATANZANIA KWA KUJIPA POSHO KUBWA MISHAHALA MIZURI, MAGARI MAZURI,UFISADI, MIKATABA FEKI INAYOSABABISHA SHIDA KWA WANANCHI KAMA UMEME, MFUMUKO WA BEI KUPANDA KWA DOLA NA MENGINE MENGI YANAYOSABABISH HALI NGUMU KWA WANACHI. TUUNGANE TENA TUUNGANE KUMPINDUA MKOLONI MWEUSI.its me toto la kisafwa
ReplyDelete