*Alikuwa ndani ya 'uniform' za jeshi
Na Ramadhan Libenanga, Morogoro
POLISI mkoani Morogoro linamshikilia Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Bulolo James (26) wa kikosi cha 34 Lugalo Dar es Salaam kwa tuhuma ya
kusafirisha bangi gunia 12 akiwa na sare za jeshi hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Adolphina Chialo, alisema mwanajeshi huyo alikamatwa na polisi wa doria saa 8 usiku wa kuamkia jana.
Alisema askari huyo alikamatwa katika Barabara Kuu ya Morogoro Iringa akiwa anaendesha gari aina ya Toyota Mark 2 lenye namba T 602 ABJ likiwa na bangi gunia 12.
Kamanda Chialo aliwataja watu wengine waliokamatwa katika gari hilo kuwa ni Bw.Ally Mustafa (25) na Bw.Idd Said (30) wote wakazi wa Tabata, Dar es Salaam na kwamba askari huyo ni mmoja wa waliotakiwa kushiriki gwaride la maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara kuanzia leo na kilelele kesho.
Alisema askari huyo alikuwa akitoa bangi hiyo Kata ya Mugeta Wilaya ya Mvomero mkoani humo kwenda Jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo alisema uchunguzi zaidi unaendelea ili kupata taarifa zaidi za askari huyo.
Wakati huo huo, watu watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro kwa kosa la utapeli akiwemo Ofisa Usalama wa Taifa.
Wakisomewa shtaka mbele ya Hakimu Mkazi Agnes Ringo, Mwendesha Mashtaka Sinai Mwaseba, alisema washtakiwa wote, Bw.Nicholaus Mgenge (Ofisa Usalama), Bw.George Mweyunga na Bw.Kolelo Fikio wanatuhumiwa kushiriki kosa hilo.
Alisema mtuhumiwa Bw.Mgenge na wenzake wanatuhumiwa kwa kosa la kumtapeli Bw.Awadhi Salehe, kwa kudai kumpatia hati ya kiwanja Plot namba 6 Block N mtaa wa Mindu Manispaa ya Morogoro.
Alidai kuwa Desemba 2, mwaka huu mtuhumiwa Bw.Mgenge alijitambulisha kwa Bw.Salehe kuwa ni Ofisa Uslama wa Taifa kutoka Ikulu (Ofisi ya Rais) hivyo anaweza kufanikisha upatikanaji wa hati hiyo na kupewa sh.500,000.
Alidai siku iliyofuata alirudi tena kwa Bw.Salehe kudai kupewa sh.milioni mbili ili kumwezesha kwenda kushughulikia hati hiyo.
Hata hivyo watuhumiwa wote walishindwa masharti ya dhamana na kupelekwa mahabusu hadi Januari 16, mwaka 2012 kesi yao itakapotajwa tena.
si ajabu kwa wanajeshi kuwa na bangi , kwani hizo ndizo zinawaharibu akili kuweza kuwatumikia wanasiasa kama watumwa na kutesa wananchi. Kwa kawaida wanajeshi wengi hawana shule kichwani ndio maana wakaingia kwenye taaluma hio ambayo ni ya kitumwa haihitaji kufikiri inahitaji kutii amri kama robot.
ReplyDeleteMakosa yanayotendwa na mtu binafsi yanamhusu yeye mwenyewe hayapaswi kuhusishwa na taasisi yoyote anayotokea mtu huyo. Na kwa maana hiyo huyo aliyekamatwa atajibu mashtaka kwa nafasi yake binafsi na kama atatiwa hatiani taasisi anayofanyia kazi zake itamchukulia hatua ipasavyo.
ReplyDeletehahaa ndugu wachangiaji tujaribu kufikiri saana juu ya maneno yetu, hv tz nzima ina wana jeshi wangapi ina maana wote hawana shule? na unaposema jeshi una jua unahusisha nani na nani? jaribu kusemea mtu aliye kutwa na tatizo sio taasisi nzima kwani una mjumuisha hadi kiongozi wako wa nchi ambayo sio busara, kumbuka hadi leo hii unaweza kusema maneno haya kwa madaha tu ni kwa sababu una amani ya kutosha nchini mwako, so usipende kujumuisha na wasio husika, tusiwafikirie vibaya wanajeshi wetu kwani nao ni binadamu kama sisi tusilikuze jambo na kusema mengi kisa tu aliye kutwa na hilo tukio ni mwanajeshi kwani sisi raia tuna fanya mangapi mabaya?
ReplyDeletehuyu mwananjeshi ameshiriki uhalifu kwa nafsi yake binafsi na sio kwa nafasi yake kama mwanajeshi.Itabidi ahukumiwe kama mhalifu mwingine ye yote hakuna uhusiano wa uhalifu anaotuhumiwa kushiriki na nafasi yake kama mwanajeshi. Na kama alitumia cheo chake kufanya maovu nao huo ni uhalifu. Kuna baadhi ya watu ambao ni watumishi wanaotumia nyadhifa zao katika kutenda maovu huku nyadhifa zao zikiwalinda wasionekane wahalifu. Hatuna budi kutii kanunu na maadili ya utumishi kila tunapopewa dhamana ya kuwa watumishi katika sekta yo yote ile.
ReplyDeletewanajeshi wengi hujihusisha na uhalifu na uonevu kwa wananchi , kama mwongo hebu jaribu kuendesha gari lako halafu mbele iwe inakuja gari ya jeshi uone wanavyokuja na mabavu utapata joto yako , subiri uharibikiwe na gari au pikipiki yako kwenye barabara inayopitia kwenye kambi uone mateso utayopata kama vile ulitaka uharibikiwe na chombo chako eneo la jeshi , kuna mke wa mwanajeshi aliibiwa kule visiwani , wanajeshi walikwenda kwenye eneo lile na kupiga kila mtu jee huoni huo ni uonevu? wanajeshi wenye shule ni wachache sana na hawawezi kufanya upumbavu niliouleza kwani wapo ktk nafasi za juu za kitaaluma, wenye kufanya uonevu ni wale limbukeni waliokuwa mbumbumbu shuleni wakapata nafasi ya kuvaa uniform ya jeshi basi ndio imekuwa kama kapewa ufalme.
ReplyDeleteNaona huyo mtu anayesema kwamba wanajeshi hawana shule aombe radhi kwa jeshi zima na anapata nguvu ya kusema hayo kwa sababu ana amani ambayo wanajeshi wetu wanajaribu kuilinda kwa kila hali.Ningependa kumshauritu pengine anapomuhukumu mtu hasimuhukumu kwa kazi yake bali amuhukumu kwa kosa lake,kwani ni raia wangapi wanaofanya matukio makubwa zaidi ya huyo mwanajeshi ? Tuwapendeni wanajeshi wetu kwani bila wao nchi itakuwa pabaya sana na hapo ndipo tutakapotambua umuhimu wao,tuangalie Mbagalaa na Gongolamboto tu hapo juzi nadhani jibu tunalo kwa wale wenye upeo wa kutafakari na kuona mbali.
ReplyDeleteha.. ha..haaa...nashukuru ndugu yangu kwa kukumbushia , si unaona kuwa hawana shule? vipi mabomu yalipuke ovyo na kusababisha maafa makubwa kwa raia kama wamesoma na wanajua kazi yao yangetokea?, mwanajeshi kufariki/kupona ni sehemu ya kazi yake na anatambua hilo. Nchi ingeendelea sana bila ya wanajeshi ambao hupewa mishahara minono japokuwa hawakusoma , wakati walimu,madaktari , manesi n.k wanalipwa mishahara duni. Hatuna haja ya jeshi kubwa kwani hatuwaamini majirani zetu? ikiwa hatuwaamini ya nini kuwa na ushirikiano nao? Jee unatambua kuwa jeshi hawana hata bajeti wanatumbua fedha kadiri wanavyotaka ?
ReplyDeleteWote tuna uhuru wa kutoa mawazo, tuwe na busara tusijumuishe taasisi nzima tunapotoa mawazo, mfano madoctor wa Muhimbili walio fanya upasuaji wa kichwa badala ya mguu hawakusoma? Tuseme madoctor wetu hawajasoma? kufanya makosa haijalishi umesoma au haujasoma ni suala la mtu binafsi au baadhiya manesi wanao tukana wake zetu wanapokwenda kujifungua hawakusoma? au ni taratibu zao zinawaelekeza hivyo? la! wamesoma kwa kiwango chao na taratibu hazisemi wafanye upumbavu wanao ufanya. Halikadhalika aina yoyote ya makosa na upumbavu unaofanywa na mwanajeshi mmoja ni yeye binafsi haijalishi kasoma au hajasoma, aidha taratibu za jeshi zinatoa elimu/ usomi wa kijeshi ambao hauelekezi askari kufanya upumbavu kama huo alioufanya askari huyo.
ReplyDeleteWewe umesoma hicho ulichosoma na askari ameoma mambo ya kiaskari nyote ni wasomi katika nyanja zenu Mungu alivyo wajalia ndio sababu wewe huwezi usomi wa kijeshi na yeye hawezi usomi wako. ni vyema tukaheshimiana na kukemea uovu bila kujali ninani kautenda na bila kujumuisha taasisi nzima kwa kosa la mtu mmoja.
Ndugu uliyetoa lugha mbaya kwa jeshi ni vyema ukaomba msamaha itakuwa ni busara zaidi. Aidha kutoa taarifa za waalifu hata kama ni mwanajeshi amekuonea barabarani tumfikishe mahakamani na uone jinsi sheria itakavyo chukua mkondo wake bila kujali cheo chake.
ASANTE
MASAHIHISHO KAMA YAPO
Ndugu mwandishi wa gazeti la majira ninavyo fahamu mimi RPC wa sasa au Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Afande Adolphina C. anacheo cha SACP na si ACP fanya uchunguzi wako usahihishe kama kuna ukweli ktk ufahamu wangu nijue na wengine wajue pia, katika habari ya mwanajeshi nimeona umeandika cheo chake ni ACP.
ASANTENI KWA KAZI YENU NZURI YA KUTUHABARISHA UMA.
nasikitika kuona kuwa ndugu hapo juu hata hatambui kuwa mahakama na polisi zimejaa rushwa, kesi ya sokwe kuipeleka kwa ngedere, kama kweli sheria ipo wale wanajeshi walioenda kuwapiga raia kule visiwani bila sababu , jee wamefikishwa popote? usiwe kama hujui hatuna sheria hapa, ukienda mahakamani kwa tatizo lako inakuwa ni mradi wa kila mtu mahakamani kupata dezo , makarani , mwendesha mashtaka , wakili wa utetezi na jaji wote wanakula pamoja kwa tatizo lako, kama nadanganya jaribu kwenda mahakamani uone utavyovamiwa kama paka wameona samaki!Nakubaliana na wewe kuwa hao manesi na madaktari wetu WENGI wana matatizo kama ulivyotaja, vivyo hivyo na wanajeshi , polisi na wanasheria WENGI wana matatizo na dhuluma kwa raia.
ReplyDeleteHAPA ndipo Watanganyika Wote tuzidi kuelewa kwa Umakini.Hakuna mtu binafsi anayeitwa UHURU ila kwa pamoja ndio tunao huo uhuru na Amani. Sio kweli kuwa wanajeshi pekee ndio wanao linda nchi hii, ni wote kwa Umoja wetu ndio tunao linda nchi hii. Na hao wanaotumia mali za Jeshi la wananchi/Umma hovyo hovyo na kujiona wao ni zaidi ya wengine sio sahihi kabisa. Pesa wanazolipwa kama; mishahara+posho=senti/shilingi za wanavijiji na watu wadogo wa kila rika wa nchi hii. ikiwa ni pamoja na vifaa hayo magari ya jeshi na vyote.
ReplyDeleteSasa huyo kijana aliyekamatwa na hizo "jani" ametukosea hata sisi tunaoligharimia hilo jeshi. Ahukumiwe kama yeye mtovu wa maadili pamoja na wenzake wote.(Mwanakiji-Isanzu-Isene-Iramba)
TO.Anonymous wewe huna akili wa kwanza kwa sababu sisi wanajeshi ambao hatuna akili tunakupa kiburi cha kusema hivyo kutokana na kichwani hatuna elimu inaonekana wazazi wako walifikia mgambo wa jiji hawakupata nafasi ya jeshi la wananchi
ReplyDeletemimi sio msemaji rasmi wa jeshi lakini nakuelimisha jeshi ni kama taasisi nyingine za serikali ambazo zina majukumu nyeti katika majukumu hayo nyeti jeshi limepewa nafasi ya ulinzi wa mipaka ya ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kulinda raia na mali zao. wakati wa amani jeshi hufanya shughuli nyingi hasa za kusaidia mamlaka za kiraia kama vile kutoa huduma wakati wa majanga na maafa jeshi mfano ujenzi wa miundombinu, matibabu na huduma katika hali ngumu hivyo hutoa huduma hizo kwa asilimia 100 bila kujali jaribu kuelewa jeshi limesheni wataalamu wa aina zote ambao wanaviwango vya elimu za aina zote ikiwa ni pamoja na malecture ambao wapo vyuo vikuu huwajui wewe, madaktari bingwa , marubani ambao wamesoma ndani na nje ya nchi hadi viongozi wa mifano wa nchi hii washauri wao wakubwa katika mbinun za uongozi ni jeshini kua utajua, kwa hiyo wanajeshi hawaishi kwa kuvuta bangi hiyo ni hisia ya mtu ambazo zipo sehemu yoyote ile kwasababu wanajeshi wanaajiriwa wakiwa na akili timamu na sio kuajiri walevi na wavuta bangi na kwa akili ni taasisi inayoongoza kwa wataalamu duniani ni wanajeshi, nafikiri kama kuelewa utaelewa acha kauli zako za mitaani
ReplyDeletena yale mabavu mnayoonyesha mkiwa barabarani na magari yenu jee kama si upumbavu wa limbukeni ni nini? na dhuluma mnazowafanyia raia wanaoharibikiwa vyombo vyao karibu na kambi za kijeshi badala ya kuwasaidia ? na kule visiwani mmoja ndiye alifanya kosa kumwibia mke wa jeshi , mtaa mzima watu wakapigwa huko ndio kuwalinda ? msibabaishe watu wenye akili , wanajeshi wengi ni watu wa dhuluma na kunyanyasa raia hata kama wamesoma hulka za kijeshi huwafanya kama robot vile. Elimu inaondoa ujinga sio upumbavu. jeshi inatumia sehemu kubwa ya kodi zetu walalahoi bila sababu maalum ,kama kweli wana uchungu na nchi na wananchi walitakiwa wawe mstari wa mbele kupunguza matumizi ya serikali kwa kuchukua mishahara na marupurupu madogo lakini kinyume wamekuwa wenye kupenda starehe , pombe na maisha ya juu , halafu wanasema wana uchungu na nchi? kalaga baho
ReplyDelete