Na Esther Macha, Mbeya
MFANYABIASHARA, Bw. Bushaga Masalai (30), mkazi wa Dar es Salaam amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha akiwa chumbani kwake katika nyumba ya kulala wageni
ya High Class iliyopo mjini Tunduma.
Habari za uhakika kutoka eneo la tukio zilieleza kuwa marehemu alifika hotelini hapo Desemba 2, mwaka huu akitoka Dar es Salaam.
Desemba 3, wahudumu walipokuwa katika shughuli zao za usafi katika hoteli hiyo walijaribu kugonga mlango wa chumba hicho alichopanga marehemu lakini haukufunguliwa, kutokana na ukimya huo waliamua kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi saa 6 mchana.
Polisi mji mdogo wa Tunduma walifika hotelini saa 6.30 na kuubomboa mlango huo ndipo walipomkuta Bushanga akiwa amefariki dunia.
Mwili wa marehemu ulichukuliwa na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Tunduma na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya kwa uchunguzi ili kujua chanzo cha kifo cha marehemu huyo ambacho hata hivyo kimetokea katika mazingira ya kutatanisha.
Kifo ni kifo kuna cha ajali,maradhi cha kawaida ilimradi ahadi ikifika ya kuondoka duniani haina kinga,ila hiki ni cha kujitakia kugeuza tumbo lake kuwa kontena ya kubeba madawa haramu ya kulevya!!Ahadi imefika kapasukiwa looh,pole yake
ReplyDeleteKtk gazeti jingine wameandika jina la huyo mtu ni Chambena suez buto,hoteli na daktari alaiefanya uchunguzi ni huyohuyo mbona amjina tofauti?pili kule madawa ya kulevya amekutwa nayo kete 60, huku bado haijulikani na jina tofauti lakini hoteli ni hiyohiyo na kama ni watu tofauti basi hiyo hoteli ichunguzwe kuna namna hapo!!!
ReplyDelete