15 December 2011

Gama kubariki Kombe la Nyerere

Na Mwali Ibrahim

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama, leo anatarajia kufungua mashindano ya kimataifa ya Kombe la Nyerere, yaliyoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA).
Mashindano hayo ambayo yatafanyika katika viwanja vya Hindumandal mjini Moshi na yatamalizika Jumapili.

Klabu zitakazoshiriki michuano hiyo ni Jeshi stars, Magereza, JKT, Shule za Sekondari za  Makongo na Loard Baden Powel,  Kijichi, Tanga Central, Rukwa, Moshi University, KCMC University na Mafunzo, Nyuki na Polisi za Zanzibar.

Nyingine ni KAVC, KCC za Uganda na NCC, KPLC, KBC, STIMA na Youth za Kenya ambapo mashindano hayo yatachezeshwa na waamuzi kutoka katika nchi zote tatu.

Akizungumza kwa simu akiwa Moshi jana, Mwenyekiti wa Kamati ya maendeleo ya TAVA, Alfred Selengia alisema tayari klabu hizo zimeshaanza kuwasili mjini Moshi.

Alisema, mechi ya ufunguzi itachezwa jioni baada ya klabu zote kufika.

"Hatuwezi kupanga ratiba ya mashindano leo (jana) kwa kuwa klabu nyingine bado hazijawasili, tutapanga ratiba baada ya zote kufika," alisema Selengia.

No comments:

Post a Comment