Na Grace Ndossa
WANAFUNZI wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam wamegoma kuingia madarasani kwa muda usiojulikana kushinikiza uongozi wa chuo hicho kurudisha wanafunzi
waliosimamishwa masomo.
Wakizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana baadhi ya wanafunzi walisema kuwa mgomo huo utaendelea hadi wanafunzi waliosimamishwa masomo warudishwe.
Alisema kuwa Novemba 11 wanafunzi waligoma chuoni hapo kushinikiza wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatiwe mikopo lakini baadhi ya wanafunzi walikamatwa na askari na kupelekwa mahakamani kufunguliwa mashtaka.
Baada ya wanafunzi hao kukamatwa na kufikishwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu walifunguliwa kesi ya kufanya mikusanyiko isikuwa halali.
Alisema kuwa baada ya kufunguliwa mashtaka hayo walirudishwa rumande hadi hapo uongozi wa chuo ulipoenda kuwatolea dhamana.
Waliporudi chuoni wanafunzi 35 walipewa barua za kukaa nyumbani hadi hapo kesi itakapoisha ndipo warudi chuoni.
Wanafunzi wengine 15 wamepewa barua za onyo na wengine 8 wamesimamishwa masomo kwa muda wa miezi tisa hadi mwakani.
Bw. Mabrika Mawazo ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa pili alisema kuwa, kama wanafunzi hao wamesimamishwa masomo kwa muda wa miezi tisa wangesimamishwa wanafunzi wote kwani maandamano yalifanywa na wanafunzo wote.
Pia alisema kuwa maamuzi yaliyotolewa na chuo hicho kufukuza wanafunzi hao siyo ya haki bali wangeondolewa wanafunzi wote.
Alisema kuwa hata serikali ya wanafunzi (DARUSO)
imeungana na utawala kukandamiza wanafunzi hao.
Pia alisema kuwa Rais Kikwete anatakiwa kutopewa madaraka ya kuchagua makamu Mkuu wa chuo ili kuondoa siasa vyuoni.
"Rais atakiwa kupewa madaraka ya kuchagua makamu Mkuu wa chuo anatakiwa kuteuliwa na maprofesa wenyewe ili aweze kuwa na nguvu ya kutoa maamuzi,"alisema Bw. Mawazo.
Naye Bw. Ndunguru Francis ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu amepewa barua ya kufukuzwa chuo kwa muda usiojulikana kutokana na kusababisha mgomo chuoni hapo.
Alisema kuwa mgomo uliofanyika chuoni hapo ulikuwa ni wa amani na haukuwa ni wa kutisha hadi wanafunzi kupelekwa mahakamani.
"Tunashangaa hapa chuoni migomo ipo kila leo na mikubwa kushinda hiyo iliyofanya wanafunzi wakamatwe na kupelekwa mahakamani,"alisema Bw. Mrema.
Alisema kuwa yeye binafsi kutokana na barua hiyo aliyopewa ya kukaa nyumbani muda usiojulikana ataendelea kukaa ndani ya eneo hilo mpaka ajue hatima yake.
"Mimi binafsi sitaondoka chuoni hapa mpaka nijue hatima yangu, sitakula wala kunywa,"alisema Bw.Mrema.
Naye makamu mkuu wa chuo utawala Bw.Yunus Mgasa alisema wanafunzi waliosimamishwa masomo wamefuata taratibu na sheria za chuo.
Aliongeza wanafunzi hao hawatarudishwa chuoni kuendelea na masomo hadi hapo watakapomaliza kesi zao mahakamani na wale wanaodai mikopo tayari mikopo yao imeingizwa katika akaunti zao za benki.
jamani nyie watoto,someni mje mpiganie haki yenu uraiani,chuo ni kupoteza muda wenu bure,someni mje mtutetee,mnatuumiza wazazi tunapoona mnagoma kila kukicha.hivi kweli hizo degree mtakazopata kweli zitakuwa za halali iwapo kila siku mpo kwenye migomo?ajira kwenu itakuwa ngumu.
ReplyDeleteBig up guys! Hii serikali yetu inataka purukushani ili ifanye kazi utadhani gari bovu?
ReplyDeleteHawa viongozi wetu hawafanyi lolote la maana labda kukomoana hao wanachuo warudishwe masomoni msiringanishe taaluma na siasa marumbano yenu ndani ya chama (tawala) na bifu zenu zisiharibu taaluma vyuoni. Kila pakitokea mgomo wanadhani wanachuo wakorofi, hawafikiri kuwa sababu ya mgomo huo umetokana na nini. Vyanzo vya migomo yote Vyuoni na mashuleni vinasababishwa na utawala wa vyuo hivyo (wakuu wa vyuo na wakuu wa shule). Daini haki zenu msikate tamaa.
ReplyDelete