01 November 2011

Washauriwa kutumia dawa za asili

Na Mwandishi Wetu

WATANZANIA wameshauriwa kutumia tiba za asili kutibu magonjwa mbalimbali yanayowasumbua badala kutegemea dawa za hospitali na
kwenda nje ya nchi kutibiwa kwa gharama kubwa wakati dawa za asili zina uwezo mkubwa na hazina madhara.

Ushauri huo ulitolewa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa tiba asili kutoka wa Mkoa wa Kagera Bw.Yustas Nyakubaho, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu na faida za tiba asilia katika maonyesho ya wajasiriamali katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

Alisema watanzania wasiwe na fikra potofu juu ya dawa za asili badala yake wabadilike na kuanza kuzitumia kwa matibabu kwa kuwa zina uwezo mkubwa kutibu magonjwa yote kama dawa zinazotolewa hospitalini.

"Watu wengi hawana imani na tiba za asili na tunapowaambia zinatibu magonjwa mbalimbali wanadhani tunawadanganya,"alisema.

Pia alisema watanzania wanatakiwa kutambua kwamba serikali imetoa vibali kwa watoaji wa tiba hiyo na kuwataka kuamini kwamba dawa za asili zina tibu magonjwa mbalimbali.

Aliwataka vijana kujitokeza kwenda katika viwanja hivyo ili waweze kuelimishwa jinsi ya kutengeza dawa za asili.

No comments:

Post a Comment