01 November 2011

Msitegemee ajira serikali -Waziri Simba

Na Agnes Mwaijega

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi.Sophia Simba, amewataka vijana kutegemea shughuli za ujasiriamali ili kujikomboa
kiuchumi na kuondokana na umasikini badala ya kujenga tabia ya kutegemea kuajiriwa na serikali.

Akifungua Tamasha la wanawake wajasiramali (MOWE) yaliyoandaliwa kwa ushirikiano kati na Shirika la Kazi Duniani (ILO) Dar es Salaam jana, Waziri Simba alisema hatua hiyo itawawezesha vijana kuondokana na umasikini.

Alisema hivi sasa nafasi za ajira ni chache ikilinganishwa na idadi ya vijana hivyo dawa ni kuondokana na dhana potofu ya kusubiri serikali kuwapatia ajira wakimaliza masomo yao.

"Nawaomba vijana wajikite katika ujasiriamali ili waweze kupambana na changamoto mbalimbali za maisha," alisema.

Aliongeza kuwa shughuli za ujsiriamali ni muhimu na zinachangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa hivyo kuwataka watanzania kuendelea kujishughulisha zaidi katika ujasiriamali ili taifa liweze kuwa na maendeleo mazuri.

Pia aliwataka wajasiriamali kuzingatia kanuni na taratibu za ujasiriamali ili waweze kuwa na mafanikio makubwa na kuhakikisha wanatumia fursa na huduma mbalimbali zinazotolewa na serikali taasisi mbalimbali ili kuweza kufikia viwango vya kimataifa. 

3 comments:

  1. Asante kwa ushauri wako Mh. Waziri, ujasiriamali ni muhimu sana kwa mtanzania wa leo ambaye serikali yake inagubikwa na ufisadi kwa viongozi wake.(ufisadi uliokomaa)
    Fedha zetu za kodi zinazotumika kifisadi zingetosha kabisa kuwapa maskini wa kitanzania mitaji kwa ajili ya ujasiriamali huo.

    ReplyDelete
  2. Nafasi za ajira sio chache kama inavyosemekana au kuzungumzwa na baadhi ya viongozi wa nchi hii,tena wale wasiopenda kuachia madaraka tangu nchi ipate uhuru, ni vipi kijana wa karne hii apate ajira kama wazee hawana dalili za kustaafu?Hata hivyo nchi yetu inazo fursa nyingi za ajira kwa vijana wake,tatizo kubwa hapa ni usimamizi mbovu wa keki za taifa. kindugu.

    ReplyDelete
  3. maendeleo mazuri hayazalishwi mahali penye mianya ya rushwa na ufisadi,tunahitaji fikra mpya zinazotaka mabadiliko....................!

    ReplyDelete