26 October 2011

Sitta alipuka

*Ahusisha ugonjwa wa Mwakyembe na kulishwa sumu
*Asema kuengulia kwake uspika mkakati wa mafisadi
*Alazimika kubadili namba za simu kukwepa vitisho

Na Tumaini Makene

KATIKA hali ambayo itaibua na kuendeleza mijadala ya kisiasa nchini, Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Samuel Sitta amezungumzia ugonjwa wa Dkt. Harrison Mwakyembe anayetibiwa nchini India unahusishwa kulishwa sumu na kuibua hoja mpya kuwa kuenguliwa kwake kuwania uspika mwaka jana kulitokana na nguvu ya mafisadi nchini.

Akizungumza katika Kipindi cha Dakika 45 cha ITV, Bw. Sitta, alirusha shutuma nzito kwa baadhi ya vyombo vya habari kuwa vimenunuliwa na mafisadi ambao hakuwataja, kwani vyombo hivyo vimekuwa vikimwandika vibaya yeye na wenzake, tofauti na vile vilivyoanza.

Bw. Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, alisema kuwa nguvu ya watu aliowaita mafisadi ni dhahiri ndani ya CCM, lakini akasema kuwa hawatafanikiwa, hivyo, akawaomba Watanzania wasiwaruhusu watu hao kuifikisha nchi mbali. Aliongeza pia kuwa hatarajii kuwania urais mwaka 2015, akisema kuwa wako vijana wengi ndani ya CCM, wanaoweza kuchukua nafasi hiyo na kuirejesha nchi katika mstari.

Ugonjwa wa Mwakyembe

Akizungumzia ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Mwakyembe ambaye anatambulika kuwa ni swahiba wake katika vita dhidi ya mafisadi ndani ya CCM, Bw. Sitta alisema kuwa anashangaa vitendo vya hujuma vinatokeaje, kwani hata yeye amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa, hali inayomlazimisha kubadili namba zake za simu mara kwa mara.

Bw. Sitta anakuwa mtu wa kwanza, kati watu wa karibu na Dkt. Mwakyembe na kiongozi serikalini kuzungumzia kwa uwazi kiasi hicho ugonjwa unaomsumbua mwanasiasa huyo mahiri, ambaye alianza kujipatia umaarufu baada ya kuwasilisha taarifa ya Kamati Teule ya Bunge juu ya kashfa ya Richmond, ambayo ilisababisha serikali kuanguka bungeni, baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu, kisha baraza lote la mawaziri kuvunjwa.

"Nilienda kumuona nyumbani kwake pale Kunduchi Mtongani, kwa kweli nilishtuka sana, mimi na umri wangu wote huu wa uzee kuona mtu akiguswa vumbi linadondoka chini...mkono umevimba, kichwani kuna vitu kama mba hivi akiguswa nywele zinadondoka, mke wake alikuwa amechukua picha ya video akatuonesha...mgongo kwa kweli unatisha.

"Yaani mpaka madaktari bingwa wa hapa kwetu mpaka anaondoka ilikuwa bado haijulikani ni kitu gani...kuna uwezekano wa kitu cha hovyo kuweza kuwa kimefanywa au sumu...mimi nashindwa kuelewa sijui haya mambo yanafanyika namna gani, mimi nimetishiwa sana kuuawa, utaona ninabadilisha sana namba zangu za simu.

"Na mambo haya ni sehemu ya vita hii ya mafisadi na inaonekana dhahiri kabisa katika magazeti yao, magazeti kama...(anataja majina) yanatumika yamekuwa yakituandika vibaya sana sisi...(anataja jina la mmoja wa waandishi waandamizi nchini) ndugu yetu huyu amenunuliwa, gazeti ambalo tulikuwa tunaliamini sasa linatuandika vibaya tofauti na lilivyoanza."

Alisema kuwa nguvu ya mafisadi ni kubwa na inategemea fedha, lakini akasema kuwa ina ukomo wake, akitolea mifano namna viongozi wengine waliokuwa na nguvu za fedha na mamlaka kama Muammar Ghaddaf na Hosni Mubarak walivyoondolewa na wananchi waliochukizwa na matendo maovu ya viongozi hao pamoja na familia zao, wakiwemo watoto, kuchezea rasilimali za umma.

Kutemwa uspika

Kuhusu suala la uteuzi wa mgombea uspika kupitia CCM lililoibua mijadala mkali,
Bw. Sitta alionesha kuwa mchakato huo ulisimamiwa na mafisadi, ambao baada ya kugundua nguvu aliyokuwa nayo mbele ya wabunge wengi kutokana na uongozi wake katika bunge la tisa, waliamua kusema kuwa mgombea wa CCM awe mwanamke, sharti ambalo asingeweza kutimiza.

Alisema kuwa baadhi ya mambo anayofanyiwa na chama chake ni magumu sana kuvumilia, akisema kuwa mengine yanadhihirisha kuwa ni vitimbi vya 'watu haramu' ambao ni mahasimu wake kisiasa.

Alikumbushia namna alivyonusurika kunyang'anywa kadi katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) mwaka 2009, akisema alipuuza mpango huo baada ya kugundua ulikuwa ni uhuni.

"Mwanzoni hakukuwa na suala la viti maalumu katika suala hili (la kuwania uteuzi wa kugombea uspika)...walidhani wataweza kutumia fedha kwa wabunge ndiyo maana tukagombea wengi, lakini wakaona haiwezekani kabisa, nikiingia nitashinda kwa kura, siku moja kabla ya uteuzi ndiyo wakaweka sharti hilo la mgombea awe mwanamke, hilo likanishinda..."

Viongozi roho ya kuku

Bw. Sitta alizungumzia pia viongozi aliodai kuwa wana roho ya kuku, ambao wamekuwa wepesi wa kubadilika wanapoona pesa, hivyo akasema kuwa chama hicho kitakuwa makini katika kuwachuja viongozi wake wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani, mwaka kesho, ambao ndiyo utaonesha sura halisi kinakoelekea ili kiwe tofauti na kilivyo sasa.

Alisema kuwa ana imani na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kuwa ni mtu makini atakayeweza kukisimamia chama hicho kurudi katika mstari kwa kuwashughulikia viongozi wabinafsi.

CCJ na misimamo yake CCM

Alikiri kukifahamu Chama Cha Jamii (CCJ) lakini kwa mara ya pili akakana tuhuma kuwa yeye ni mmoja wa waanzilishi wake, kuwa walikianzisha ili liwe kimbilio lao kutokana na misimamo yao ndani ya CCM baada ya kuonekana ikikinzana na wengine, hivyo kuibua mitafaruku ya kimitizamo juu ya masuala ya msingi katika uongozi.

Alisema kuwa misimamo yake ndani ya CCM haijafikia mahali pa kumlazimisha aondoke katika chama hicho, lakini akasisitiza kauli ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere,  kuwa "CCM si baba wala mama", kuwa iko siku anaweza kulazimika kuondoka iwapo ataona kila analofanya halionekani kuwa la maana na mabadiliko yameshindikana.

Uchaguzi wa Igunga

Alikiri nguvu ya chama kikuu cha upinzani nchini, CHADEMA kuwa ilikuwa kubwa kutokana na kusimamia masuala muhimu kama vile uhusiano uliopo baina ya ukosefu wa uadilifu katika uongozi uliopo madarakani na umaskini wa Watanzania.

"Uchaguzi ulikuwa mgumu kwa CCM. Ulikuwa ni mtihani, hasa kutoka kwa CHADEMA ambao mwaka jana hawa*Ahusisha ugonjwa wa Mwakyembe na kulishwa sumu
*Asema kuengulia kwake uspika mkakati wa mafisadi
*Alazimika kubadili namba za simu kukwepa vitisho

Na Tumaini Makene

KATIKA hali ambayo itaibua na kuendeleza mijadala ya kisiasa nchini, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Samuel Sitta amezungumzia ugonjwa wa Dkt. Harrison Mwakyembe anayetibiwa nchini India unahusishwa kulishwa sumu na kuibua hoja mpya kuwa kuenguliwa kwake kuwania uspika mwaka jana kulitokana na nguvu ya mafisadi nchini.

Akizungumza katika Kipindi cha Dakika 45 cha ITV, Bw. Sitta, alirusha shutuma nzito kwa baadhi ya vyombo vya habari kuwa vimenunuliwa na mafisadi ambao hakuwataja, kwani vyombo hivyo vimekuwa vikimwandika vibaya yeye na wenzake, tofauti na vile vilivyoanza.

Bw. Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, alisema kuwa nguvu ya watu aliowaita mafisadi ni dhahiri ndani ya CCM, lakini akasema kuwa hawatafanikiwa, hivyo, akawaomba Watanzania wasiwaruhusu watu hao kuifikisha nchi mbali. Aliongeza pia kuwa hatarajii kuwania urais mwaka 2015, akisema kuwa wako vijana wengi ndani ya CCM, wanaoweza kuchukua nafasi hiyo na kuirejesha nchi katika mstari.

Ugonjwa wa Mwakyembe

Akizungumzia ugonjwa unaomsumbua Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Mwakyembe ambaye anatambulika kuwa ni swahiba wake katika vita dhidi ya mafisadi ndani ya CCM, Bw. Sitta alisema kuwa anashangaa vitendo vya hujuma vinatokeaje, kwani hata yeye amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa, hali inayomlazimisha kubadili namba zake za simu mara kwa mara.

Bw. Sitta anakuwa mtu wa kwanza, kati watu wa karibu na Dkt. Mwakyembe na kiongozi serikalini kuzungumzia kwa uwazi kiasi hicho ugonjwa unaomsumbua mwanasiasa huyo mahiri, ambaye alianza kujipatia umaarufu baada ya kuwasilisha taarifa ya Kamati Teule ya Bunge juu ya kashfa ya Richmond, ambayo ilisababisha serikali kuanguka bungeni, baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu, kisha baraza lote la mawaziri kuvunjwa.

"Nilienda kumuona nyumbani kwake pale Kunduchi Mtongani, kwa kweli nilishtuka sana, mimi na umri wangu wote huu wa uzee kuona mtu akiguswa vumbi linadondoka chini...mkono umevimba, kichwani kuna vitu kama mba hivi akiguswa nywele zinadondoka, mke wake alikuwa amechukua picha ya video akatuonesha...mgongo kwa kweli unatisha.

"Yaani mpaka madaktari bingwa wa hapa kwetu mpaka anaondoka ilikuwa bado haijulikani ni kitu gani...kuna uwezekano wa kitu cha hovyo kuweza kuwa kimefanywa au sumu...mimi nashindwa kuelewa sijui haya mambo yanafanyika namna gani, mimi nimetishiwa sana kuuawa, utaona ninabadilisha sana namba zangu za simu.

"Na mambo haya ni sehemu ya vita hii ya mafisadi na inaonekana dhahiri kabisa katika magazeti yao, magazeti kama...(anataja majina) yanatumika yamekuwa yakituandika vibaya sana sisi...(anataja jina la mmoja wa waandishi waandamizi nchini) ndugu yetu huyu amenunuliwa, gazeti ambalo tulikuwa tunaliamini sasa linatuandika vibaya tofauti na lilivyoanza."

Alisema kuwa nguvu ya mafisadi ni kubwa na inategemea fedha, lakini akasema kuwa ina ukomo wake, akitolea mifano namna viongozi wengine waliokuwa na nguvu za fedha na mamlaka kama Muammar Ghaddaf na Hosni Mubarak walivyoondolewa na wananchi waliochukizwa na matendo maovu ya viongozi hao pamoja na familia zao, wakiwemo watoto, kuchezea rasilimali za umma.

Kutemwa uspika

Kuhusu suala la uteuzi wa mgombea uspika kupitia CCM lililoibua mijadala mkali,
Bw. Sitta alionesha kuwa mchakato huo ulisimamiwa na mafisadi, ambao baada ya kugundua nguvu aliyokuwa nayo mbele ya wabunge wengi kutokana na uongozi wake katika bunge la tisa, waliamua kusema kuwa mgombea wa CCM awe mwanamke, sharti ambalo asingeweza kutimiza.

Alisema kuwa baadhi ya mambo anayofanyiwa na chama chake ni magumu sana kuvumilia, akisema kuwa mengine yanadhihirisha kuwa ni vitimbi vya 'watu haramu' ambao ni mahasimu wake kisiasa.

Alikumbushia namna alivyonusurika kunyang'anywa kadi katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) mwaka 2009, akisema alipuuza mpango huo baada ya kugundua ulikuwa ni uhuni.

"Mwanzoni hakukuwa na suala la viti maalumu katika suala hili (la kuwania uteuzi wa kugombea uspika)...walidhani wataweza kutumia fedha kwa wabunge ndiyo maana tukagombea wengi, lakini wakaona haiwezekani kabisa, nikiingia nitashinda kwa kura, siku moja kabla ya uteuzi ndiyo wakaweka sharti hilo la mgombea awe mwanamke, hilo likanishinda..."

Viongozi roho ya kuku

Bw. Sitta alizungumzia pia viongozi aliodai kuwa wana roho ya kuku, ambao wamekuwa wepesi wa kubadilika wanapoona pesa, hivyo akasema kuwa chama hicho kitakuwa makini katika kuwachuja viongozi wake wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani, mwaka kesho, ambao ndiyo utaonesha sura halisi kinakoelekea ili kiwe tofauti na kilivyo sasa.

Alisema kuwa ana imani na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kuwa ni mtu makini atakayeweza kukisimamia chama hicho kurudi katika mstari kwa kuwashughulikia viongozi wabinafsi.

CCJ na misimamo yake CCM

Alikiri kukifahamu Chama Cha Jamii (CCJ) lakini kwa mara ya pili akakana tuhuma kuwa yeye ni mmoja wa waanzilishi wake, kuwa walikianzisha ili liwe kimbilio lao kutokana na misimamo yao ndani ya CCM baada ya kuonekana ikikinzana na wengine, hivyo kuibua mitafaruku ya kimitizamo juu ya masuala ya msingi katika uongozi.

Alisema kuwa misimamo yake ndani ya CCM haijafikia mahali pa kumlazimisha aondoke katika chama hicho, lakini akasisitiza kauli ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere,  kuwa "CCM si baba wala mama", kuwa iko siku anaweza kulazimika kuondoka iwapo ataona kila analofanya halionekani kuwa la maana na mabadiliko yameshindikana.

Uchaguzi wa Igunga

Alikiri nguvu ya chama kikuu cha upinzani nchini, CHADEMA kuwa ilikuwa kubwa kutokana na kusimamia masuala muhimu kama vile uhusiano uliopo baina ya ukosefu wa uadilifu katika uongozi uliopo madarakani na umaskini wa Watanzania.

"Uchaguzi ulikuwa mgumu kwa CCM. Ulikuwa ni mtihani, hasa kutoka kwa CHADEMA ambao mwaka jana hawakuweka hata mgombea lakini wamepata takriban asilimia 44 ya kura. Na hii inatokana na vitu wenzetu wanavisema tunapaswa kujihadhari sana, hasa uadilifu.

CHADEMA wamekuwa wepesi kuunganisha ukosefu wa uadilifu na umaskini wa Watanzania ni vigumu kukanusha hili mpaka sisi viongozi tubadilike."

Pia Bw. Sitta alisema kuwa hatashangaa iwapo Watanzania wataandamana kupinga malipo ya Dowans, iwapo serikali italazimika kuilipa kampuni hiyo mabilioni ya tozo inayolidai Shirika la Umeme (TANESCO).kuweka hata mgombea lakini wamepata takriban asilimia 44 ya kura. Na hii inatokana na vitu wenzetu wanavisema tunapaswa kujihadhari sana, hasa uadilifu.

CHADEMA wamekuwa wepesi kuunganisha ukosefu wa uadilifu na umaskini wa Watanzania ni vigumu kukanusha hili mpaka sisi viongozi tubadilike."

Pia Bw. Sitta alisema kuwa hatashangaa iwapo Watanzania wataandamana kupinga malipo ya Dowans, iwapo serikali italazimika kuilipa kampuni hiyo mabilioni ya tozo inayolidai Shirika la Umeme (TANESCO).

21 comments:

  1. Kila mtu analalamika!! Kunyooshena vidole kila siku! Tumechokaa! tuleteeni maendeleo nchini! Tunataka Kasi ya ujenzi wa Barabara ya LAMI Tunduma-Smbawanga-Mpanda-Kigoma iongezekee! Wengine barabara za lami mpaka vijijini kwao! tutakufa bila kuiona hii barabara wakati kodi tunalipa. Mzee Magufuli wasikufunge gavanor kwenye hili!

    ReplyDelete
  2. Ni upumbavu kila kiongozi kulalamika tu pasipo kutoa suluhisho la matatizo yetu wananchi, hali kama hii itaendelea mpaka lini, kiongozi wa nchi analalamika, wanaomfuata wanalalamika, wananchi nao wanalalamika

    ReplyDelete
  3. Jamani, kubadilisha nchi si suala la viongozi peke yao. Kwani wananchi wakichagua uongozi mbovu, watavuna utendaji mbovu! Na ili kupata ciritcal mass yakubadilisha mambo lazima tuongee, tueleweshane, mpaka tukubaliane kwa ujumla wetu kuwa tatizo ni kubwa na linahitaji nguvu ya umma kulibadilisha! Hakuna tatizo lolote linaloweza kutatuliwa lisipoongelewa! Kwa mfano, watanzania wengi vijijini hawajui kuwa kuna ufisadi ndani ya CCM. Hawana habari kabisa tena wanashangaa vyama vya upinzani vimekuwepo kwasababu gani. Watu hawa hawataweza kuunga mkono vita dhidi ya ufisadi kama ufisadi hautapigiwa kelele na kuelezwa kwa kina mpaka umma wote wa watanzania uelewe na kuupinga kwa sauti moja. Watanzania tuache kuwa ndumila kuwili! Wasiposema-tunasema hatupashwi habari au hatulielewi tatizo, wakisema-tunasema waache kulalamika! Hapa, tunahitaji nguvu ya umma na siyo ya wachache. Tumewaachia wachache wapambane kwa niaba yetu (Mimi nampongeza sana Waziri Sitta kwa ujasiri wa kuongea hayo bila kuhofia kuipoteza nafasi yake). Tena wakisulubiwa tunawakebehi na kuwashangaa! Leo hii mpinzani akiteswa na polisi tunamcheka! Hivi kwanini mafisadi dhahiri wanasafishwa na kupewa kura kila kukicha? Wapiga kura tuna matatizo gani? Nadhani watanzania hatujajua vizuri madhara ya kuchagua viongozi wabaya!Tumebweteka tunasubiri maendeleo yaje "ki-katiba" kama tulivyopata "uhuru wa katiba". Hatutaki kuumia hata kidogo ili kuleta mabadiliko! Tunataka mabadiliko yake kimteremko kabisa! Sijui tumeliona wapi hili likiwezekana! Mungu atusaidie!

    ReplyDelete
  4. AMEARIBU SANA SITTA PALE TU ALIPOSEMA ANA IMANI NA MWENYEKITI KIKWETE WAKATI YEYE NDIYE CHANZO CHA MATATIZO YOTE NDANI YA CCM KWA KITENDO CHAKE CHA KUTOKUWA NA MSIMAMO NA HUYO MWENYE MOYO WA KUKU KWA MAONI YANGI NI JAKAYA KIKWETE RAIS DHAIFU KABISA SIJAWAHI KUONA.

    ReplyDelete
  5. Sitta tumekuchoka. kazi yako kuwasengenya wana chichiemu wenzio. kama hupendi madaraka jitoe chichiemu na ukakiibue chichijei. Kila siku mafisadi mafisadi. Hata askofu mkuu wa kanisa la kianglikana amekuponda kwa kusema Lowasa sio fisadi

    ReplyDelete
  6. jamani ni mtu gani wa bagamoyo aliyefanikiwa kuongoza ha mtaa hapa nchini akaleta mabadiliko sasa jakaya anaendana na asili yake fitna,chuki,vinyongo wivu na ugoni

    ReplyDelete
  7. sita ia part of a problem but not a solution...yeye alikuwepo kwenye baraza la mawaziri la mwisho la the real JK.................mwaka 1985.............pia mkapa, makinda, ahmed salim, warioba, tyson n.k walikuwemo...........hadi leo he has been part of the rot now bedevilling our nation...............sasa atadaije mikono yake ni misafi........................hivi hiyo sumu ambayo inamkawiza mwakyembe all this time ni sumu ya kuua panzi nini?

    ukweli ni kuwa hiv is the real deal here and elsewhere....................naniasubiria kusikia naye zitto karogwa na nani........just thinking aloud......

    ReplyDelete
  8. Naomba CCM na Vigogo wake wasifanye fujo nchini. Sitta asilinganishe Tanzania na Libya.Vita ipo kati ya Kada ya CCM. Ndiyo maana wanatishana kuuana. Nitafurahi kama watauana au kulogana wao kwa wao. Wasiifanye vita hii, ya wao kwa wao, eti ni vita ya Wananchi. Na wasidhani eti yeyote atakayechaguliwa kugombea Urais, ndiyo atakuwa Rais. Basi hata Sitta, Lowasa, Kikwete Jr. wakigombea hawaupati Urais!!Chukueni Chenu Mapema ( CCM )mnaondoka safari hii.

    ReplyDelete
  9. Hakuna Mnafiki kama huyo. Alifikiri kiti cha uspika ni wake milele. mwenyewe ni sehemu ya tatizo katika nchi hii

    ReplyDelete
  10. Dr. Hhangali Q. H

    Hakika CCM na Viongozi wake Mafisadi, hawakuwa chaguo la Watanzania.....! Katika Uchaguzi uliopita! Bali, ubabe, uchakachuaji na nguvu ya dola wanazotumia imewapa fursa ya kutawala bila ridhaa ya wananchi wengi...!

    Bila tume huru ya uchaguzi, watanzania hawatampata Rais au Serikali wanayoipenda kwa dhati.

    Nionavyo, uvumilivu utatushinda na kukitokomeza CCM kama KANU ya Kenya...!

    2015 itajulikana hatima ya "CCM", tumechoka kuchakachuliwaaaaa!

    ReplyDelete
  11. mwakyembe atapona tu, kama hamujui kwamba kyela ni mpakani mwa malawi, malawi ndo kisiwa cha uchawi na uganga, wanakyela wote wanashugulika na hawalali usiku kucha, mnakumbuka ya zito na mudhihili,mudhihili alifanyaje, na mpaka sasa yuko wapi?
    sitta wewe ni jembe hapa tz, wote wanaokuponda vibaraka wa rostam na lowassa wake. huyo askofu aliesema lowassa si fisadi, si ndo yule ameomba aludishiwe shule zake? huyo askofu ni njaa tu ndo zinazomsumbua. mwakyembe ungapasyaga sisi wanyakyusa wote tupo nyuma ako Kyala ugwa mmabingo akutulege fijo. n

    ReplyDelete
  12. adhabu ya Mungu inawakabili wanasiasa, kwa kudhulumu haki za wananchi,wanajilipa mishara na marupurupu manene huku mlalahoi akiteseka,hapo mungu anawaonyesha pesa si suluhisho la maisha katika dunia. hakuna uchawi wala kurogwa wala kutiliwa sumu hiyo ni laana ya Mungu mnayoipata,naomba mteseke,mfe.mpate vilema na kila jambo baya liwapate,hata wewe Sitta ni mnafiki tu na usubiri zamu yangu ya adhabu ya Mungu

    ReplyDelete
  13. Kwa kweli nchi hii ina shida kubwa lakini ipo siku tutaingia tu msituni mimi ni ccm lakini vitu ccm tunavyovifanya havifanani na uadilifu.Polisi nao upuuzi mkubwa,wapo watu wanasukumwa tu ndani ya jeshi hilo.Eti chombo cha dola si cha dola ni cha ccm,hilo linakubalika.Ccm kuna viongozi wachache waadirifu lakini wengi ni majangili kabisa.Sitta anasema ukweli na mwaka 2015 mtaona ccm tutashindwa,hata Rais naye ni dhaifu sana tena saana.

    ReplyDelete
  14. Alikiri nguvu ya chama kikuu cha upinzani nchini, CHADEMA kuwa ilikuwa kubwa kutokana na kusimamia masuala muhimu kama vile uhusiano uliopo baina ya ukosefu wa uadilifu katika uongozi uliopo madarakani na umaskini wa Watanzania LAZIMA SERIKALI IKAE CHONJO HASA INAPOONA KIONGOZI MWANDAMIZI ANAONGEA HABARI KAMA HIZO

    ReplyDelete
  15. Ila nchi hii ya Tanzania kuna siku hii amani tuliyonayo itatoweka na patachimbika.kwa walio nacho na wasonacho kwa haya maisha magumu.

    ReplyDelete
  16. Majira nanyi malizeni tatizo lenu la kuendesha gazeti kifamilia hata kwa vihiyo wasio na taaluma. Kumbe alipokufa mheshimiwa mbunge na gazeti nalo likafa. Mbughuni acheni roho mbaya na roho mbaya ya kipare kuendesha gazeti kishenzi. Wapare mna tatizo gani? Angalia kila taasisi yenye wapare ni ukabila na familia. Nenda pale Al nur, Ubungo Islamic Secondary School Kinondoni secondary school mkuu wa shule alipokuwa mpare mmoja mfupi aitwaye mruma. Acheni ushamba na roho mbaya wapare nyie.

    ReplyDelete
  17. Serikali (SIRIKALI ) ya Chama Tawala CCM inahamishia makao makuu yake yawe India. Baraza ra Mawaziri tayari liko huko ( Mwakyembe n.k. )

    ReplyDelete
  18. Samaki moja akioza wote wameoza, sasa ndani ya ccm robotatu wameshaoza inakuaje awepo hata mmoja mzima, adui mwombeee njaa ila me ccm nawaombea sio njaa tu na kwashakoo kabisa wanaharamu nyie, mnawafool watanzania wa vijijini na pesa za wizi simply cuz hawana elimu. death on all ya mofkhaz.Especially kiwete.

    ReplyDelete
  19. Huyo Sitta kichaa. kakosa uspika basi imekuwa porojo kila siku. hata wewe fisadi tu. ofisi yako ya bunge ilitumia mapesa mengi mno. na hata CDA uliiba sana tu sema hakukuwa na muamko kama sasa.

    ReplyDelete
  20. Sita ni kichaaa kabisa ,hivi yeye alipotaka kujenga ofisi ya spika Urambo na baadaye kung'ang'ania nyumba ya spika sio ufisadi huo?Au uspika ni uchifu kwa hiyo alidhani atadumu nao milele?Kweli kafanyiwa uhuni lakini yeye ni mhuni zaidi,kwa usomi wake akugundua kuvunja mkataba wa Richmond ni upuuzi uliolete Taifa hasara?HATUDANGANYIKI CCM NI CCM TU Hamna jipya!

    ReplyDelete
  21. Nahisi maelezo ya Mh. Waziri Sitta ni hisia na fikra zake. Mara nyingi fikra au hisia zinasaidia katika kuleta ukweli. lakini mimi namshauri Mh Sitta aachane na haya maneno ya kujiona kama yeye yuko safi na wengine wabaya.Namuomba akae nje ya Chama ili aweze kutoa mawazo vizuri vinginevyo tutamwita dumilakuwili

    ReplyDelete