14 July 2011

Zitto ataka kamati kuchunguza Meremeta

Na Gladness Mboma

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Bw.Zitto Kabwe amekuja juu na kudai kuwa  ataliomba
bunge liridhie kuundwa kwa kamati teule ya ubunge kwa ajili ya kuchunguza
ubadhilifu
katika kampuni ya Maremeta.
Akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa iliyowasilishwa jana na Waziri Dkt. Hussein Mwinyi, alisema amefikia
hatua hiyo kutokana na suala hizo kuzingumzwa kwa zaidi ya miaka mitano bila
kupatiwa ufumbuzi.
 
Alisema kamati ya Jaji Bomani ilipokuwa ikipitia mikataba ya madini, iliishauri
serikali kulifanyia uchunguzi suala hilo, lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika na
kuongeza kuwa Juni mwaka 2009, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), alitakiwa
kulifanyia uchunguzi suala hilo lakini mpaka sasa hajaeleza chochote.
 
“Tunajua kuwa kuna mambo mengine ya jeshi hayafai kutangazwa, haitasaidia kusema
jambo hili ni usalama wa taifa. Nitatumia kanuni ya 117  kutoa hoja ya kuomba Bunge
liunde  kamati teule kujua ilikuwaje Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuilipa dola
milioni 132 benki ya Nead ya Afrika Kusini,” alisema na kuongeza kuwa haiwekani
suala hilo kuachwa hivi hivi huku jeshi hilo likiendelea kupakwa matope.
 
 Bw. Zitto alimweleza Waziri Mwinyi kuwa atampatia nyaraka zote kuhusu suala hilo,
kwani ana nki hiyo dola milioni 132 ( sh bilioni 216) pamoja na barua ya awali ya
mkopo wa dola 10,000
Meremeta ni moja ya makampuni yaliyotuhumiwa kufanya wizi mkubwa wa fedha za umma
lakini Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, katika Bunge lililopita alizima mjadala juu
ya suala hilo akisema kuwa hiyo ilikuwa ni kampuni ya jeshi na kwamba masuala
yanayogusa usalama wa nchi hayawezi kujadiliwa hadharani.
Aidha, mbunge huyo machachari alisema haionyeshi dhamira ya kweli ya kurudisha
mafunzo ya JKT kwani katika suala hilo zimetengwa sh bilioni 3 ambazo alisema
hazitasaidia lolote.
“Shilingi bilioni tatu zitasaidia nini kwa ajili ya ukarabati wa kambi ambazo
tumeelzwa zitakuwa zinachukua watu 20,000. Skidhani kama kuna dhamira ya kweli
katika suala hili,” alisema.
 
Alisema tangu kusikishwa kwa mafunzo hayo mwaka 1994, kuna vijana wengi mitaani
wasionufaika na mafunzo hayo na kuishauri serikali kuandaa mafunzo maalum ya wiki
nane  kwa viongozi vijana wanasiasa Novemba mwaka huu, ili iwe hamasa kwa vijana
wengine kujiunga na kuongeza kuwa yeye yupo tayari kwenda kwenye mafunzo hayo.
 
Pamoja na hayo,Bw Zitto aliishauri serikali kuanzisha chuo cha ulinzi cha Taifa
(National Defence College) na kwamba atakuwa tayari kuomba kujiunga ili afahamu
jinsi ya kuilinda nchi.
 
Akichangia hotuba hiyo, Mbunge wa Mji Mkongwe, Muhammad Sanya (CUF) ametishia
kuondoka na siwa la bunge iwapo serikali itashindwa kuongeza kiwango cha fedha kwa
wastaafu wa jeshi la polisi.
Alisema wanajeshi wamejitoa kulitumikia taifa, lakini wanapostaafu huishi maisha
magumu kutokana na kulipwa kiwangi kidogo sh 50,000 kwa mwezi ni fedheha.
 “Mwaka huu namesemehe kwa wastaafu kulipwa shilingi 50,000, lakini mwakani
nitaondoka na siwa. Shilingi 50,000 kwa mwezi ni danganya toto kabisa, serikali
iviangalie upya viwango hivi angalau ifike shilingu 150,000.
“Tuangalie sisi wabunge hizo shilingi 50,000 tunatumia kwa siku ngapi? Nilikutana na
mstaafu mmoja aliniambia nyama anakula mara mbili kwa mwaka,”alisema.
Pamoja na hayo, mbunge huyo alishauri wastaafu hao kupatiwa mikopo ili waweze
kufanya kazi ndogondogo na kuwataka kuwa na nidhamu ya kurejesha mikopo hiyo.
Mbali na hilo, alishauri serikali kuwakopesha mabati na viwanja, ili waweze kujenga
kujenga nyumba zao, kwani askari wengi hawana nyumba.
Mbunge huyo pia aliiomba serikali kuwalipa askari malimbikizo yao ya  sh bilioni 49.
Akizungumzia nyumba za askari, aliomba suala hilo lifanyiwe kazi kutokana na
serikali ya watu wa China kuridhia kutoa dola milioni 300, kwani askari kuishi
kambini kutaondoa matatizo mengi.

3 comments:

  1. zito hongera kwa hilo tatizi ni moja watanzania uliopo nao mjengoni hawatetei masalai ya wapiga kura wangekuwa wanafanya hivyo huo mchezo wa meremeta ungekuta umemalizika na watuhumiwa kuwepo ndani. zito, kaza boot tupo pamoja.

    ReplyDelete
  2. Mtoto wa mkulima ameshanogewa na ulaji sasa ameshaanza na kuwasahau hata wapiga kura wake.Hili ndio tatizo kubwa la viongozi wakishapewa madaraka tu huwa wanasahau wajibu wao.

    ReplyDelete
  3. Tunakupongeza mheshimiwa zitto,hawa waheshimewa wanatuona sisi watanzania tumelogwa hatuoni wanachofanya wakumbuke dhambi wanazofanya zitawatafuna wakati ukifika.Mungu ibariki Tanzania tuje kupata viongozi waliobora..

    ReplyDelete