14 July 2011

Banka atupiwa virago Simba Ngwai, Ngade waitwa kikosini

Na Mwandishi Wetu

KLABU ya Simba imeamua kumtema kiungo wake mahiri, Mohamed Banka katika kikosi hicho kutokana na sababu mbalimbali.Habari za uhakika kutoka ndani Kikao cha
Kamati ya Utendaji ya Simba, iliyokutana Dar es Salaam juzi zilieleza kuwa kiungo huyo ametemwa kutokana na kushindwa kuisadia timu hiyo katika michezo mbalimbali.

"Sina uhakika kilichosababisha Banka, kutemwa lakini kuna habari kwamba haendani na mfumo wa Kocha Mkuu, Moses Basena kwa hiyo inawezekana labda ni mapendekezo ya huyo kocha," kilieleza chanzo hicho.

Chanzo hicho kilieleza kwamba baada ya kuamua kuachana na Banka, Basena amewapendekeza Paul Ngwai na Juma Ngade wa Kagera Sugar ili kuiongezea nguvu safu ya ushambuliaji.

Wachezaji hao wanaongezwa baada ya benchi la ufundi kugundua upungufu katika safu ya ushambuliaji kwenye michuano ya Kombe la Kagame kutokana na waliopo kushindwa kutumbukiza mpira kimiani licha ya kupata nafasi nyingi za kufunga.

Licha ya wachezaji hao, pia uongozi huo unatarajia kumsajili mshambuliaji mwingine kutoka Gori Mahia ya Kenya, katika kuhakikisha timu hiyo inafanya vyema kwenye michuano ya Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.

"Kikao kilikubaliana kuwaongeza Ngade na Ngwai ambaye pia humudu nafasi ya kiungo kwa kuwa tuna wasiwasi na Kazimoto (Mwinyi) ambaye aliumia katika mechi na Yanga," kilieleza chanzo hicho.

Katika hatua nyingine, mshambuliaji Felix Sunzu, aliyekuwa akikipiga katika timu ya Al Hilal ya Sudan alitarajiwa kutua jana usiku na kusaini mkataba wa kuitumikia Simba katika msimu ujao wa ligi na michuano ya kimataifa.

Habari zilizopatikana jana zilieleza kuwa uongozi wa Simba, tayari umeshafanya mazungumzo naye kwa kina na kilichobaki ni mshambuliaji huyo kusaini mkataba wa kuichezea.

Chanzo hicha habari kilieleza kwamba uongozi huo wa Simba, umeamua kuachana na mshambuliaji wa SOFAPAKA ya Kenya, Bob Mugalia baada ya timu yake kumwekea ngumu kuja kuitumikia timu hiyo na ndiyo maana sasa wanataka kumsaini mshambuliaji wa Gori Mahia.

4 comments:

  1. TANZANIA TUACHANE NA TABIA NA SABABU UCHWARA UKISHAFUNGWA KUANZA KUFUKUZANA WAKATI USAJILI UMEPITA JUZIJUZI TUU,NI KUHARIBIANA KIMICHEZO.INGAWA BANKA WANADAI KUWA KIPAJI CHAKE NI KIDOGO LKN UKWELI NI KUWA YEYE KASABABISHA GOLI WAKATI KROSI ILIPOPIGWA YEYE ALIINAMA NA KUMWACHA ASAMOH APIGE KICHWA,PIA KUENDEKEZA KUSAJILI WACHEZAJI WAKIGENI WAKATI SISI HAPA KWETU KUNA VIPAJI LUKUKI. TUACHANE NA KUWADHARAU VIJANA WETU NANI WA KUWAINUA KAMA SI TIMU ZETU ZA HAPA NYUMBANI? NA PIA SIJAONA HAO WACHEZAJI WAKIGENI KIKUBWA WALICHOKIFANYA MPK SASA LABDA KIDUCHU HUYO KIPA WA YANGA.TUONDOKANE NA TABIA HIZI

    ReplyDelete
  2. HAYA YOTE YANAKUJA BAADA YA KICHAPO.

    ReplyDelete
  3. ku
    fungwa, kufungwa, kufungwa ni kubaya sana

    ReplyDelete
  4. mlishaanza kuwatukana yanga ah tutawafunga, ah wamebebwa ,ah hawana kitu mkajisahau kabisa kumbe mwenzenu anajifunza kwa adui... haya sasa mtafukuza mpaka aden rage bado kichapo kinakuja shield au ngao ya hisani....3 -0 bisha .

    ReplyDelete