14 July 2011

JKT yalaumiwa kuingia mkataba na mtuhumiwa EPA

Na Gladness Mboma, Dodoma

KAMBI ya Upinzania Bungeni, imeshtushwa  na kitendo Jeshi la la Kujenga Taifa (JKT) kuingia mkataba na Bw. Jeetu Patel kuingiza matrekta nchini wakati  anakabiliwa na kesi ya wizi wa
mabilioni ya fedha kutoka Benki Kuu (BoT) kwenye akaunti ya malipo
ya nje (EPA) na kesi yake bado inaendelea .
Kutokana na hali hiyo Kambi ya Upinzani Bungeni imeitaka serikali kuwaeleza
Watanzania juu ya jeshi kumtumia mtuhumiwa wa wizi wa fedha za walipa kodi kuingia
makubaliano ya kibiashara kwa kutumia udhamini wa fedha za walipa kodi.
Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani –Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Bw.
Joseph Selasini aliyasema hayo bungeni wakati  alipokuwa akitoa hotuba kuhusu
Makadirio ya Mapato na Matumizi  kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012.

“Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi inayoitwa “Public good,rents and business in
Tanzania” iliyotolewa na Bw. Brian Cooksey iliyotolewa Juni mwaka jana inasema kuwa
serikali imetoa udhamini wa sh. Bilioni 40 kwa SUMA-JKT na shirika hili la jeshi
likaingia mkataba na Bw. Patel  kuingiza matrekta hapa nchini , sasa ni kwa vipi
tena jeshi linaingia nae mkataba wa kufanya mabakubaliano na India kwa udhamini wa
fedha za walipa kodi,”alihoji.
Bw. Selasini alisema kuwa taarifa ya Waziri inaonyesha kuwa sh. Bilioni 1.123
zilitumika kwa ajili ya utoaji wa matrekta hayo bandarini na hadi sasa matrekta hayo
yamewekwa Mwenge Dar es Salaam na mengine wameyaona hapo maeneo ya Kisasa Dodoma.
“Swali la kujiuliza ni kweli matrekta haya ni mali ya jeshi au kuna Maofisa wa jeshi
wanafanyabiashara hiyo kwa kutumia jina la jeshi na kama ni mali ya jeshi Waziri
alieleze bunge hili jeshi lilitarajia kupata faida  kiasi gani baada ya kufanya hiyo
biashara ya kuuza matrekta hayo,”alisema.
Alisema kuwa kitendo cha jeshi kujiingiza kwenye biashara ambayo siyo jukumu lake
kimsingi linawatia mashaka  makubwa sana kama kweli jeshi linatumika kufanya
biashara na baadhi ya watu.
“Hoja hii inapata nguvu kutoka kwenye hotuba ya Mheshimiwa waziri wakati
akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya ulinzi  na Jeshi la
Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2010/2011 katika haya ya 24 inayohusu shirika la
Nyumbu
Katika mwaka wa fedha 2009/2010 Shirika la Nyumbu limekamilisha kuandaa mpango
mkakati wake wa muda mrefu ambao una lengo la kuliganya shirika kuwa kituo maalum
cha kuendeleza teknolojia za magari, mitambo ya ndani na nje ya nchi, kufanya
utafiti na uzalishaji mdogo mdogo wa bidhaa na vipuri mbalimbali kwa ajili ya sekta
za ulinzi na usalama,kilimo, viwanda na usafirishaji,”alisema.
Alisema kuwa Kambi ya Upinzani ilitegemea kuwa Jeshi la Wananchi lingeingia mkataba
kwa ajili ya kuimarisha taasisi ya Nyumbu ili iweze kuzalisha vifaa mbalimbali
vitakavyokuwa vinatoa teknolojia rahisi katika mchakato mzima wa uzalishaji wa mazao
ya kilimo.
Bw. Selasini alisema kuwa hiyo sera mpya iliyoletwa  na jeshi na kuhalalishwa na
serikali , yaani jeshi kujiingiza katika masuala ya biashara ya kichuuzi ya kununua
kwa mkopo na kuuza, badala ya jeshi kuwa Taasisi, mfano kwa kuvumbua na kusambaza
teknolojia katika Nyanja mbalimbali za uzalishaji na hivyo kuinua uchumi wan chi
inatia shaka na doa kwa jeshi.

Alisema kuwa hoja hiyo ya jeshi kutumiwa na baadhi ya wafanyabiashara na matapeli
wakishirikiana na baadhi ya Makamanda Wakuu wa Jeshini, imejidhihirisha wazi katika
taarifa iliyotolewa na gazeti la kila siku “Dira ya Mtanzania” la Julai 4-6 mwaka
huu.
Bw. Selasini alisema kuwa kutokana na hali hiyo Kambi ya Upinzani imeitaka serikali
kutoa taarifa ya kina kuhusiana na taarifa hiyo na ni hatua gani za kinidhamu
zimechukuliwa kwa Maofisa hao wa jeshi.

Alisema kuwa taarifa hiyo ni mwendelezo wa taarifa ambazo zilikwisha lalamikiwa na
jamii jinsi ambavyo Bw. Visran Sileshi alivyokuwa akifanya  biashara  haramu na
baadhi ya makamanda wa jeshi na mwisho ilikuwa kwa jeshi kununua vifaa vibovu kwa
bei kubwa sana.

Msemaji huyo wa kambi ya upinzani aliongeza kuwa kwa hali ya kawaida kuna wananchi
ambao kutokana na utundu wao wa asili wanatengeneza silaha kama magobore, lakini
badala ya jeshi kuwachukua wananchi hao na kuwaendeleza, serikali inawafungulia
mashtaka .

Alisema hali hiyo ni kuwafanya wananchi wenye uwezo wa kubuni na kutengeneza baadhi
ya vifaa kuogopa na hivyo vipaji vyao kupotea kabisa jambo ambalo alidai kuwa ni
hatari kwa Taifa dogo kama Tanzania.

Bw. Selasini alisema kuwa usiri ambao unaendelea katika miradi , kampuni ya jeshi
umeendelea kuitia hasara nchi, kwani Kambi ya Upinzani kwa miaka mitano iliyopita
imekuwa ikihoji umiliki wa mgodi wa meremeta na serikali imeshindwa kutoa majibu
sahihi,ambapo Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda aliamua kulieleza Taifa kuwa Meremeta ni
suala la ulinzi na usalama na hivyo ni siri na hakuna mtu mwenye uwezo wa kuhoji
tena na mjadala ulifungwa.

“Usiri huu umewaacha wananchi wa Buhemba ambao hadi muda huu bado walikuwa na madai
mbalimbali dhidi ya kampuni hiyo ya Meremeta . Kambi ya Upinzani inasema kuwa
kampuni hiyo ilikuwa ni ya kibiashara na hivyo bado tuna haki kabisa ya kuendelea
kuhoji ubadhirifu wote uliofanywa na baadhi ya watendaji jeshini  kwa mgongo kuwa
kila jambo ambalo liko chini ya jeshi ni siri na hakuna mamlaka ya kohoji jinsi
linavyoendeshwa,”alisema.

Alisema kuwa kuna usemi unaosema kuwa “no taxation without  representation” kama
ulivyotolewa na Katibu Mkuu wa Inte-Parliamentary Union, Bw. Anders John pamoja na
Mkurugenzi wa Geneva Center for Democratic control of armed forces, Balozi Dkt.
Theodor Winkler .
Bw. Selasini alisema kama bunge linapitisha fedha za walipa kodi kwa matumizi  ya
taasisi za jeshi, ni lazima wawakilishi wa wananchi ambao ni wabunge waelewe nini
kinafanyika na wawe na mamlaka ya kuhoji matumizi ya fedha hizo.

“Hivyo basi kaulia aliyotoa Waziri Mkuu bungeni kuwa suala la Meremeta  limefungwa
na halitakiw kuhojiwa tena kwa kuwa ni siri ya jeshi halina mashiko na ni utetezi
dhaifu, kwani kumbukumbu zinaonyesha kuwa kampuni  hiyo ya jeshi ilianzishwa kwa
fedha za wananchi na wabunge ni wawakilishi wa wananchi.
Bw. Selasini alisema kuwa pia kumekuwepo na matumizi mabaya ya vifaa vya jeshi kwa
matumizi ya kisiasa na binafsi  ya wanasiasa, jambo ambalo limeendelea kuongeza
gharama kwa jeshi hilo  na kwamba mifano hai ni mwaka juzi zilitolewa taarifa za
kuanguka kwa helikopta ya jeshi mkoani Manyara iliyokuwa imebeba wazungu waliokuwa
kwenye ziara binafsi kwa idhini ya ya Waziri wakati huo Professa Juma Kapuya.
Alitoa mfano mwingine ni ule wa juzi, ambapo ndege ya jeshi ilitumika kumsafirisha
Mwenyekiti wa CHADEMA, Bw, Freeman Mbowe kwenda Arusha kutekeleza amri ya mahakama
na ndege hiyo ilirudi ikiwa na rubani pekee , kwamba hayo ni matumizi mabaya ya
rasilimali za Taifa na halikubaliki.

Bw. Selasini alisema kuwa Kambi ya Upinzani inaamini kwamba kwa njia ya utunzi wa
sera na sheria  za ulinzi zitakazotungwa zitakuwa zimewahusisha wanachi  kwa kiasi
kikubwa na zitasaidia kuondoa migongano isiyokuwa na tija kati ya jeshi na wananchi
ikiwa ni pamoja na kuondoa kabisa matumizi mabaya ya askari wa jeshi katika
kushughuli za kisiasa kama ambavyo imekuwa ikijitokeza katika hatua mbalimbali za
mchakato wa uchaguzi.

10 comments:

  1. HIYO YA MATREKTA NI DEAL KATI YA KIKWETE. LUTENI GENERALI SHIMBO (MANDHIMU WA JWTZ) NA JEETU PATEL. WATATUMIA UMBUMBUMBU WA WANAJESHI WA TANZANIA KUPIGA DEAL ZAO. WANAJESHI WAO WAMEBUNG'AA TU. WATUNGUENI. AU NDIO NIDHAMU YENYEWE???? KAZI IKO.

    ReplyDelete
  2. LUTENI GENERALI ABDULRAHMAN SHIMBO, LUTENU KANALI JAKAYA KIWETE NA MTUHUMIWA KURUTA JEETU PATEL NDIO WENYE DILI YA MATREKTA KWA FAIDA BINAFSI. HIVI HAKUNA WANAJESHI WAZALENDO SIKU HIZI TANZANIA YA JULIUA NYERERE??

    ReplyDelete
  3. HIVI NYINYI WAPUMBAVU AMBAO KILA ISSUE MBAYA INAYOTKEA BASI NI LAZIMA MUMUINGIZE RAIS KIKWETE MBONA MAZURI ALIYOYAFANYA HAMUONGEI AU KWA KUWA NI MUISLAMU? HEBU ACHENI UDINI WENU HUO.

    ReplyDelete
  4. we Said acha uzezeta, sasa hapo dini inaingiaje? uislam kazi yake ni kununua matrekta? hayo ni mawazo mgando kabisa, mdini mkubwa wewe, baradhuli

    ReplyDelete
  5. wizu ntupu hivi ninyi viongoi mmekuwa vipofu kiasi hicho yaani tuhuhumiwa na mwizi kisha deal na serikakali. Tuambieni ukweli kama wizi ni kushurikishana madili na serikali ili watuhumiwa wote walopo maabusu nao waweza kufanya del za kuachiwa maana hkuna sababu ya kutuhumiwa kama serikali inaweza fanya deal na wezi kama ilivyofanya kwa Jitu patel

    ReplyDelete
  6. ukimuona mtu ktk mjadala wowote ule anaingiza ukabila, udini, ukazi na kadhalika basi achana naye ujue ameishiwa hoja usipoteze mudana watu kama hao huwa hawana hoja.tamka wewe hayo mazuri unayoyajua kayafanya kwanini unatulazimisha sisi kutamka mazuri aliyoyafanya JK hatuyaoni hayo mazuri tukilinganisha na mabaya aliyoyafanya mazuri yote yanafutika. uchumi wa nchi unadidimia dola ilikuwa shs.1000 anaingia sasa hivi 1600, maisha yanazidi kuwa magumu na maskini wanaongezeka kila siku hayo ndio mazuri aliyoyafanya jk umefurai sasa.

    ReplyDelete
  7. Hivi serikali pekeyake kama serikali ilishindwa kuagiza hayo matrekta mpaka imtumie jeetu patel?.Mtu ana kesi ya wizi wa mamillioni ya serikali alafu bado tena anapewa kazi nyingine tena ili aweze kuiba tena mamillioni mengine kupitia kwenye mgongo wa viongozi walafi.Kwanza kwanini jeetu patel asishitakiwe na kufilisiwa mali alizonazo?

    ReplyDelete
  8. kikwete kafanya lipi lizuri??? au unaropoka tu??? kizuri hakiitaji kutangazwa.....ulimuona mkapa akijitangaza?jumuia za nje zinamjua na kumuheshimu...sasa masikini huyu mtalii wenu nani anamheshimu? zaidi ya kumdharau? nyumbani kwake yenyewe ishu ndogo kama kuzuia mfumuko wa bei kashindwa,, umeme ndo balaa kabisa....acha habari za udini angalia facts.....amedeliver nini?au mafanikio mnayaongelea huko kwenye nyumba za ibada? hatuoni lolote zaidi ya kuwa amekuwa mtalii tu..na hana jipya!!!tunataka rais wa watanzania sio wa waislam au wakristo....THINK BIG kama una akili timamu...inchi haiendeshwi kwa sala 5...inaenda kwa facts na utendaji

    ReplyDelete
  9. Huyu alieingiza udini ni sawasawa na wale wanyamwezi wetu waliolia na wanalia eti Rostam Aziz kajivua gamba!
    Yaani hawajui uhujumu uchumi ambao hawa viongozi wabovu wanafanya, kazi ya udini, mara uislam mara ukristu!
    Kwanza wakumbuke uislamu na ukristu wala sio asili ya mbantu, uislamu uliletwa na waarabu, wakaishia kutufanya watumwa, wazungu nao ukristu wao wakaishia kututawala na kutufanya kuishi maisha kama yao.
    Kuna watanzania wako bure kabisa mpaka unawahurumia kwa jinsi zinavyofanya kazi.
    Kwaio kama mtu fisadi na ni muislamu wewe kama muislamu hutaponda? Au kwa ukristu nao utafanya hivyo?
    Tusikumbatie dini za wenyewe na kuficha maovu ya viongozi wetu hapa!

    ReplyDelete
  10. Nimesoma mijadala yenu, haina la maana zaidi ya kuona makengeza....nawashukuru mmejaribu. kikubwa hapa ni ushirika wa serikali na mtu anayetuhumiwa kwa ufisadi....macho yenu kwakuwa yapo ndani ya nchi moja yaana Tanzania, ipo hatari kubwa. vema mkatoka japo kwa mitandao mkaona kilichopo nje. mtaweza kujadili mijadla yenu vema kabisa.

    sasa nasema hivi, HAKUNA kiongozi aliyethubutu kuwafichua na kuhakikisha wanachukuliwa hatua za kisheria kama JK, HAKUNA kiongozi aliyethubutu, kugawa haki ya kimaendeleo pande zote za nchi kama JK, HAKUNA kiongozi aliyethubutu kutetea wanyonge kama JK. Najua mtakurupuka na kunena ovyo, lakini huo ndio ukweli siku nyingine nitawapasha zaidi sasa wakati wa kulala umefika..samahani

    ReplyDelete