21 July 2011

TGLU yaandaa michuano ya wazi ya gofu

Na Mwali Ibrahim

CHAMA cha Gofu cha Wanawake (TGLU), kimeandaa  mashindano ya wazi ya mchezo huo'Tanzania Ladys Open, yatakayofanyika Agosti 20 hadi 21, katika viwanja
vya Gimkhana, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa TGLU,  Mbonile Barton, alisema wachezaji wanawake 80  watashiriki mashindano hayo, ambapo amewataka wachezaji wanawake na wanaume kujitokeza kwa wingi  kushiriki mashindano hayo.

Alisema, wanaume katika mashindano hayo watashiriki kama wasindikizaji, hivyo yatakuwa na wachezaji zaidi ya 150.

"Tunataka kuchangamsha mashindano, ndio maana tumewaalika wanaume ingawa walengwa zaidi ni wanawake,  mashindano haya ni ya wazi, hivyo wanaume watacheza kama wahamasishaji," alisema mbonile.

Alisema nchi zinazoshiriki mashindano ya Kombe la Challenge Afrika Mashariki na Kati, zimealikwa kushiriki mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment