19 July 2011

Rais Kikwete aanza ziara ya kidola Afrika Kusini

Na Rachel Balama

RAIS Jakaya Kikwete, jana ameanza ziara ya kidola siku nne nchini Afrika Kusini ambayo ni ya kwanza kufanywa na Rais wa Tanzania nchini humo.Taarifa iliyotolewa
na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, inasema ziara hiyo ya kihistoria imetokana na mwaliko wa Rais Jacob Zuma wa nchi hiyo ambaye utawala wake umekuwa na uhusiano mzuri na Tanzania tangu aliposhika madaraka ya kuongoza Taifa hilo.

Rais Kikwete ambaye ameongozana na ujumbe wake akiwemo mkewe Mama Salma, waliondoka nchini jana mchana kwenda nchini humo katika Jiji la Pretoria.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, pamoja na marais waliotangulia nchini Tanzania, waliwahi kutembelea nchini humo kwa shughuli mbalimbali lakini hakuna Rais wa Tanzania ambaye aliwahi kualikwa kwa ziara rasmi ya kiserikali au ya kidola tangu nchi hiyo  iingie katika mfumo wa demokrasia mwaka 1994.

Rais Kikwete pia atafanya mazungumzo ya kiserikali Rais Zuma, kutiliana saini mikataba ya makubaliano katika nyanja mbalimbali, kufanya mkutano na waandishi wa habari na kutembelea Uwanja wa Uhuru akiwa na mwenyeji wake.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa, viongozi hao pia watakula chakula cha mchana na wafanyabiashara wa Tanzania, Afrika Kusini na kufanya mazungumzo ya pamoja ili kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya nchi hizo.

Rais Zuma ataandaa dhima ya kitaifa kwa ajili ya Rais Kikwete na ujumbe wake kwatika nyumba ya wageni nchini humo.

Julai 20 mwaka huu, Rais Kikwete na ujumbe wake watakwenda Cape Town nchini humo ambapo watatembelea kisiwa cha wapigania uhuru wa Afrika Kusini ambao walifungwa kwa miaka mingi na Makaburu akiwemo Rais mstaafu Bw. Nelson Mandela kinachoitwa Robben.

Rais Kikwete na ujumbe wake, watarejea nchini Julai 21 mwaka huu.

7 comments:

  1. Huyu jamaa bado miguu inamwasha. Aje nyumbani akakumbani na matatizo ya umeme, aache utalii

    ReplyDelete
  2. Watanzania wanakufa njaa, wako gizani lakini bwana mkubwa anarukaruka na ujumbe wake kupondo hela ambazo zingeweza kubadili hali ya nchi. Hana huruma hata kidogo na maisha ya mtanzania.

    ReplyDelete
  3. Never seen or heard of a President who travels so much. Hajari matatizo ya bongo, yeye in safari tu. Can anyone give us the number of safaris he has made since last year and what benefit have they brought to the local poor mtanzania. Watanzania amkeni, next time vote mchapakaji.

    ReplyDelete
  4. INASIKITISHA KUONA RAIS WETU HAJALI YEYE NI KUPONDA STAREHE TU. KWANI ILIKUWA LAZIMA AENDE KIPINDI HIKI KIGUMU KWA NCHI YAKE. USANII WINGI!!!!!!!!!!!!!SHAME.

    ReplyDelete
  5. Mawaziri wanatoa rushwa ili bajeti zao feki zipite lakini hakuna kinachofanyika, Rais mwenyewe kila siku yupo nje ya nchi, kwani hiyo ziara ina manufaa gani kwetu watanzania?

    ReplyDelete
  6. It is a sad situation, the man cares nothing about his country!! when is his next trip - probably to West Indies, great hotels there na pwani nzuri sana, Go Kikwete. Lets remember that we voted for him, so let him enjoy and utilise hopelessly the presidential jet.

    ReplyDelete
  7. Kikwete safari zako sasa zimepita kikomo hivi huko unakokwenda kila siku na kutumi mamilioni ya shilingi za walipa kodi hizo fedha nafikiri zingeweza kufanya kitu kingine cha maana.sasa hivi unatakiwa kukaa na viongozi wenzako na kutafuta suluhisho la umeme alafu ndio uende nje kutafuta wawekezaji.Maana unaoneka hujui unachokifanya wakati nchi yako haina umeme wa kutosha halafu unaenda kutafuta wawekezaji sijui waje kuwekeza wapi ambapo hakuna umeme.Mkizarauliwa kwa sababu ya mipango mibovu mnakasirika.Haya maliza huo utaii halafu urudi nyumbani kuja kutoa maamuzi ya Wizara ya nishati na madini alafu wakingie kifua na hao waliofanya hayo madudu na ushaidi wa kutosha upo.

    ReplyDelete