19 July 2011

Mwanamke afyekwa miguu, kiganja cha mkono wa kulia

Na Hellena Magabe, Tarime

MKAZI wa Kijiji Nyabiroga Songa Bunchari, Wilaya ya Tarime, mkoani Mara, Bi. Agnes Chacha (25), amefyekwa miguu yote miwili pamoja na kiganja cha mkono wa kulia
na mumewe Bw. Chacha Hamis, ambaye amekimbia kusikojulikana.

Tukio hilo limetokea juzi usiku ambapo Bi. Chacha, anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya hiyo wodi namba sita.

Akisimulia mkasa huo, Bi. Chacha alisema siku ya tukio, alifika nyumbani kwake usiku saa mbili akitokea katika biashara yao ya duka na kuwaagiza watoto wake wakanunue unga wa muhogo kwa wifi yake lakini watoto hao waliogopa kwa sababu ilikuwa usiku.

“Nilibandika maji ya ugali jikoni na kwenda dukani mwenyewe, baada ya kununua unga na kurudi nyumbani, nilimkuta mume wangu akiwa nje na panga, alinitaka nimwambia usiku ule nilikuwa wapi wakati aliniona nimebeba unga.

“Mimi nina mimba ya mwezi hivyo napendelea kula ugali wa muhogo kuliko ule wa mahindi, baada ya kujieleza mume wangu hakutaka kunisikia, aliendelea kuniambia nilikuwa wapi,” alisema.

Aliongeza kuwa, baada ya kuona mumewe ameshikilia msimamo huo, aliamua kumwambia alikuwa na kinana aliyemtaja kwa jina la  Muhiri ambaye mumewe anahisi ni mpenzi wake kutokana na maneno anayoambiwa na watu.

Alisema mumewe Bw. Hamis aliwahi kufungwa kipindi cha vita ya koo na baada ya kurudi uraiani, watu walimwambia mkeo ana uhusiano wa kimapenzi na Muhiri.

Bi. Chacha alisema kutokana na majibu hayo, mumewe alianza kumkata kwa panga mbele ya watoto wake ambao walipiga yowe ambapo watu walikusanyika na kumuwahisha hospitali.

“Kama Mungu atanijalia uzima na kupona, nitarudi kwa mume wangu kwani kama ataishi na mke mwingine, watoto wangu watanyanyasika, kutokana na ulemavu huu siwezi kupokelewa na mwanaume mwingine,” alisema.

Muuguzi wa zamu katika wodi hiyo ambaye hakupenda kutajwa jina lake, alisema wauguzi waliokuwa zamu usiku waligoma kumtibu Bi. Chacha ambaye hakuwa na PF3 kutoka polisi pia alikataa kueleza mazingira ya tukio hilo hivyo matibabu ameanza kuyapata jana asubuhi baada ya polisi kufika hospitali na kumchukua maelezo.

Wagonjwa waliolazwa katika wodi hiyo, walisema Bi. Chacha ametoroka hospitali na kuamua kwenda kwa dada yake baada ya mumewe kwenda kumuangalia asubuhi na kumwambia akitoka hospitali asirudi nyumbani kwani atamuua.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya, Deusdedit Katto, hakuweza kupatikana katika simu ili kuelezea tukio hilo.

2 comments:

  1. sijawahi ona ujinga kama huu! Nilishangaa kule Ugana mwanamke analazimishwa kunyonyesha vitoto vya mbwa na mumewe anadai ni haki kabisa, kisa mahari! leo hii hapa kwetu kuna upuzi kama huuna mtu bado analilia mapenzi tu! na Janadume bado linatamba tu! Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni!

    ReplyDelete
  2. majibu ya huyu mama hayajaenda shule, alijibu kwa jeuri, ana unga, jibu tu nimetoka kununua unga, lakini yeye alimpandisha mumewe hasira kwa jeri yake ya kujibu kwamba alikuna na kinana (hawara yake anaye tuhumiwa kuwa naye pindi mumewe apolikuwa hayupo). sasa amepata mshahara wa majibu yasiyo na busara, na kwa ujinga wake zaidi, ametoroka hospitalini, vile vile anadai kurudi kwa hyo mume. Mtu kama huyu muacheni akafie kwa mumewe, na ale jeuri yake. Mnahangaika naye wa nini huyu, wakurya si watu wa kuzoea wala kuhurumia, karibu wote akili zao mbovu haziendani na ustaarabu wa dunia na hawana utu. Wanayo majibu yasiyo na diplomasia ya kienyeji, hawana mila nzuri wala desturi. Mimi sioni kwa nini ahurumiwe, wamezoea hawa, bila mapanga hawaendi. Waacheni wakatane, ndiyo mapenzi yao hao.

    ReplyDelete