03 March 2011

Bukoba wafurika maandamano ya CHADEMA

Na Suleiman Abeid, Bukoba

PAMOJA na Rais Jakaya Kikwete juzi kuwaomba wananchi kususia maandamano yanayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), maelfu ya
wakazi wa mji wa Bukoba na vitongoji vyake jana wamepuuza ushauri huo na wamejitokeza kwa wingi kushiriki maandamano hayo.

Hata hivyo msafara wa viongozi wa CHADEMA ukiongozwa na Katibu Mkuu wake, Dkt. Willibroad Slaa ulichelewea kuwasili mjini Bukoba kutokana na kiongozi huyo kukamatwa na kuhojiwa na polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa saa kadhaa.

Polisi jana saa 1:15 asubuhi walimkamata Dkt. Slaa pamoja na wabunge wawili wa viti maalumu, Bi. Chiku Abwao na Bi. Rachel Mashishanga wakituhumiwa kwa kosa la kufanya mkutano katika eneo la Malampaka wilayani Maswa ambao haukuwa na kibali cha polisi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Bw. Diwani Athumani alisema jeshi lake liliamua kumkamata Dkt. Slaa na wabunge wawili wa viti maalumu ambao walihojiwa kutokana na kitendo hicho cha kufanya mkutano katika eneo hilo bila kibali kwa kuwa wangeweza kusababisha kutokea kwa uvunjifu wa amani.

Kamanda Athumani alisema baada ya mahojiano ya takriban saa moja na robo viongozi hao waliachiwa na kuendelea na msafara wao kuelekea mkoani Kagera ambako waliendelea na ratiba yao kama kawaida.

Viongozi wa CHADEMA kwa upande wao walikanusha madai ya kuendesha mkutano pasipo kibali kwa vile kila mkoa wanakopita kufanya maandamano ya amani na mikutano ya hadhara hutolewa kibali kwa wilaya zote za mkoa husika.

Dkt. Slaa alisema anazo habari zilizodai kwamba kukamatwa kwao haikuwa sababu ya tatizo la kibali bali ni katika juhudi za kutaka kuvuruga ratiba za shughuli ya maandamano ya amani na mkutano mkubwa wa hadhara uliokuwa umeandaliwa kufanyika mjini Bukoba jana mchana.

Alisema mipango hiyo inatokana na shinikizo la Balozi Khamis Kagasheki, ambaye ni mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi kutaka kukwamisha maandamano hayo yasifanyike katika jimbo lake, baada ya njama za awali za kuwazuia vijana waendesha pikipiki na baiskeli kushiriki katika maandamano
kukwama.

Mbali ya tukio hilo la kukamatwa kwa viongozi hao wa CHADEMA, maelfu ya wakazi wa mji wa Bukoba walijipanga kuanzia eneo la Kemondo Bay ambako ndiko walikowapokea viongozi hao na kuandamana kwa msafara wa magari, pikipiki na baiskeli hadi eneo la Rwamishenye ambako maandamano ya kutembea kwa miguu yalipoanzia.

Maandamano hayo yalipita katika mitaa mbalimbali ya mji wa Bukoba na kuishia katika uwanja wa Uhuru katikati ya mji huo ambako shughuli zote za kibiashara zilisimama kwa muda kabla ya Bw. Mbowe na Dkt. Slaa kuwahutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi.

Akihutubia katika mkutano huo, Dkt. Slaa aliwashukuru wakazi wa mji wa Bukoba na vitongoji vyake kwa kupuuza wito wa Rais Kikwete na kujitokeza kwa wingi na pia kwa jinsi walivyoshiriki katika maandamano ya amani.

Alisema wakazi wa Bukoba wameonesha jinsi gani ambavyo wanakiunga mkono CHADEMA kwa vile ndicho chama ambacho hivi sasa kinaonesha wazi nia halisi ya kuwakomboa Watanzania katika kupigania haki zao.

Hata hivyo alisema amepata taarifa ya kufanyika kwa ziara ya Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda ambapo aliwaomba wajitokeze kwa wingi katika mkutano utakaohutubiwa na Bw. Pinda, na wamuulize kuhusu fedha za Watanzania zilizopotea katika mazingira ya kifisadi ikiwa ni pamoja na zile zilizochotwa na kampuni ya Meremeta zaidi ya sh. bilioni 155.

Ndugu zangu mimi nakupongezeni sana kwa jinsi mlivyotuunga mkono katika uchaguzi mkuu uliopita, pamoja na mlivyoshiriki katika maandamano ya amani na mkutano wa hadhara leo hii (jana) bila kujali vitisho vya Rais Kikwete.

Rais wetu ni mtu wa ajabu ni sawa na kinyonga, anasahau sana, awali alikuwa akivilaumu vyama vya upinzani kwamba haviendi vijijini ambako ndiko waliko wananchi, lakini leo tumekwenda anapata hofu na kutaka kutuzuia kwa kisingizio kuwa tunawachochea Watanzania kufanya vurugu,รข€ alieleza Dkt. Slaa.

Alisema CHADEMA haiwatii hofu Watanzania bali CCM na serikali yake ndiyo inayowatia hofu kutokana na kuwakumbatia matajiri wanaomiliki biashara zote kubwa na kupandisha bei za bidhaa ovyo na hivyo kupanda kwa bei za vitu kila siku na Watanzania kukabiliwa na ugumu wa maisha.

Alisema Rais Kikwete na waziri mkuu wake Bw. Pinda wanapaswa sasa kutoa majibu yote yanayoulizwa na Watanzania kuhusiana na ugumu wa maisha, Meremeta, Kagoda na Mwananchi Gold Mine ambazo zote kwa pamoja zimechota zaidi ya moja ya tano ya bajeti ya nchi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Taifa, Bw. Mbowe alisema pamoja na kupinga suala la malipo ya Dowans, lakini huenda chama chake kikawahamasisha wananchi kuingia tena mitaani kupinga mkataba mwingine unaofanana na ule wa Richmond ambao serikali inatarajia kuingia tena kwa kipindi cha miezi minne.

Bw. Mbowe alisema serikali hivi sasa inakamilisha mchakato wa kuingia mkataba mwingine mfano ya ule wa Richmond, ambapo itakodi mitambo ya kuzalisha umeme kwa kipindi cha miezi minne kuanzia Julai mwaka huu ambapo kila mwezi itakuwa ikilipa sh. bilioni 400.

Ndugu zangu serikali yetu inatushangaza, hivi sasa inajipanga kuingia mkataba mwingine wa kifisadi wa kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme kwa gharama ya sh. bilioni 400 kila mwezi ambapo pia itakuwa ikilipa sh. bilioni 23 kwa ajili ya kununulia mafuta, sasa hii tunaikataa pia, alieleza Bw. Mbowe.

Leo viongozi wa CHADEMA wanahitimisha ziara yao katika mikoa ya kanda ya Ziwa ambapo pia kitatoa tamko rasmi kuhusiana na hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa mwishoni mwa mwezi uliopita akiituhumu CHADEMA kutaka kuchochea vurugu nchini.

22 comments:

  1. CHADEMA KWELI MPO JUU RAIS AMETETEMEKA PAMOJA NA WASIRA WAKE ALIENUNUA UONGOZI BUNDA,NAFIKIRI SALAMU HIZO WANAZIPATA TUNAWASUBIRI MJE NA HUKU KANDA YA KATI.

    WATANZANIA TULIHITAJI CHAMA PINZANI CHENYE NGUVU TUKIPE MADARAKA MUDA MUREFU LAKINI TUNAMSHUKURU MUNGU KUSIKIA KILIO CHETU NA KUTULETEA CHADEMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!!!1HAKIKA CHADEMA NI JIBU YA NGUVU YA MUNGU.

    ReplyDelete
  2. “I taught them leadership principles. I taught them to respect authorities. I taught them to respect and obey their parents. I taught them to strive for personal excellence. I taught them responsibility and accountability. I taught them to exercise servant leadership and I taught them that the community and the country is more important than politics and parties. I challenged them to study hard, work hard and be an example for the youth to follow. And as I looked into the excited eyes of the young leaders who loved the session, I silently prayed to myself that this generation would rise up to make a difference in their community and make this country a better place. The innocence and idealism of the young should not be corrupted by the greed and malice of their seniors. This should not be.” BY FRANCIS K.KONG
    Watoto wetu wa leo wanaangalia jinsi taifa linavyosulibiwa na wachache, ni matumaini yangu kuwa kizazi chetu hiki kibaya kilicholaaniwa na wimbi la ufisadi na uroho wa ikulu tutakapoondoka wote kwenda kwa Bwana nchi hii itageuka kuwa kimbilio la mataifa mengi. Slaa na Kikwete (CCM NA CHADEMA) tumieni busara kuepusha maafa na tuishi kwa amani ya uchumi na utulivu wa roho. Wote mna makosa na wote mko right,kwa watoa maoni: hakuna maoni yasiyo na faida, yote ni mawazo hata mnazoziita pumba unaweza kupata chenga. You can not force me to be CCM or CHADEMA all are idealism, at the end of the day all are majizi! Ask them how they got their money to to put up investment? wengi ni majizi: Chadema na CCM, the differece is the same.Nitumie upinzani wako kwa email yangu:
    bartolamiesha@yahoo.com

    ReplyDelete
  3. Inaonekana tumefikia ukomo wa CCM iliyotutenda hivi! Miaka 50 baada ya uhuru, rais wetu bado anatuzungumzia kudra za mvua ili tusife njaa! Miaka 50 baada ya uhuru mtazania hawezi kumudu bei ya sukari! Miaka 50 baada ya uhuru maji safi na salama ni ahadi ya wanasiasa ambayo hawatekelezi, miaka 50 ya uhuru madini yetu yanaporwa huku sisi tukipigwa na polisi eti tumevamia ardhi na sehemu za machimbo.Miaka 50 ya uhuru uchumi wetu unamilikiwa na wahindi wachache wanaoshrikiana na viongozi mafisadi wa CCM Miaka 50 ya uhuru bado hatuna usalama hata majumbani mwetu, ujambazi na mabomu yantulipukia tukielezwa kila mara eti ni bahati mbaya! miaka 50 ya uhuru umeme 10% tu ya watanzania pia umewashinda! Miaka 50 shule ni mahali pa kufelisha kizazi chote bila hata uchungu! CCM ya Mafisadi lazima tuiondoe sasa! Wakati ni huu... Mapinduzi yanawezekana kama tumechoka na hayo...lakini kama hatujachoka nayo basi tueendelee na CCM

    ReplyDelete
  4. Kiukweli tumechoka, vijana tupo na usasa, zaidi hatudanganyiki tena, Rais wetu anaongoza wananchi wasomi na waliomzidi sana kielimu, na hatufai kabisa, walichakachua kura na ndio matokeo yanaonekana sasa!kama ana akili timamu hawezi kusema kashinda eti 60% ktk wapiga kura 8milio wakati Watanzania tupo 60milioni.
    Crazy Guy! Even if chadema nao watafuata mkondo huohuo lakini tuongozwe na chama kingine na sio ccm.
    Tumekua dilemma for Hasa na Ungozi wa rai wa sasa.

    ReplyDelete
  5. Nimeona BANGO moja kwenye picha za maandamano ya CHADEMA huko Bukoba likisomeka "HERI YA UKIMWI KULIKO CCM" imekaaje hii?

    ReplyDelete
  6. kulwa-brunei. unaposema "Wote mna makosa na wote mko right" unamaanisha nini? Ulishawahi kuona giza na mwanga vimechananyikana? Hawawezi kuwa na makosa na kuwa hawana makosa kwa wakti mmoja. Kama walikuwa na makosa zamani, wakatubu na kuyaacha, hawana makosa tena.

    CCM wanapenda tuishi gizani. Tusijue chochote wanachofanya. Tusiwaulize, tukae kimya tuvumile mpaka 2015. Itakapofika 2015 kwa kukaa gizani, tutawaondoaje? Tutawapingaje? Tutawezaje watu wengine wa kutuongoza toka miongoni mwa watu walio gizani? Itabidi tuendelee kuwatii wao kwa vile bado giza litaendelea.

    CHADEMA wanajitahidi watutoe gizani. wanatuonyesha jinsi serikali yetu imetufanya watumwa ndani ya nchi yetu. Wanawaelimisha wananchi, wakubwa kwa wadogo, ili yamkini tupate watu wenye uchungu na wananchi wetu.

    Utasemaje wote wako sawa. Kumbuka amani ya kweli haiji ila kwa ncha ya upanga. Si lazima upanga uwe wa chuma. Haya maneno yanayosemwa na CHADEMA ni mkuki mkali kwa CCM na Kikwete.
    Hii tayari ni vita dhidi ya ufisadi. Mlio katikati mnaosema wote ni sawa sawa mnatuangusha. Hata kama huna kadi ya CCM au CHADEMA, kiitikadi lazima uegemee upande mmoja. Waoga na wasioamini sehemu yao ni katika ziwa liwakalo moto.

    ReplyDelete
  7. Kama ilivyo kwa waumini kuwa sadaka inatolewa madhabahuni au mbele ya madhabahu,ni utaratibu uliowekwa ambao hadi sasa inaonekana ni mwema.
    Vivyo hivyo kwa siasa za nchi yetu huna budi kufanya shughuli za siasa kupitia kwenye chama unachokiona sera na utendaji wake vinaendana na misimamo yako.
    Ccm members are in satisfaction with their party manifesto and operations, similar y to chadena members; if not so they could have departed or formed party of their enthusiasm.
    Political Challenges are there for intimating change for the way forward toward development
    goals.
    Keep it up CHADEMA

    ReplyDelete
  8. hongera dk slaa na mh mbowe.... tuko pamoja

    ReplyDelete
  9. Tusimaie ukweli jamani-Hivi Mkuuwa nchi anaposimama na kukitupia madongo CHADEMA kuwa kinataka kuleta fujo - fujo inasababishwa na askari wanapozuia maandamano ya amani.

    Kwa maoni yangu CCM waondoe hofu na wawaache CHADEMA wajitambulishe kwa wananchi- wao ndio hatimae watachagua mbivu na mbichi

    ReplyDelete
  10. Kitendawiliii!
    chaama chetu cha mafisadi chama chao cha wateule
    JiBuuuu.........

    ReplyDelete
  11. kwisha habari yenu CCM.
    MUNGU AKULAZENI MAHALA PEMA KWENYE MAKAA YA MAWE KAMA YA KIWIRA NA GASE KALI INAYOWAKA KAMA SONGOSONGO.

    ReplyDelete
  12. Pumbavu wote chadema. Mtalia na kusaga meno 2015. Nyie chekeni sasa hivi. Jeuri yenu mtaipata. Kikwete au kiongozi yeyote wa serikali msijihangaishe kujibizana na hao maiti. Hata wafuasi wao ni maiti tu ona wanavyoongea ugoro hapo juu. Wananchi sasa wamekwisha tambua makosa ambayo wangeyafanya kwa kuwaweka chadema madarakani hasa babu Slaa ambaye amelaaniwa na Mungu kwa kuacha upadre. Angalia sasa anavyokimbizana na wake za watu. Mbowe huyo anyamaze tu. Eti anatetea wanyonge. Kwanza atueleze mali alizonazo amezipataje. Angekuwa CCM angeitwa fisadi. Washenzi nyie Chadema.

    ReplyDelete
  13. Acha matusi mkubwa! matusi hayajengi, we kama ni Chadema au CCM Toa hoja za kutetea chama chako sio kumshambulia mtu.

    ReplyDelete
  14. anonimous said kwanza inaonekana hana elimu,utashi na pia uelewa wake wakufikiri ni mdogo kwani debe tupu ahaliachi kutika vyombo vya habari kama gazeti hili limeweka sehemu ya maoni watu watoe ushauri na kuelimishana wewe anonimous said nakuonea huruma sana kama utakuwa unaufinyu wa mawazo namna hiyo basi ata mkeo atajutawala sana

    ReplyDelete
  15. hana jina:"kulwa-brunei. unaposema 'Wote mna makosa na wote mko right' unamaanisha nini?"

    wewe ndiye moga kwanza jina lako halipo, unaogopa nini?

    Demokraya ni moja ya njia mbaya ya kuchagua viongozi bora. siyo kwa kuwa wengi wanakupenda so, ni mtu mwema. Kuna vyama visivyojulikana tanzania lakini ukichunguza viongozi wake ni watu wema sana.
    Kuna mtaalm mmoja anasema while fighting for power there is no one who will be clean. Lazima kuna motivation chafu ingawa kidogo kila upande tu. Mwingine anasema 'power corrupts and absolute power corrupts absolutely.' Usiniambie yote yanayosemwa na viongozi wa chadema au ccm yote ni right.Au yote aliyosema rais kikwete kwa vile ni Fisadi hayana maana. (utakuwa hujatenda haki ya ubongo wako) Kuna pumba na chenga ni jukumu la wananchi kuchambua hizo kwa chadema na CCm. In short sipendi CUF, Chadem na CCM, the beautiful ones of my heart are not yet born and it is not wrong to be so ni kama ambao wana miaka 50 bado hawajampata mzuri wa kuishi naye ni chagua lako. Hope umenipata. nipo hapa asia ya kusini brunei.

    ReplyDelete
  16. CHchadema moto mlio uanzisha msiuzime mpaka kieleweke. maisha yamekuwa magumu mpaka tabu.watazame wa machinga. wakitafutariziki wanapigwa tukiandamana kwa hamani tunapigwa serikari ya kikwete haifai kama hii serikali wana upeo wakutosha wajiuzuru kwani hawatujali wananchi.

    ReplyDelete
  17. ki ukweli si chadema wanaoleta vurugu katika nchi dhambi ya uchakachuaji wa kura za chadema inawatafuna. tazama jinsi wanavyo haha kwani dhaili wanajua wame dhulumu haki ya wenzao. this people hawajui kisicho riziki hakiliki...
    ukowapi uhuru wa maandamano ukipingwa, ikowapi demokrasia tanzania kama raisi anaongoza kuivunja. all i can say mtanzania mwenzangu, omba omba omba. biblia inasema MUNGU hakutupa roho ya woga bali roho ya ujasili.tuwaunge mkono chadema kupinga ufisadi na kila aina ya kudhulumu malizetu.

    ReplyDelete
  18. ASANTEN SANA WANA WANCHI MWENYE MACHO AAMBIWI TANZAMA WANA WA ISRAEL JAPOKUWA WAMEPATA SHIDA MPAKA WAMEITWA TAIFA SASA FREEDOM IS A PROCESS TUNAKARIBIA KUIPATA NAONA LIBYA HAYAKUSTAHILI ILA BONGO WE NEED NEW FIGURE NEW PARTY TO EXPERIENCE THE DIFFERENCE PAMOJA MWANA WA NCHI BY NKYA

    ReplyDelete
  19. baraka shilolelo kahama....Chadema fanyeni kazi yenu tunatambua kuwa ninyi ndio wakombozi wa taifa la Tanzania tuteteeni sana kwa hao tuwaitao mafisadi.hata rais atambue kama tanzania ya sasa ni nomaaaaaaaaaaa.

    ReplyDelete
  20. huyo anayetoa matusi badala ya hoja inaonesha ameshiba kwa ufisadi wa ccm, pengine baba au mama au ndugu zake wanapata kitu toka ccm kinachompa shibe akapata nguvu ya kuongea upumbavu. jibu hoja kwa hoja na si hoja kwa matusi.

    ReplyDelete
  21. BIG UP CHADEMA, 2015 TUNAINGIZA WABUNGE 200, TUNAKAMATA UDIWANI 3/4 YA NCHI. JAMANI CHADEMA MNATUWAKILISHA VIZURI. TUNAWAPENDA SANA. CCM WE WERE TOGETHER BUT FOR NOW WE ARE BORED SIMPLY BECAUSE U ARE CORRUPT "FISADI". BYE, BYE CCM, HOPE TO MEET U JEHANAMU!

    ReplyDelete