18 February 2011

TOC yataja zitakazoshiriki All Africa Game

Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Olimpiki Tanzania (TOC), imesema timu zenye viwango na zitakazofuzu kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika 'All Africa Game', ndiyo zitakazopata
nafasi ya kushiriki michuano hiyo.

Akizungumza kwa simu Dar es Salaam jana Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi alisema katika Mkutano Mkuu wa Kamati hiyo uliofanyika mwaka jana, walipendekeza baadhi ya michezo kushiriki mashindano hayo.

"Shida iliyopo ni kwamba baadhi ya michezo bado haijafuzu viwango vinavyotakiwa, hivyo tunasubiri kikao ambacho vyama vilitakiwa kukaa na serikali ili kujua nini kitafanyika na michezo ipi itashiriki mashindano hayo.

Alisema kwa sasa wanaisubiri serikali kuandaa kikao hicho cha pamoja, ambacho kitazungumza na vyama mbalimbali vya michezo vilivyopendekezwa kushiriki mashindano hayo.

Mashindano hayo yanatarajia kufanyika Maputo, Msumbiji Agosti mwaka huu na kushirikisha michezo mbalimbali kutoka nchi za Afrika.

No comments:

Post a Comment