Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), linapenda kuwaomba radhi wateja wake na wananchi katika Jiji la Dar es Salaam kutokana na kukosa umeme kwa
saa kadhaa juzi kutokana na mvua kubwa iliyoharibu miundombinu ya umeme.
Miongoni mwa miundombinu iliyoharibika ni pamoja na kuanguka kwa nguzo za msongo mkubwa (HT) katika maeneo ya Jangwani na Kinondoni Mkwajuni.
Taarifa ya TANESCO iliyosainiwa na Meneja Mawasiliano, Bi. Badra Masoud ilisema jana kuwa hali hiyo ilisababisha maeneo mengi ya Jiji la Dar es Salaam kukosa umeme kuanzia saa 5.10 asubuhi hadi mafundi wa TANESCO walipofanikiwa kuurudisha kwa awamu kuanzia saa 10 jioni.
Vilevile transforma lenye ukubwa wa kVA 315 la Golani Msewe liliungua na kusababisha wateja katika maeneo ya Kimara, Golani na maeneo yaliyo jirani kukosa umeme kuanzia Jumamosi usiku.
Jitihada zimefanyika na transforma ya KVA 50 imefungwa katika eneo hilo. Pia Mbezi Kwa Musuguri waya unaounganisha transfoma uliungua na kusabibisha eneo la Mbezi kukosa umeme.
TUNAWAPA PONGEZI KIASI FULANI KWA KAZI YAO NGUMU LAKINI ISYO NA UADILIFU MAANA INAFANYA KWA UPENDELEO KUNA SEHEMU ZINGINE UMEME UKIKATI HAKIKA HAWALALI USIKU USIKU HADI UMEME UREJESHWE LAKINI KUNA BAADHI HAWANA UMUHIMU CJUI NI NINI?!! KWA MFANO WAMESEMA MGAO SIKU 3 KWA WIKI WAKABADILISHA SASA NI SIKU 5 LAKINI TEMEKE UKIWAULIZA WANAKWAMBIA NI SIKU ZOTE SABA
ReplyDeleteNA KUNA BAADHI YA MAENEO TOKEA MGAO UANZE WAO NI MASAA MACHACHE TUU NDIO WANAKATIWA,TATIZO LIKO TEMEKE HASWA KIGAMBONI YAANI HUKU NI KILA SIKU SIKU 7 ZA WIKI KIBAYA MNO KUNA SIKU UNAWASHWA SAA 12.30 IKIFIKA SAA 2 UNAZIMIKA MPK SAA 5.300 USIKU SIKU NYINGINE NI MPK ASUBUHI KAMA KUNA SEHEMU KATIKATI YA PC NA CHADIBWA HAPO MAKABURINI MAGOGONI KULALA KIZA HAPO NI KAWAIDA WAMEWEKA TRANSFOMA LAKINI NI NDOGO INAZIDIWA KILA MARA INATRIP,HALI NGUMU SANA ENEO HILO!!WENZETU WA UPANDE WA FERI UNAWAKA NA MJIMWEMA UNAWAKA VIJIBWENI WAO MGAO HAWANA HAWAKATIWI KWA SABABU KUNA HOSPT NA OFISI YAO TANESCO IKO HAPO, TUANAWAOMBA WAWE MAKINI KTK KUTEKELEZA WAJIBU WAO NA WASITOE UPENDELEO KWA BAADHI YA WATU ETI KUONA SEHEMU ZINGINE HAZINA UMUHIMU KILA MTU ANAUHITAJI UMEME.
Halfu waziri katangaza kupeleka umeme wilayani, hapo dar tu panawashinda!Halafu na sisi ambao hatuna makao makuu ya wilaya na hatumjui mkuu wa wilaya kama wilaya ya morogoro tutapataje huduma hiyo? au ndiyo mtindo wa kupima na kuchimika nguzo kama mgeta na kuwadanganya watu miaka tisa? Hii serikali itaondoka kama ya misri na rafiki zake wanaokaribia kama wa tunisia, iran, algeria na mwisho ni tanzania, mtaona!
ReplyDeleteTATIZO LENU TANESCO MNAPENDA RUSHWA.
ReplyDeleteNGUZO NYINGINE ZIKO WAZI KABISA KUWA ZITAANGUKA MUDA WOWOTE LAKINI HAMJISHUGHULISHI.
HUKU MBEZI MALAMBA MAWILI NGUZO NYINGINE HADI ZIMELALA TENGE NA KUSABABISHA NYAYA KUSOGEA CHINI KABISA NA TAARIFA MLISHAPEWA LAKINI MNAPITA MNAZITAZAMA TU KWA MACHO YA MAKENGEZA KAMA HAMZIONI VILE,MNASURIRI ZIANGUKE NA KUSABABISHA MADHARA NDIYO MUWE BUSY KUREKEBISHA.
NYAYA NYINGI ZIMESHUKA CHINI JAMBO AMBALO NI HATARI,LAKINI MNATAKA 'MSHIKO' KWANZA,HII NI HAKI KWELI?
Kuanguka kwa nguzo isiwe kisingizio,kwani hata kabla ya kuanguka kwa hizo nguzo mlikuwa mnakata umeme pasipo maelezo. na huu ni mgao wa aina gani? kila baad ya saa mbili mnakata umeme? acheni ubabaishaji,
ReplyDelete