28 February 2011

Sitta azidi kuwakuna wasomi

*Wasema aliongoza bunge kwa maslahi ya taifa
*Wataka katiba mpya iwalinde watu kama yeye


Na Martha Fataely, Moshi

WASOMI wa vyuo vikuu Kanda ya Kaskazini, wameeleza kuridhishwa na utendaji wa aliyekuwa
Spika wa Bunge la Tisa, Bw. Samueli Sitta kutokana na kuendesha mijadala mbalimbali kwa maslahi ya taifa.

Wasomi hao kutoka vyuo vikuu vya Mwenge, Tengeru, Mount Meru, KCMC College, Chuo Kikuu cha Stephano Moshi (SMMUCo) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara (MUCCoBS), wameyasema hayo  katika mdahalo wa kujadili katiba mpya.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Bw. Clemence Mbogo kutoka MUCCoBS, alisema katiba ya sasa haioneshi kuwalinda viongozi wanaoweka maslahi ya taifa mbele kama alivyokuwa Bw. Sitta.

Alisema Bw. Sitta ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipokuwa spika wa bunge aliweka utaifa mbele na siyo maslahi bianfsi au vyama vya siasa kama wanavyofanya baadhi ya viongozi kwa sasa.

Katiba yetu ya sasa imekaa kimya, haioneshi namna gani itawatetea viongozi wanaoweka maslahi ya taifa mbele na hii inasababisha wenye mamlaka kuwaondoa nani asiyejua Sitta alifanya kazi kwa maslahi ya taifa alihoji.

Kuhusu madaraka ya rais wasomi hao walisema katiba ya sasa inampa rais madaraka makubwa ya kuteua mawaziri, wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya bila ukomo.

Wakizungumzia suala hilo, Bw. Godfrey Banza, Bw. Antony Lyimo na Paul Momba walisema katiba haioneshi idadi kamili ya mawaziri wanaopaswa kuteuliwa jambo ambalo husababisha rais kuteua idadi itakayompendeza yeye bila kujali gharama kwa taifa.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Moshi, Bw. Japhary Michael aliwabeza baadhi ya watu wanaopinga wanasiasa kuzungumzia katiba kwani siasa ndiyo mhimili pekee ambao kila jambo nchini hupitia kwao.

Aidha meya huyo alibeza kauli za baadhi ya viongozi wa CCM wanaotaka Watanzania wasizungumzie katiba kwa madai hawaifahamu kwani mahitaji ya katiba mpya kwa sasa yanatokana na katiba iliyopo kutofahamika na asilimia kubwa ya Watanzania.

Akifungua mdahalo huo, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Dkt. Norman Sigalla aliwataka wasomi kuwa makini katika kufafanua katiba inayohitajika kwani mtazamo wa ubovu wa katiba iliyopo sasa huenda ukaonekana hivyo kutokana na uongozi uliopo madarakani.

Katiba inaweza kuwa nzuri au mbaya kutokana na uongozi uliopo madarakani lakini pia viongozi wasipokuwa na uhusiano mzuri na wananchi wao huweza kuleta hali ya kutaka mabadiliko, alisema.

Awali waandaaji wa mdahalo huo, Waziri wa Elimu wa Serikali ya Wanafunzi MUCCoBS, Bw. Zawadi Kalist na Naibu wake, Bw. Amani Laizer walisema mdahalo huo umelenga kutoa muongozo sahihi kwa jamii kuhusu mabadiliko ya katiba badala ya kuvutwa na ushabiki wa kisiasa.

7 comments:

  1. hata wakitupa kmada wao makinda badala ya sitta watanzania tumeamka na hamna spka atakayezba midomo na nguvu za umma.tunawaamn chadema na tunajua watamfundisha adabu makinda na hongo za akna rostam na mafisadi wengne lazma aztapke.huyu mama tunajua ni malaya na bla shaka uspka wake ameupata kwa kumvulia chup kikwete na matahira wenzake wa ccm .awamu hii lazma avae chup

    ReplyDelete
  2. makinda analitia aibu bunge la sasa kwan hata kiswahl hajui sembuse sheria na taratbu za kuendesha bunge. tunayo hasara kubwa watanzania kuwa na spka pmbi kama makinda.analiaibsha bunge. yeye ni taahra na pmbi kama kikwete.

    ReplyDelete
  3. makinda n aibu kwa bunge na si zaid ya parapanda ya ccm na chama bandia cha upnzan cha cuf.chadema piganen kwan nyie tu watetez wa kwel wa wanyonge.tazama ss tuko nany daima

    ReplyDelete
  4. HAYA NI MAONI YAKO MWANDISHI. UKWELI NIKWAMBA SITA NI FISADI WA SIASA. KWA SABABU YETU WATANZANIA KUENDEKEZA CHUKI, WIVU, UNAFIKI, UONGO, UVIVU BASI TUNAMUONA SITA NI SHUJAA MAANA SIFA ZA SITA NA KUDI LAKE NI HIZO.

    TWAMBIE SITA AMEFANYA NINI ZAIDI YA KUONGOZA BUNGE KWA MAJUNGU NA FITINA NAWE MTANZANIA UNA MPONGEZA TUKUELEWEJE!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. wewe n mkituko mkel kwel. kama sitta aliongoza bunge kwa majungu basi kikwete anaongoza nchi kwa vp. wewe una tatzo la fkra omba uelimishwe

    ReplyDelete
  6. wewe mchangiaji wa 8:17pm we pimbi kweli,huoni aibu huna aibu wafanana na mtu anavua nguo zake mbele ya jukwa la watu mabilioni, nenda mirembe watakupa tiba,pole sana unaungonjwa wa kufisha.

    ReplyDelete
  7. KWELI NAAMINI KUSOMA SIO KUELIMIKA,INASHANGAZA
    KUSIKIA MCHANGIAJI KAMA HUYO ASIJEJIJUA MAISHA YAKE NA WALA ASIYEJUA MAMBO YALIVYOKWENDA KATIKA BUNGE LA 9 POLE SANA NDUGU YANGU.
    WEWE KAMA HUJIJUI MAISHA YAKO UTULIE.
    WAACHE WENYE UCHUNGU KAMA SITA NA WACHACHE TUNAOWAJUA.
    KWELI HUNA AIBU HATA KIDOGO,WASWAHILI WANASEMA ANAYEFICHA MARADHI KILIO KITAMUUMBUA.
    SAMWELI SITA AMEFANYA MAMBO MAKUBWA NA SIDHANI KAMA YATATOKEA TENA.
    SIO MFITINI NI HURUMA KWA WATANZANIA WENGI
    AMEIBUA KASHFA KAMA YA RICHMOND AMBAYO
    MPAKA LEO INAITESA NNCHI WEWE HUJUI HILO?
    WATANZANIA WANAISHI MAISHA MABAYA YA UMASKINI WA KUTUPA,AU NA WEWE NI FISADI?
    NI AIBU KARNE HII WATU WANAZUNGUMZIA UMEME
    AU WEWE HUJUI?
    MAENDELEO YATATOKA WAPI?
    VIONGOZI WASIO WAKWELI JUA MAENDELEO PIA HAKUNA HAPO.
    WATANZANIA WANAUMIA SANA NA UGUMU WA MAISHA
    WACHA USHABIKI WA KISIASA.

    ReplyDelete