09 February 2011

Muswada wa katiba kuwasilishwa Aprili

Na Kulwa Mzee, Dodoma

WAZIRI Mkuu, Bw. Mizengo Pinda amesema serikali inatarajia kuwasilisha bungeni muswada wa kuruhusu bunge liunde tume ya kuratibu maoni ya
katiba mpya.

Akizungumzia hayo bungeni jana, Bw. Pinda alisema muswada huo utawasilishwa katika mkutano wa bunge wa Aprili mwaka huu.

Waziri Pinda alisema tume hiyo itakapoundwa itapewa maelekezo ya jinsi itakavyofanya kazi na kwamba bunge litatoa maelekezo ya namna ya kufanikisha utekelezaji huo.

“Katiba ni mali ya wananchi na ili ifanyike kwa umakini lazima wananchi washirikishwe kwa sababu ni mali yao, kwa hiyo katika utekelezaji huo, katika Bunge la Aprili Serikali itawasilisha muswada wa kuunda tume hiyo ili Bunge liipe baraka,” alisema.

Pamoja na kuwapo mchakato wa kuunda katiba hiyo, Waziri Mkuu alisema katiba ya sasa inastahili kuheshimiwa kwa kuwa ndiyo iliyolifikisha taifa katika mafanikio yaliyopo.

Pamoja na kasoro ndogo ndogo zinazoonekana kuwapo, katiba hiyo imeimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania.

Alisema hatua ya serikali kukubali katiba mpya haitokani na msukumo wa vyama vya upinzani vya CUF na CHADEMA kama wengi wanavyosema, bali huo ni uamuzi uliofikiwa na serikali.

1 comment:

  1. Mzee wa busara Pinda tunaitaka haraka wananchi,muulize msekwa alichokiona msidhani watanzania tuna mzaha 2015 hapatatosha kama hakuna katiba mpya....wakuu wa wilaya na mikoa nje,tume ya uchaguzi itoke bungeni na baada ya kuundwa Rais ana step down pamoja bunge kuvunjwa soon,mawaziri wastepdown mara moja na makatibu wakuu ndio watakuwa wasemaji wakati wa uchaguzi tu,jaji mkuu ateuliwe kutoka bungeni na baada ya hapo jaji mkuu atateua majaji wengine na kuidhinishwa na bunge,mwanasheria mkuu halikadhalika majina matatu yaende bungeni na bunge lipige kura kumchagua mwanasheria mkuu,wakurugenzi wa majiji,manispaa na miji wote wateuliwe katika mkoa husika na Mkuu wa mkoa au gavana atakaechaguliwa na wananchi na si mkuu wa mkoa wa kuteuliwa.mikataba yote ya madini,misitu,uvuvi na makampuni ya serikali lazima ipite bungeni,kiongozi atakaekiuka maadili hasa kujihusisha na ufisadili ni lazima avuliwe wadhifa wake na afikishwe mahakamani na ikithibika amehusika kwa namna moja au nyingine afilisiwe kwa maslahi ya taifa.....

    ReplyDelete