14 February 2011

Mikakati urais CCM 2015 yashika kasi

*Makundi yaanza kujipanga mjini Dodoma
*Wapambe waitwa kutathmini hali ya hewa  


Na Mwandishi Wetu, Dodoma

KATIKA hatua inayoonesha kuwa mbio za kuwania urais mwaka 2015 zimeanza, makundi ya
wanasiasa yameanza harakati kuunda mitandao huku wengine wakiita wapambe wao na kufanya mikutano kujua namna ya kujipanga.

Uchaguzi mkuu ujao utakuwa na mvuto wa aina yake kwani Tanzania itapata Rais wa Awamu ya Tano kwa mujibu wa katiba kutokana na kwamba Rais wa sasa Jakaya Kikwete kumaliza muda wake kikatiba.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini makundi ya wapambe wakimiminika mjini Dodoma kunakoendelea kufanyika mkutano wa pili wa Bunge la kumi la Jamhuri ya Muungano.

Habari za kuaminika zilizolifikia Majira, zimeeleza kwamba baadhi ya vigogo wenye nia ya kuwania nafasi hiyo juzi na jana walikutana na makundi ya wapambe kwa lengo la kuweka sawa mitandao hiyo kwa ajili ya mwaka 2015.

Mmoja wa watu walioshiriki kwenye mikakati hiyo, alipoombwa na kuzungumzia vikao hivyo juzi kwa njia ya simu, hakukataa wala kuthibitisha jambo hilo bali alisema maandalizi yoyote ya kisiasa yanahitaji mipango na mikakati ya muda mrefu.

"Kweli nipo Dodoma, nimekutana na watu lakini si kwa ajili ya urais tu wa 2015, wengine ni marafiki zangu wa siku nyingi (alitaja majina),tuna mambo mengi ya kuzungumza ya kawaida kwani hata tukizungumzia urais kuna ubaya gani?" alihoji.

Ilielezwa kuwa mkakati huu ni awamu ya tatu baada ya ule wa kwanza na ya pili uliolenga kujiimarisha ndani ya bunge, kuonesha dalili chanya katika kutekeleza lengo hilo.

Awamu ya kwanza ya mkakati huo ililenga kuhakikisha wabunge wasiopungua 85 wanaounga mkono moja ya kambi zinazowania urais, wanapata nafasi ya kurudi au kuingia bungeni jambo ambalo limeelezwa kuwa lilifanikiwa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mkakati wa pili ulitajwa kuwa ni kuhakikisha makundi hayo yanashika nafasi nyeti ndani ya kamati mbalimbali za bunge, kazi ambayo nayo imeelezwa kuonesha mafanikio.

Uchunguzi wa Majira umebaini kuwa wapambe hao kutoka mikoa mbalimbali walikutana kwa nyakati tofauti na baadhi ya  wanasiasa hao kuweka mikakati hiyo, wengine wakiwa makada wa chama tawala CCM kutoka mikoa na wilaya mbalimbali nchini.

"Haya mambo si madogo inawezekana hawa wanapima upepo ndio maana wameamua kuita watu mbalimbali, waangalie watu mikoani wanasemaje na wanajipanga vipi? kilisema chanzo chetu.

Baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakitajwa kuwania urais mwaka 2015 ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Benard Membe, mawaziri wakuu wa zamani Bw. Edward Lowassa na Bw. Fredereck Sumaye, Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya.

11 comments:

  1. Nasikitika, hii habari imekaa ki-UMBEA zaidi. Can you come up with more concrete substance than this?

    ReplyDelete
  2. jaman mbona waandishi mnashambulia sana mikakati ya CCM?kwani hilo nalo ni jambo baya?hata chadema wanamikakati hiyohiyo pia,lakin hatuoni mkiianika...
    Halafu kujipanga kwetu mapema ndiko kunakopelekea usindi wetu, na mwisho wa siku mnakuja kutuzushia kuwa tumeiba kura...mmh

    ReplyDelete
  3. Hicho chama bado kidogo kitakufa.Vijana hatuwezi kukubali kuendeshwa.Tunataka tuweke raisi bora siyo bora raisi.

    ReplyDelete
  4. Wengine hawana hata aibu,wamelipeleka Taifa pabaya hadi sasa halafu bado wanataka Uraisi.Watachomwa moto siku ya mwisho kwa kuwa wanadanganya umma.Lakini sijui kwa kuwa wengine wako dini za mashetani.

    ReplyDelete
  5. Kuna mmoja hapo anatajwatajwa sana hivi anafikiri watanzania ni wajinga eee..
    Hakuna fisadi atakayepata Uraisi 2015.Wakichakachua kura tunafanya kama Misri na Tunisia.Hizo helo walizoiba zinatosha waende wakaishi Ulaya waiache nchi kwa wazalendo.

    ReplyDelete
  6. Nimesikia JKT haiajiri,lakini inatoa mafunzo.Nafurahi sana kwa kuwa hawa vijana watasaidia kulikomboa taifa dhidi ya ufisadi pale watakapoongoza maandamano ya mapinduzi.

    ReplyDelete
  7. CCM hata kama mna dola na fedha 2015 hamtaingia madarakani. Tumechoka kuwa na hayo majina Lowasa hatumtaki kabisa. Sumaye amezeeka hana jipia.Membe hana maana hana busara kabisa Lazima CCM ififundishwe adabu.

    ReplyDelete
  8. Ni mama profesa Tibaijuka tu ndiyo kimbilio la CCM 2015......................

    ReplyDelete
  9. mkono Rutashubanyumabilinganyamana.

    ReplyDelete
  10. kwa nini Magufuli mchapa kazi tusimpe urais. kwa hao wanao kaa vikao kisiri siri sijaona anaye faa kuwa Rais.

    ReplyDelete
  11. Tunataka raisi anayejiamini kama Dr Silaa na waziri mkuu kama Magofuli ili tuwalipue wanaohujumu nchi, sita awe makam wa raisi.

    ReplyDelete