LONDON, Uingereza
MSHAMBULIAJI wa Manchester United Michael Owen, anaweza kujikuta akikaa tena nje ya uwanja kutokana na kuumia korodani wakati akiwa
mazoezini.
Owen aliumia wakati timu yake ikifanya mazoezi katika Uwanja wa Carrington Jumatatu.
Mshambuliaji huyo alitolewa nje ya uwanja baada ya kujisikia maumivu.Alikwenda kufanyiwa kipimo juzi na United, inatarajia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 atakuwa nje kwa muda kadhaa.
Owen amecheza mechi sita za Ligi Kuu katika msimu huu ameweza kufunga goli moja tu, lakini alicheza katika mechi ya Kombe la FA ambayo United ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Southampton.
Alikaa nje ya uwanja kwa miezi mitatu baada ya kuumia paja Oktoba, mwaka jana lakini hatacheza katika mechi dhidi ya Crawley Town kwenye Uwanja wa Old Trafford Jumamosi.
No comments:
Post a Comment