Na Waandishi Wetu
WAKATI Jeshi la Polisi mkoani Singida limekamata bunduki mbalimbali 36, katika Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi yamekamatwa magobore 27 yanayodhaniwa
kuwa yalikuwa yakitumika katika matukio ya uhalifu na uwindaji haramu.
Katika Mkoa wa Singida, Kaimu Kamanda wa Polisi, Bw. Nyigesa Wankyo alisema jana kuwa silaha hizo zilipatikana wakati wa misako iliyoendeshwa katika maeneo mbalimbali mkoani humo kipindi kilichopita.
Akitoa taarifa yake kwa waandishi wa habari ofisini kwake hivi karibuni Bw. Wankyo alifafanua kuwa kati ya silaha zilizokamatwa ni bunduki moja ya aina ya SMG, bastola mbili, rifle nne, Shortgun moja na magobore 28.
Alisema katika misako hiyo ambayo ilifanyika kwa njia ya kushtukiza pia jumla ya risasi 105 zilikamatwa zikiwepo 37 za SMG na SAR 47 za bastola, moja ya rifle, saba za shortgun na 13 za gobore.
Kutoka Rukwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Bw. Isunto Mantage alisema kukamatwa kwa magobore 27 kumetokana na oparesheni maalumu iliyoendeshwa na jeshi hilo kwa kushirikiana na askari wa wanyamapori kwa takribani wiki mbili.
Kamanda Mantage alisema kuwa bunduki hizo zilikamatwa kwa nyakati tofauti katika Kijiji cha Nkuswe, Itunya, Kaparamsenga katika Tarafa ya Karema na Kikiji cha Majalila kilichopo katika kilichopo katika tarafa ya Kabungu.
Kati ya magobore hayo, 17 yalisalimishwa na wamiliki kwa mwenyekiti wa Kijiji cha Nkuswe baada ya wananchi kugundua kuwa kuna operesheni hiyo.
Katika oparesheni hiyo pia wamefanikiwa kukamata risasi 40 za gobore, nyama ya mbawala kilo 15 nyama ya myemela kilo 2 pamoja na nyama ya kiboko kilo 50.
No comments:
Post a Comment