Na Waandishi Wetu
KAULI mbili tata za Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema kuhusiana na suala la malipo ya sh. bilioni 185 kwa kampuni ya Dowans na kupinga kuandikwa upya kwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimepokelewa kwa
maoni tofauti na wananchi katika maeneo mbalimbali.
Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya wanasheria wakiwemo vigogo serikalini walisema Jaji Werema amejisahau kuwa ni mshauri wa Serikali na si mtoa hukumu.
"Kwanza kauli ya Jaji Werema ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali imewashangaza na kuwashtua sana wanasheria wengi wa ndani na hata wa wale nje tuliozungumza nao asubuhi ya leo (jana).
Nadhani amejisahau kuwa yeye bado ni Jaji wa kutoa hukumu mahakamani, hajui kuwa kazi yake ni kuishauri serikali hasa rais, katika masuala ya kisheria na si kutoa hukumu mapema," alisema mmoja ya kigogo wa serikali na kusisitiza jina lake kutotajwa.
Alisema alichotakiwa kufanya Jaji Werema ni kuishauri Serikali kusitisha hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) baada ya kuandikisha hukumu hiyo katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
"Kwa mujibu wa sheria za migogogoro ya kibiashara za Tanzania hukumu hiyo bado inaweza kubatilishwa na Mahakama Kuu kupitia kitu kinachoitwa Judicial Review baada ya kuandikishwa, huo ndio ushauri ambao Jaji Werema angetakiwa kuutoa kwa serikali badala ya kuwajengea hofu wananchi," alisisitiza.Alisema wana hofu kama Jaji Werema alipitia jalada la hukumu hiyo yeye mwenyewe na kuelewa kilichomo kwa kuwa ushauri wake ni tofauti na hali halisi.
Alisema wao kama wanasheria wanamtaka Jaji Werema kuishauri serikali kuhoji sababu ya wahusika kushindwa kuandikisha hukumu hiyo mahakama Kuu ili kuruhsu hatua zaidi badala ya kuwachanganya wananchi kwa kauli tata.
"Sisi tuna taarifa kuwa mafisadi wanaohusika na Dowans wanaogopa kuandikisha hukumu hiyo Mahakama Kuu kwa kuwa majina yao yatatajwa, wanahofia Watanzania kuwatambua, hili Jaji Werema hajui? alihoji kigogo huyo.
Alishauri Rais Jakaya Kikwete, kuingilia kati suala hilo kama alivyoomba na baadhi ya wananchi kwa kuagiza hukumu hiyo kuandikishwa haraka Mahakama Kuu ya Tanzania au kufunga mjadala huo hadi wahusika watakapotekeleza kipingele hicho.
Mwanasheria mwingine ambaye yuko karibu na Jaji Werema alisema hakuamini kama kiongozi huyo angetoa kauli hiyo kwa kuwa ni mapema mno kufanya hivyo kwa kitu ambcho bado mlolongo wake ni mrefu."Inakuwaje Mwanasheria Mkuu wa Serikali aoneshe dalili ya kunyong'onyea mapema kwa kitu ambacho kwanza hakijulikani, hata anayeidai Tanzania hafahamiki ni nani" alisema.
Alisema walitarajia Jaji Werema angeishauri serikali kusubiri kwanza hadi wahusika wa Dowans watakapoandikisha hukumu hiyo Mahakama Kuu ndipo atoe ushauri na si kuongeza mkangaiko."Mimi nadhani Jaji Werema hakusoma hukumu hiyo vizuri, kilichopo mle ni kuwa Dowans wenyewe wanakiri kuvunja mkataba kutokana na kile walichosema ni mazingira ya Tanzania kutoruhusu uwekezaji wao.
Na hata kilichoamuliwa ni Dowans kulipwa madai ya malimbikizo mbalimbali ya huduma, si kwa kuvunjwa kwa mkataba kama inavyodaiwa," alisisitiza.Katika hatua nyingine, baadhi ya wakazi wa mji wa Shinyanga walikwenda mbali zaidi na kumtaka Jaji Werema kujiuzulu wadhifa wake, wengine wakidai kuwa huenda anatumika vibaya pasipo yeye mwenyewe kujielewa.Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Majira mjini hapa jana, wakazi hao walisema kitendo cha Jaji Werema kufunga mjadala wa malipo ya Dowans ni sawa na kutumia ‘udikiteta’ katika jambo ambalo wananchi walipaswa kufahamishwa undani wake kwa kina
kabla ya malipo.
Walisema madai yaliyotolewa na Jaji Werema kupitia vyombo vya habari kwamba baada ya kuipitia na kuisoma hukumu iliyotolewa na mahakama ya kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC) amekubali kuwa hukumu hiyo iko sahihi ni sawa na kuwauza Watanzania.
Bw. Khalid Kyaruzi alisema “Kwa kweli hapa mwanasheria wetu ameonesha wazi kuwa ameshindwa kutumia wadhifa wake
katika kuitetea nchi, wapo watu wanafikishwa mahakamani kwa makosa halisi kabisa, lakini bado wanakana kutenda makosa hayo kwa nguvu zote, na wakati mwingine wanashinda kesi.
“Leo mwanasheria wetu anakubali kirahisi tu kwamba hukumu hiyo ni sahihi, tunauliza kwa misingi ipi, nani mmiliki wa Dowans…tutajiwe ni nani mwenye hiyo Dowans, Werema (Jaji) si amtaje?” alihoji.Kwa upande mwingine, mmoja wa watumishi wa serikali mkoani Shinyanga ambaye hakupenda kutajwa jina alidai kuwa kitendo cha Jaji Werema kukataa kuwepo kwa katiba mpya hapa nchini kinaonesha jinsi gani mwanasheria huyo asivyoweza kwenda na wakati.
“Watanzania wote pamoja na baadhi ya viongozi wastaafu na walioko madarakani wanakubali kuwa suala la katiba mpya linazungumzika, lakini mwanasheria wetu anakurupuka na kudai kuwa hakuna haja, bali kinachowezekana ni ‘kuiwekea viraka zaidi hii ya sasa’, nafikiri huyu bwana anatumika vibaya,” alieleza mtumishi huyo wa umma.
Mtumishi huyo alishangazwa na kauli ya Jaji Werema kwamba katiba iliyopo inastahili kuendelea kuwepo na kwamba kama suala la masahihisho ni bora katika baadhi ya vipengere badala ya kuandikwa mpya na kutoa mfano wa katiba ya India ambayo alidai imefanyiwa marekebisho zaidi ya mara 50.
Naye mmoja wa wajumbe wa Baraza la wa wazee wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mjini Shinyanga ambaye hakupenda pia kutajwa gazetini amemuomba Rais Kikwete akubali kulizungumzia suala la malipo ya sh. bilioni 185 kwa kampuni ya Dowans kwa kumtaja mmiliki wake.Suleiman Abeid, Shinyanga na John Daniel, Dar
jamani Watanzania msimuhukumu bure huyu mzee kwani haya kuhusu katiba ni maoni yake binafsi hana uwezo wa kutuzuia kupata katiba mpya. binafsi huyu jamaa ni kibaraka wa Rais hivyo siku zote kauli zake si za maslahi ya nchi bali ni za kumfuraisha Rais na hiki ndio kielelezo tosha kwanini tunaitaji katiba mpya ili kumfanya mwanasheria mkuu kufanya kazi kwa maslahi ya Watanzania badala ya maslahi ya mtu mmoja.
ReplyDeleteHata hivyo ni sawa tu kwa AG kuwa upande wa Kombani kwa vile yeye ni mwanasheria wa serikali, anaitetea serikali inapofanya maovu. Ndio kazi yake. Kama ambavyo muuaji au mwizi anaajiri mwanasheria au wakili ili amtetee. Hayo SIO MAONI YAKE, ila ni msimamo wa bosi wake. Hii haina maana kuwa yeye na bosi wake watashinda. Tutamshinda kwa nguvu ya umma!
ReplyDelete1.RAIS KIKWETE ANAPIGANIA NA KUTETEA DHULUMA YA MAFISADI KAMA ALIVYOAINISHA HOSEA NA UBALOZI WA MAREKANI, KWA HIYO MSITEGEMEE ATAFANYA CHOCHOTE KUWALINDA WAJINGA WATANZANIA WALIOMCHAGUA. KWA HIYO ANACHESEMA WEREMA SI MAONI YAKE, NI MAONI YA KIKWETE NA SERIKALI YAKE KAMA PIA YALIVYOWASILISHAWA PIA NA WAZIRI KOMABANI NA RAIS MSTAAFU MWINYI.
ReplyDelete2. ANGALAU PINDA KASEMASEMA KATIBA POSITIVELY LAKINI READING BETWEEN THE LINES, SERIKALI HAITAKI. TUNASEMA NI KIONGOZI MJINGA TU AMBAYE ATACHEZA NA MOTO WA KATIBA MPYA. TIME WILL TELL.
3. DOWANS WATALIPWA MAAN NI MRADI WA KINA KIKWETE NA MAFISADI, WALA HAKUNA NIA WALA UTASHI WA SERIKALI KUPAMBANA. INASIKITISHA SANA.
JAMANI KATIBA NI HAKI,SERIKALI YENYEWE INAJUA KWAMBA KULIKATALIA HILI WANATAFUTA KIYAMA,NCHI HAITATAWALIKA MADAI YA KATIBA YAKIPUUZWA,HATA HIVYO WADANGANYIKA WALISHAAMUA KUPITIA UCHAGUZI ULIOPITA KUBADILI SERIKALI,KICHOSAIDIA HAWA SISIEM NI UCHAKACHUAJI.KUHUSU DOWANS NAPENDA KUMUONYA MHESHIMIWA KIKWETE KWAMBA ASIPOTENDA HAKI KATIKA HILI ATAJUTA BAADAE,HUWEZI KUJUA KIONGOZI ATAKAYEKUJA HATA KAMA NI WA CHAMA CHAKO ATAKUAJE,WENGINE NI WEHU ATI,UKIJAKUONDOLEWA KINGA UTAFANYAJE?
ReplyDeleteSERIKALI MSISUBIRI MAANDAMANO YA KUDAI KATIBA;HAYA YATAKAYOFANYIKA SIKU ZA KARIBUNI NI MAKUBWA NA HUENDA YAKAFIKA MPAKA IKULU,SASA WADANGANYIKA TUKIFIKA KULE MAGOGONI HATUTOKI HADI TUMWAPISHE LIPUMBA AU SLAA PALE
ReplyDeleteHuyu Warema sio mwanasheria, majibu yake ni kufurahisha kundi fulani. Wakati anakiuka haki, na cheo chake na kuonyesha udhaifu wake ulivyo kwa watanzania.
ReplyDeleteYeye anafikiri ni kwenda kucheza taarabu huko Ikulu, afikifirie haki za watanzania ziko mkononi mwake. Huyu angekuwa kiongozi wa wenzetu ungekuta saa hizi yuko mitaani. Anafikifi ni yeye pekeyake ameenda shule kumbe si hivyo. Watanzania wa leo sio wa kuburuzwa kama anavyofikiria yeye.
Jamani upeo wa kusoma nyakati lazima uwepo sasa hivi kwa sababu mambo yanabadilika. Huwezi kusema eti mtu ambaye hajui kusoma hata gazeti au kusikiliza radio atakubali mabadiliko hakuna. Tunachomshukuru mungu watanzania tumeelimika na tunatambua tunako kwenda na tulikotoka. Na haya ndio madhara mojawapo ya hii katiba kutokumpa mwanasheria nguvu ya kupambanua zama jinsi zinavyobadilika na watu wanavyotaka kutawaliwa. Huu ni ubabe tu. Hizi ni vurugu za serikali ili kupima tu watanzania wanaelimu kiasi gani?
WEREMA NA WEWE CHUKUA BEGI LAKO UONDOKE, WAPISHE WENYE UELEWA KUWA WATANZANIA WANATAKA NINI USIWE MZIGO KWA WATANZANIA ZAIDI YA DAWANS, TTCL, NK. WEWE WEREMA UMESHAKUWA MZIGO MWINGINE TENA KWA WATANZANIA KWA UFAHAMU WAKO WA SHERIA NA USHAURI WAKO KWA RAIS.
Mwnasheria Werema sio kwamba hajui kinacho endelea kuhusu katiba na mambo mengine yeye lengo lake ni kuwafurahisha viongozi wa juu serikalini ili aonekane yupo upande wao ili aendelee kula vinono kutokana na wadhifa alionao. viongozi hawa wapo peponi.wewe acha tu
ReplyDeleteni wanafiki na ndumila kuwili.
viongozi mnasahau ya kuwa haki na amani havitengamani,kwa hiyo kunyima haki ya watanzania ni sawa na kuvunja amani iliyopo.
ReplyDeleteMfumo wa uongozi mlionao itafika kikomo chake kwani mfumo utaondoka kwa kanunu ya mkiuko wa mkiuko[negation of the negation...] mpende msipende.Kwani mfumo wa utumwa uliondokaje.
Wale wote wanopinga kuandikwa kwa katiba mpya watambue wazi kuwa wanapingana na sauti ya umma,ambayo si rahisi kuishinda. Ni bora wakakakubali sasa hivi ambapo mambo bado yanaongeleka kuliko kuchelewesha na kusubiri mambo kuahribika.kwani yakishaharibika hata kwao yataharibika hayo wanayohisi wanayatetea na kuyalinda.
ReplyDeleteKusoma na kuhitimu ni jambo moja, na kuelimika ni jambo lingine. kuelimika ni pamoja na kutambua unatakiwa kuongea nini wakati gani na mahala gani. Lakini ikitokea ukakurupuka kuongea tu eti kwa sababu una mdomo na wadhifa mkubwa bila kurfikiri umma utakuelewa vipi kama AG alivyofanya, hiyo inatia shaka na kuelimika kwa watanzania hasa wanopewa dhamana kubwa ya kutetea maslahi ya umma.Pia inatia shaka kwa anayewateua.
ReplyDeleteSwali kwa daktari wa rais Je hivi Rais wetu ni bubu, mbona hatumsikii akiongea chochote pamoja na Taifa letu hivi sasa kuwa katika wakati mgumu ambao yeye sasa anatakiwa kuongea?au ni kiziwi hivyo haskii watu wanalalamikia vitu gani? 6. Nashauri mikataba yote muhimu kwa taifa iwe inaandikwa kiswahili ianawezeka lugha nayo ni tatizo na hivyo kupelekea watu kusahini vitu wasivyo elewa mitego iliyomo,nchi nyingi zisizo na matatizo ya mikataba huwa inakuwa imeandikwa kwa lugha zao wanazo zielewa 7. Hivi Werema sasa amekuwa sawa na Makamba wa CCM maana hawana tofauti katika kiwango cha kuongea PUMBA. Mwisho tunajua wamelazisha kuingia madarakani wa njia ambazo azikuwa halali na kila mtanzania anajua hilo na uenda ndicho kinacho mfanya Kikwete aone aibu kuongea na Taifa kuhusu mambo mazito,kama nchi imemshinda kuongoza bora aturudishie kwa amamni kuliko huko anako taka kutupeleka.
ReplyDeleteQuote
HUYU WEREMA AWEKWE DANI/JELA KWA KULA RUSHWA, NA KUWA UPANDE WA MAFISADI, NDIYO MAANA ANAPINGANA
ReplyDeleteNA WAZIRI MKUU MZEE PINDA KWA KILA KITU, NINAIMANI HUYU WEREMA NI MMOJA WA GENGE LA MAFISADI WANAOTAKA KUWANIA URAIS 2015.
Yaleyale alikua Chenge,akaja Mwanyika na sasa ni huyu mheshimiwa Werema ni lini tutapa AG mwenye uchungu na nchi yake?au ndiyo chukua chako mapema?muhimu watueleze ni kina nani wamiliki wa Dowans na wawatake wafungue kesi mahakama kuu ili tujue mbivu na mbichi...hivi jamani hao mafisadi wana nini mbona kila mtu anawahofia?inabidi tuingie msituni kama nchi nyingine tupate haki yetu
ReplyDeleteHii inasikitisha kabisa and kukatisha tamaa wananchi!!!!!!
ReplyDeleteSpeak up Tanzanians!!! If you dont speak up now, when will you??? JITETEE Mtanzania, jitetee. Usiwache Haki yako ikamegwa, wacha kuchukuliwa yote. Hakuna Aliekuja kutoka katika tumbo la mamake na kipande cha ardhi kinaitwa Tanzania. (Mimi naitwa Sitia) Sikuja na kipande cha ardhi kinaitwa Sitia.... Nimekuta Tanzania, na hao walokuja waliikuta pia,na wataokuja wataikuta pia. Kwa hio wewe una haki sawa na uliowachagua wawe viongozi wako - Hapana tafauti yeyote. Jua HAKI yako kabla hujafa. Usiwaache waroho watuibie. AMKA SASA... Wanatia Aibu viongozi, na wewe usione aibu kutaka ukweli.
ReplyDeleteHivi kweli kampuni ambayo viongozi wa serikali hawana masilahi inaweza kudiriki kufanya kama Dowans?
ReplyDeleteNaamini week moja tu wamiliki wake wote wangekuwa lupango.
huyu jaji werema hadi hapo kwa dhati ya moyo wake hivi bado anastahili kuwepo ktk ofisi hiyoooooo? HUTUFAI NA KAMA WEWE NI JAJI BASI NNA SHAKA NA UJAJI WAKO.
ReplyDelete