NEW YORK Marekani
RAPA Jay- Z kwa mara nyingine tena ameonesha jeuri ya fedha kwa kutumia pauni 220,000, ambazo kwa fedha za Kitanzania zaidi ya sh. milioni 499 kwa kununua zawadi za Krismasi kwa ajili ya mkewe Beyonce Knowles.Mwanamuziki huyo
mwenye umri wa miaka 41, alitumia muda mwingi akiwa katika duka la mavazi ya bei mbaya la Hermes, kabla ya Krismasi na alishindwa hata kula chakula cha mchana.
Chanzo cha karibu kilisema: "Jay alikuwa kwenye chumba maalumu katika dakika za mwisho kabla ya Krismasi kwa ajili ya kununua mavazi na vitu vinine. Walinzi wake walikuwa nje kulinda usalama."
Chanzo hicho kilisema mwanamuziki huyo, alinunua mabegi ya mkono ya Birkin ambayo inauzwa pauni 78,000 kila moja pamoja na vifaa vingine.
Jay-Z alionekana kuwa bize akiwa dukani katika duka lililoko mjini New York, kiasi kwamba muda wa kula chakula cha mchana uliopita na kuagiza kuletewa chakula.
Hayo ni mambo ya watu wenye fedha. Hivi karibuni, Beyonce alimzawadia mumewe Jay-Z zawadi ya gari la kisasa na kifahari ambalo ndilo lenye kasi zaidi kuliko yote duniani. Gari hilo linaelezwa kuwa kama litakwenda kwa kasi yake ya juu linaweza kusafiri kutoka Dar es Salaam hadi Iringa kwa muda wa pungufu ya saa mbili!
Gari hilo aina ya Bugatti, alilonunua kwa dola milioni mbili aliagiza kwa kutuma oda maalumu kiwandani, lilitolewa baada ya mwaka mmoja, alipolipata alifanya siri na akamkabidhi Jay-Z wakati wa sherehe ya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, kitu ambacho kilimshitua.
No comments:
Post a Comment