LONDON, England
KWA kile kinachoonekana ni kuvimba kichwa, kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anaamni kwamba kikosi chake kwa sasa kimekomaa baada ya mafanikio kilichoyapata dhidi ya Chelsea.Kabla ya mechi hiyo iliyochezwa usiku wa
kuamkia jana, Gunners ambao nao walikuwa wanafanya vibaya lakini katika mechi hiyo wakaweza kuonesha kiwango cha hali ya juu na kuilaza Blues 3-1 kwenye Uwanja wa Emirates.
Arsenal walipata mabao yao matatu kupitia kwa wachezaji wake, Alex Song, Cesc Fabregas na Theo Walcott wakati bao la kufutia machozi la Chelsea lilifungwa kwa mpira wa kichwa na Branislav Ivanovic.
Baada ya filimbi ya mwisho, Wenger hakuwa na neno baya la kusema juu ya kikosi chake zaidi kusifu nidhamu yao, ukomavu na kuzingatia katika kupata mafanikio yanayotakiwa."Tumepevuka. Tumebakia na kuchanginyiywa katika mechi kubwa za ugenini msimu huu," aliiambia Sky Sports.
"Tumekuwa na nidhamu na kupevuka na kila mchezaji, alikuwa akicheza na mwenzake ambapo bao la kwanza ndilo lililotoa mchango mkubwa," aliongeza.
Alisema malengo na nidhammu ndani ya timu kwa sasa ni mazuri, licha ya kuwepo mapungufu kidogo katika baadhi ya maeneo.
No comments:
Post a Comment