Na Patrick Mabula, Kahama
HAKIMU wa Mahakama ya Wilaya ya Kahama, Bi. Lilian Rugarabamu amewataka madiwani kufanya kazi kwa kufuata misingi ya katiba ya nchi wanapotekeleza majukumu ya kazi zao katika kuihudumia jamii.Bi. Rugarabamu alisema
madiwani lazima wajue sheria kwa kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria kwa hiyo wanapofanya kazi zao lazima wazingatie hilo na wasivuke mipaka ya kazi yao ili kuepusha mifarakano na uvujifu wa amani.
Hakimu huyo aliyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama ambao wameanza kazi baada ya kuapishwa na kuwataka
wafanye kazi kwa kuzingatia sheria.
Alisema kiapo kiko kisheria, maana yake wafanye kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na maadili ya udiwani ikiwa ni pamaoja na kutunza siri za ofisi, pia wasikilize matatizo ya wananchi wanaowawakilisha bila kuvuka mipaka ya wajibu wao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Bw. Bahati Matala alisema madiwani wana wajibu wa kufanya kazi kwa kufuata kanuni za baraza, wajiepushe na tabia inayoweza kuleta mfarakano kwa jamii na uvujifu wa amani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama Bw. Alfred Mhanganya alisema madiwani lazima wafanye kazi bila kwenda kinyume cha kanuni na sheria ya kazi yao na waache itikadi zao za kisiasa kwa kuwa wakifanya hivyo watawagawa wananchi waliowachagua.
Mbunge wa Jimbo la Kahama, Bw. James Lembeli aliapa kupambana kufa na kupona na wala rushwa na wafujaji wa fedha za serikali na mapato kwenye halmashauri ili kumaliza mchwa wenye tabia hiyo.
atakaye bainika kujihusisha na vitendo hivyo.
No comments:
Post a Comment