26 November 2010

Mbeya wafurahia 'Mwa' kwenye baraza la mawaziri.

Na Charles Mwakipesile, Mbeya.

WANAHARAKATI wa siasa na maendeleo Mkoa wa Mbeya wamefurahia uteuzi wa Dkt. Harrison Mwakyembe, Prof. Mark Mwandosya na Bw. Philipo Mulugo kuingia
kwenye Baraza la Mawaziri uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete, wakisema hiyo ni ishara kuwa ana imani na mkoa huo.

Katika kipindi kilichopita, mkoa huo ulikuwa na mawaziri wawili, Profesa Mwandosya na Profesa na Dkt. David Mwakyusa ambaye hakuteuliwa kipindi hiki, huku Dkt. Mwakyembe akichukua nafasi hiyo kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Bw. Mulugo kuwa Naibu Waziri wa Elimu.

Akizungumzia uteuzi huo, Mfanyabiashara Bw. Livingstone Sabukile alisema awali wana Mbeya walikuwa na wasi wasi wa kuwamo katika baraza hilo kutokana na hali iliyojitokeza wakati wa kampeni iliyosababisha matokeo ya CCM kupoteza majimbo mawili.

"unajua Mbeya ilikuwa ngome ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini kutokana na makosa yaliyotokea wakati wa mchakato wa kura za maoni uliozua mpasuko ndani ya chama ndio hasa uliosababisha  majimbo mawili ya Mbozi Magharibi na Mbeya kunyakuliwa na CHADEMA hali ambayo tungetegemea rais  akasirike "alisema.

Alisema kuwa pamoja na wana Mbeya kujenga hofu, Rais Kikwete ameona athamini uwezo wa watu ambao alikuwa anawahitaji kuingia katika baraza lake jipya.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha APPT -Maendeleo na Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama vya Upinzani saba vilivyokuwa vimeungana wakati wa Uchaguzi Mkuu, Mkoa wa Mbeya, Bw. Godfrey Davis alisema kuwa rais kumteua  Prof Mwandosya kurudi kwenye Wizara ya Maji, Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi ni kutimizwa kwa ahadi yake ya kuwa na baraza la wachapa kazi.

Alisema kuwa rais kwa kuthamini vijana walioingia bungeni mwaka huu ameonesha imani kwa kumteua kijana Bw. Philip Mulugo kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Stadi .

Bw.Davis alisema kuwa  rais ameonesha dhamira ya kweli katika kuchagua watu bila kufuata uzito wa majina  hali iliyosababisha watu maarufu waliokuwemo kwenye baraza hilo awali kuondolewa.

Alisema Dkt. Mwakyembe ni mtu jasiri mfuatiliaji mwenye uwezo wa kusimamia kile anachoamini na kutetea vitu ambavyo hivyo alisema kwa kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi  kutasaidia wizara hiyo kusonga mbele.


Alisema kuwa kwa kushirikiana na Waziri wake, Dkt. John Pombe  Magufuri  anaimani kuwa barabara zitajengwa kwa kiwango kinachotakiwa  pasipo kutafunwa fedha za walipa kodi.

Naye Kamishna  wa NCCR-MAGEUZI Bw.Daimon Mwasampeta alisema kuwa  mawaziri hao wana  deni kubwa kwa wakazi wa Mkoa wa Mbeya kutokana na ukweli kuwa moja ya shabaha ya rais kuwapa heshima hiyo ni kuona kuwa Mkoa wa Mbeya unakuwa  wenye maendeleo usiokuwa na  mipasuko isiyo ya lazima.

Alisema  ni wajibu wa mawaziri  hao kuhakikisha wanaiunganisha Mbeya kuwa kama alivyofanya mtangulizi wao Prof. Mwandosya ambaye aliamua kuthubutu kuishawishi serikali na kuanzisha ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa.

Wakizungumza kwa njia ya simu wakazi wa  Jimbo la Songwe  walisema kuwa wamefarijika na uteuzi wa  Mwalimu Mulugo kuwa Naibu Waziri  hali ambayo walisema ni malipo ya Mungu kwa kijana huyo ambaye alisomesha  zaidi ya yatima  350 kwa miaka mitatu kabla ya kuwa na fedha.

Mbali na kusomesha yatima walisema kuwa kitendo cha kuanzisha elimu ya watu wa zima ,wazee na vijana waliokosa kuipata  ambao aliwafungulia kituo  na kisha kuwapa nafasi ya kufanya mitihani katika shule yake ya Southern Highlands ni  ishara ya kutosha kuwa heshima aliyopewa na rais.

6 comments:

  1. Hongereni kaka zangu
    Fanyeni kazi zenu bila kujali mkoa mtokao.

    ReplyDelete
  2. pETRO eUSEBIUS mSELEWANovember 26, 2010 at 12:33 PM

    Hatari kubwa hii...hili si jambo la kulikenulia meno,ishieni hapohapo!

    ReplyDelete
  3. Hongera Mwakyembe kwa kuchaguliwa hakikisha uwanja wa ndege Songwe unamalizika maana Magufuli hatuna wasiwasi yeye kazi mtindo mmoja na Mwandosya naye kilio cha Maji kiishe MBALIZI na SONGWE SALUJI

    ReplyDelete
  4. Big up sn Mwakyembe.Mwandosya na Mulugo fanyeni kz kikamlifu ndg zngu, hakikishe mnaleta Maendeleo Mbeya na sehemu nyingine sio manaishia kuwa mafisaiodi tu,tabia hiyo hatuitaki. fanyeini kazi mliyotumwa na watanznia.

    Mdau toka Mby
    Hon.R

    ReplyDelete
  5. prof Mwandosya, wengi wetu tunakuaminia kwa uchapa kazi wako!!! hata Mh. Raisi kakuaminia pia. Sn Mwakyembe ni wakati wako huu sasa wa kuonyesha ukweli wa juhudi zako kwa watanzania kwani wengi tumefurahia uteuzi wako maana kasi zako za awali zimeiamusha CCM na imeshakumbuka kwamba chama hiki si cha wananchi wenye pesa tu bali ni cha waungwana, wapenda haki na usawa. Hongereni sana naamini mtachapa kazi!! Ndaga fijo malafyale ugwa mmabingu!!

    ReplyDelete
  6. Naipenda sana nchi yangu na asilimali zake za thamani. Upole na uungwana wa watanzania ni kigezo tosha cha kuifanya nchi yetu hii nzuri ing'ae na kusonga mbele kuliko kuishi kimasikini daima. Maneno haya yamebeba majonzi yangu mengi kwa viongozi wazembe na wasiojivunia uzuri wa nchi yetu!!! Ni wakati sasa wa viongozi wetu kuwatumikia watanzania na si kujinifaisha.

    Pr. Mwandosya na sn Mwakyembe, wanambeya tuanaimani sana na nyi mtauwakilisha mkoa wetu muwanufaishe watanzania wote. Ukizingatia,Wanambeya ni wakarimu sana na huchukia uzembe!!! Na ndiyo sifa mlizonazo!!!!! Hogereni sana!!!!!!!!!
    Asante Mh. Raisi kwa uteuzi huu.

    ReplyDelete