01 December 2010

Hatma ya Mrema mikononi mwa Magufuli

Na John Daniel

HATMA ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Bw. Eprahim Mrema, sasa ipo mkononi mwa Waziri wa Ujenzi, Bw. John Magufuli huku kukiwa na matumaini
makubwa kuwa atatangaza uamuzi huo leo.

Habari za kutoka ndani ya wizara hiyo zilieleza jana kuwa tayari Bw. Magufuli amefanya maamuzi mazito juu ya mtendaji huyo na kwamba atawasilisha mapendekezo yake kwa Rais Jakaya Kikwete leo kabla ya kuwekwa hadharani.

"Juzi (Jumatatu) kulikuwa na juhudi kubwa za Bw. Mrema kutaka kuonana na Waziri Magufuli ili wazungumze zaidi lakini alikataa, akisema anachotaka kwanza ni taarifa za utendaji na majibu ya tuhuma mbalimbali.

"Baada ya kupata majibu aliyotaka amefikia maamuzi mazito sana lakini anataka kwanza kuwasiliana na ikulu kuhusu maamuzi hayo kabla ya kuwekwa hadharani," kilisema chanzo chetu.

Majira ilipomtafuta Bw. Mrema ofisini kwake ilikataliwa kufanya naye mahojiano kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utaratibu aliojiwekea wa kujibu maswali ya wana-habari kwa njia ya maandishi na si kuonana nao.

Katibu Mukhtasi wa Bw. Mrema alimtaka mwandishi wetu kuonana na Ofisa Mahusiano wa TANROADS, Bi. Aisha Malima ambaye alimwelekeza kuandika na kuacha maswali ili apelekewe Bw. Mrema.

"Wewe niandikie tu hayo maswali hapa nimpelekee bosi atayajibu ndio utaratibu wake, nakuomba sana unisamehe tu hata kama unamwona, labda akiamua yeye," alisema Bi. Malima.

Baada ya Majira kuandika maswali hayo ofisa habari huyo aliomba ufuatiliaji wa majibu kufanyika leo kwa kuwa kwa kawaida hutoa majibu si zaidi ya siku tatu.

Majira ilipomtafuta Waziri Magufuli ili kupata ufafanuzi hakupatikana kutokana na kuwa na kikao mfululizo, na baadaye kuondoka kwenda kukabidhi wizara aliyokuwa akiongoza.

Waziri Magufuli alielekeza Majira kufanya mawasiliano na Ofisi ya Habari katika jengo la Wizara ya Uchukuzi.

Hata hivyo wahusika wa ofisi hiyo walirusha mpira kwa Bw. Magufuli kwa maelezo kuwa suala hilo ni zito, hawawezi kuzungumza.

9 comments:

  1. Excellent Dr.Magufuli....Tunataka barabara tu ..ondoa Mrema maEngineer tupo wengi sana Tanzania tunaweza kuongoza hiyo TANROADS....Tutatuma CV zetu ..vigezo tunavyo..

    ReplyDelete
  2. pETRO eUSEBIUS mSELEWADecember 1, 2010 at 9:15 AM

    Tatizo sio Mrema,tatizo ni mambo ashutumiwayo Mrema.Kila la aina hiyo ni tatizo.Tutalikemea,litakemewa na Dr.Magufuli atalikemea.Hatuhitaji maneno matupu kwa hili..it is a serious matter.Ufisadi mbaya jamani.Angalieni mitaani,baada ya wiki nne tu tangu uchaguzi kila kitu kimepanda bei.Maskini wa Tanzania wanaangamia.Zile pesa walizojikopesha kuelekeza kwenye kuwahonga wapiga kura ndo hizo zinazopwaisha uchumi wetu kwa sasa.Marekebisho yanahitajika haraka.Baada ya hapo,kila kitu kitakuwa shwari kabisa.Viva Tanzania!

    ReplyDelete
  3. TUNAKUTAKIA KILLA LA KHERI KTK KAZI YAKO
    DR,MAGUFULI,MUHIMU KUNA WATU WANAJIONA HAPO WIZARANI NA HIVYO VYEO NI VYAO VYA KUDUMU VINAWAPA JEURI NA KIBRI, HUYO JAMAA MREMA HAFAI YEYE KILA KUKICHA KUWAPIGA STOP, NA KUWANYOWA WENZAKE SASA ZAMU YAKE NAE KUNYOLEWA
    WAZIRI MAGUFULI TUNAKUOMBA TATIZO KUBWA LIMEHAMIA KIGAMBONI HUWEZI AMINI SASA TUMERUDIA ENZI YA 2005/2007, HUWEZI VUKA BILA KUKAA ZAIDI YA MASAA MAWILI NI TATIZO INATUBIDI TUTOKE MAJUMBANI ALFAJIRI SAA 11.30 NA UNAWEZA KUVUKA SAA 1,TUNAJUWA TATIZO KWA DAR YOTE LAKINI HUKU SASA NI KERO ZAIDI

    ReplyDelete
  4. Kwani Magufuli hawezi kumshugulikia Hosea pia? atafute kigezo chochote tu ktk jurisdiction yake kama waziri apate kumng'oa na huyo kupe Hosea, Mrema peke yake haitoshi!

    ReplyDelete
  5. Mh. Magufuli unaheshimika kwa utendaji wako usioyumba. Baba, kamilisha kazi uliyoianzisha. TANROADS hiwezi kuwa kichaka cha mafisadi. Tanzania bila ufisadi inawezekana.

    ReplyDelete
  6. Dk.Magufuli anzia mkoa wa Iringa na Wilaya zake ufisadi umezidi..Makandarasi wanapewa nukuu (quotations)na wahandisi wa wilaya kabla hata zabuni hazijatangazwa...Wahandisi wa H/shauri na Wakurugenzi wamekuwa Miungu watu watu....wanatutishia hata sisi Makandarasi kuwa kama hatuna 10%(ten percent)tukachimbe mitaro ila kazi kwao hatuna..Mh.Magufuli wengine ni teller wa bank wanapewa kandarasi za kujenga madaraja bila sifa kwa kuwasaidia wahandisi kupitisha hela za rushwa kwenye akaunti za uongo.Mh.Makyembe upo?

    ReplyDelete
  7. JAMANI, HIVI SERIKALINI HAKUNA UTARATIBU UNAOPASWA KUFUATWA NA WATUMISHI WOTE? utasikia"... ana utaratibu aliojiwekea!!" - WIZI MTUPU!!!. kila mtu akijiwekea utaratibu wake tutafika wapi? Ndio maana mambo hayaendi kama inavyotakiwa, kwa vile kila mtu ana kautaratibu kake!! kuanzaia Kikwete hadi Mrema!

    ReplyDelete
  8. huyu mrema amewekwa kwa maslai ya rostam

    ReplyDelete
  9. Mh.Magufuli unafanya kazi nzuri sana lakini pia uwe makini na hatua unazochukua kwani hao watu wamewekwa na watu walio juu yako, soma wakati pia, yasijekukuta ya Samweli Sita. J.J.K - Iringa TZM.

    ReplyDelete