LONDON, England
KOCHA Arsene Wenger amesema nahodha wa Arsenal, Cesc Fabregas huenda akakaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki zaidi ya tatu, baada ya kuumia misuli ya paja wakati wa mechi ya
michuano ya Klabu Bingwa Ulaya, ambayo juzi timu hiyo ilipata kichapo kutoka kwa timu ya Braga ya Ureno.
Katika mchezo huo ambao timu hiyo ilifungwa mabao 2-0, Fabregas alitolewa uwanjani dakika 69 sambamba na mwenzake, Emmanuel Eboue ambaye naye pia alikumbwa na majeraha ya goti.
"Eboue atakuwa nje ya uwanja wakati kesho (jana), tukimwangalia Fabregas," Wenger aliiambia tovuti ya klabu hiyo baada ya mechi.
"Inaweza kuwa ni muda wa wiki mbili ama tatu. Inachanganya mno kwa sababu kabla ya mechi tulitarajia kucheza naye muda mrefu, lakini amepata majeraha na hili ni pigo kubwa kwetu," alisema.
Jumamosi wiki hii Arsenal, inakutana na Aston Villa katika michuano ya Ligi Kuu na Wigan Athletic katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Ligi.
No comments:
Post a Comment