Na Amina Athumani
MCHEZAJI gofu Hassan Ally, ameibuka kidedea katika mashindano ya gofu ya mwisho wa mwezi yaliyodhaminiwa na Kambuni ya simu za mkononi Zantel, yaliyofanyika juzi kwenye viwanja vya
Gymkhana, Dar es Salaam.
Ally aliibuka kidedea kwa kupata pointi 69 kwa wachezaji wenye kiwango A, akifuatiwa na Pembe Kondo aliyepata jumla ya pointi 69.
Katika kiwango B, nahodha wa klabu hiyo, Joseph Tango alishika nafasi ya kwanza kwa pointi 67, Lawrence Pangani alishika nafasi ya pili kwa pointi 69 na kiwango C, Abdallah Mashausi alishika nafasi ya kwanza kwa kupata pointi 72 na Hashain Rahim alishika nafasi ya pili kwa kupata pointi 73.
Kwa wanawake nafasi ya kwanza ilikwenda kwa Violet Peter, aliyepata pointi 71 akifuatiwa na Maniwe Pangazi aliyepata pointi 74 na kwa wachezaji wakongwe nafasi ya kwanza ilikwenda kwa Monabe Nyirabu aliyepata pointi 70 na Joseph Tairi alikusanya pointi 74.
Akikabidhi zawadi kwa washindi katika hafla iliyoandaliwa na Zantel, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Nomarn Moyo, alisema amefurahi kuona wachezaji wengi zaidi ya 100 kujitokeza katika mashindano hayo na wamepata nguvu ya kuendelea kudhamini mashindano hayo, ili kuweza kuibua vipaji vingi kwa vijana.
"Tutaendelea kudhamini mashindano haya ya gofu na pia tutadhamini ya kumtafuta mshindi wa Desemba, ili kuendelea kuimarisha na kuboresha mchezo huu," alisema Moyo.
No comments:
Post a Comment