16 August 2012

Mzee miaka 64 amtawiti mtoto wa miaka 4



Na  Patrick Mabula, Kahama
 
JESHI la Polisi Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, linamshikilia mkazi wa Kijiji cha Shunu, Kata ya Nyahanga, Bw. Manyanda Katulie (62), kwa kosa la kumlawiti mbaka mtoto wa miaka minne.

Taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Everist Mangalla, ilisema Bw. Katulie anadaiwa kufanya kosa hilo juzi jioni katika kijiji hicho baada ya kumrubuni mtoto huyo na kumlawiti.

“Watu walisikia mtoto huyu alikilia kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata na kwenda kumpa msaada,” alisema.

Kamanda Mangalla alisema, Bw. Katulie alimrubuni mtoto huyo wakati akitoka kucheza na wenzake na kuongeza kuwa, uchunguzi wa tukio hilo ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

1 comment:

  1. Yale yale!!! Hebu soma hizi sentensi:
    "Mzee miaka 64 AMTAWITI mtoto wa miaka 4"

    'kwa kosa la kumlawiti mbaka mtoto wa miaka minne'.

    Halafu kichwa cha habri miaka 64, kwenye habari yenyewe miaka 62!!!

    Hawa kweli ni watu makini waliosomea kazi hii?

    ReplyDelete