23 January 2012

Ilala yaamisha taka zilizokaa muda mrefu

Heri Shaaban

TAKATAKA zilizokuwa zimetelekezwa katika eneo la shule ya msingi Kisukuru Kimanga
na kulamamikiwa na wakazi wengi zimeondolewa na Manispaa ya Ilala.
Akizungumza mara baada ya kumaliza mpango wa kuhamisha taka hizo, Ofisa Usafishaji Ilala,Bw.Samwel Bubegwa alisema kuwa manispaa imeweka upelelezi kwa atakayeonekana akitupa taka.
"Manispaa yangu inafanya upelelezi wake ili kubaini magari yaliyokuwa yana mwaga taka eneo la shimo hili ambalo lipo jirani na makazi ya shule na wananchi na wahusika wakipatikana watapelekwa katika vyombo vya sheria,"alisema Bubegwa.
Alisema kuwa manispaa hiyo tayari imechukua hatua mbalimbali zikiwemo za kupulizia dawa katika vyumba vya madarasa ya shule ili kuuwa wadudu ili wanafunzi waweze kusoma.
Bw.Bubegwa alisema magari hayo ya taka yalikuwa yakitumia upenyo wa kumwaga taka eneo hilo kutokana na kuwa na shimo kubwa bila wahusika kufahamu.
Pia alisema kuwa kila wiki manispaa hiyo imeweka utaratibu wa kuondosha taka katika mitaa kwa kutumia magari ya manispaa ikiwa ni pamoja na kuweka kila mtaa kasha la uchafu.
Kwa upande wake mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kisukuru, Bw.Josephat Sambua alisema kuwa hali ya hewa katika shule hiyo ilibadilika kutoka na uchafu huo kuwa karibu na shule na wanafunzi kushindwa kusoma.

No comments:

Post a Comment