23 January 2012

CHADEMA yajibu mapigo

*Yakana kutumiwa na Ujerumani
*Dkt. Slaa asema mpaka kieleweke
*Sengerema wamvaa Ngeleja


Na Zena Mohamed

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekanusha tuhuma dhidi yao kwamba
, kinapokea fedha za msaada kutoka Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la Ujerumani ili kuchochea maandamano na kuvuruga nchi.
Akizungumza katika semina ya dharura ya umuhimu wa  mabadiliko ya hali ya hewa kwa sera ya upinzani, viongozi na wanakamati wa CHADEMA, katibu mkuu wa chama hicho Dkt. Willbrod Slaa alikiri kwamba, chama hicho kinapokea fedha kutoka KAS na kwamba, ni kwa ajili ya mambo ya maendeleo ya jamii.
"CCM imekuwa ikishutumu CHADEMA kwamba tunapokea fedha kutoka KAS kwa ajili ya kuchochea vurugu, madai haya sio ya kweli," alisema Dkt. Slaa na kuongeza
"Sisi tunawahaidi wananchi kwamba, tutaweka pamba masikio na kutoogopa maneno yao hadi kuweza kuitoa nchi mahali ilipo sasa kwenda kwenye neema kwani maisha bora kwa Mtanzania hayapatikani kwenye jukwaa la siasa," alisema.
Alisema, chama hicho kimeitisha semina hiyo na Kamati Kuu ya Wataalam wa Mazingira ili kujadili na kupata tathimini jinsi ya kutunza mazingira kwa lengo la kupata nyaraka sahihi kuhusu mazingira pindi watakapokutana kwa mara nyingine.
Mkurugenzi wa KAS Bw. Stefan Reith alisema, shirika lake limeshawishika kukisaidia chama hicho kutokana na kuonesha mwelekeo mzuri katika kusaidia wananchi.
Alisema, kwa mtazamo wa KAS, CHADEMA ndio chama kilicho na mwelekeo wa maendeleo nchini hasa katika suala la  mazingira.
Bw. Reith alisema, hawawezi kulala hadi pale chama hicho kitakapowe kitakapoweza kuboresha uhuru wa wananchi katika sehemu zao za kazi na sio kufanya kazi bila kupumzika kama ilivyo sasa.   
Katika Bunge la kufunga ngwe ya Awamu ya Kwanza ya Rais Jakaya Kikwete kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka juzi, Waziri wa Mambo ya Nje Bw. Benard Membe aliwaambia wandishi wa habarik kuwa, wapo baadhi ya mabalozi nchini wanaijishughulisha na siasa za nchini.
Alisema, baadhi yao wamekuwa wakiweka mikakati na vyama vya upinzani ili kuiangusha CCM na kwamba, kitendo hicho ni kinyume na sheria za nchi.
Pia alisema, serikali haitakuwa tayari kuona mabalozi hao wanakuwa chanzo cha migogoro ndani ya nchi na kwamba, yoyote atakayebainika atawajibishwa kulingana na sheria za nchi.
Katika suala la kulinda mazingira, Dkt. Slaa aliitaka serikali kuwa makini katika mabadiliko ya hali ya hewa katika nchini kwasababu maisha bora hayaji bila mikakati sahihi ya kutunza mazingira.
Pia aliitaka serikali kutekeleza yale yanayotakiwa ikiwa ni pamoja na kukabiliana na majanga makubwa yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa. kudhibitiwa kwa kuchukua hatua ya kujenga nchi kwa kuitunza ndipo nayo iwatunze.
Wakati huo huo Gabriel Moses anaripoti kwamba, CHADEMA imepinga vikali madai ya kupokwa kwa viongozi wake wa ngazi za juu mkoani Shinyanga.
Kaimu Mwenyekiti wa CHADEMA, Sengerema Bw. Said Shaaban alisema jana kuwa, taarifa zilizoenezwa na Waziri wa Nishati na Madini Bw. William Ngeleja ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema (CCM) kuhamisha uongozi wote wa juu wa CHADEMA Wilaya ya Sengerema hazina ukweli wowote.
"CHADEMA Wilaya ya Sengerema tunapinga uzushi huo. Tunajua kuwa uzushi huo ni sehemu tu ya mpango na mkakati ambao CCM inafikiri itaweza kujinusuru, kuwasahaulisha na hatimaye kuirejesha Kanda ya Ziwa katika Nchi ya Misri, baada ya watu Kanda ya Ziwa kuonesha kasi ya ajabu kuikimbia nchi hiyo ya mateso kwenda nchi ya ahadi," alisema.
Alisema, CHADEMA ililazimika kutopuuza uzushi huo kwa kuwa, malengo yake ni kutaka kuwavunja nguvu wananchi na wanachama wa chama hicho.
Hivi karibuni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bw. Hamis Mgeja alidai kuwarudisha kundini viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho kwa lengo la kuiongezea nguvu CCM.
Miongoni mwa watu waliotajwa kujiunga na CCM ni pamoja na Bw. Ayub Thomas Malima aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Sengerema, Bw. Sarah Mathayo aliyekuwa Katibu BAWACHA na Bw. Kesy Misalaba.

No comments:

Post a Comment