*Mpendazoe asema walinadiwa na JK ni wachapakazi
Na Waandishi Wetu
KADA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Fred Mpendazoe amebeza hatua ya Chama Cha Mapinduzi kuwatosa makada wake
maarufu kwa kinachoelezwa ni kuvua gamba akiita hatua hiyo ni ufaniki
Bw. Mpendazoe alitoa kauli hiyo juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika juzi kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Yombo, ukiwa na lengo la kuwashukuru wananchi kwa kuwachagua wagombea wa chama hicho ambapo viongozi mbalimbali wakiwemo wa kitaifa walihudhuria.
Kauli hiyo ilitolewa wakati mwanasiasa huyo akizungumzia kujivua gamba kwa CCM, ambapo alibainisha kuwa ni unafiki wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kuwalazimisha kujiuzulu wajumbe wake, Bw. Edward Lowassa, Bw. Andrew Chenge na Bw. Rostam Aziz.
Kutokana na maamuzi hayo yalitolewa takriban miezi minne iliyopita, Bw. Aziz alijizulu hivi karibuni, ikiwa ni miezi mitatu iliyotangazwa na chama hicho kuwa ndio ukomo wa kuwataka kujitoa, vinginevyo wangechukuliwa hatua.
Hata hivyo Bw. Aziz aliwatupia lawama Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Bw. Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu (Bara), Bw. John Chiligati kwa 'siasa za ovyo' za kuwachafua watuhumiwa hao, kinyume na maamuzi ya NEC.
Akizungumzia hali hiyo, Bw. Mpendazoe alisema kuwa CCM imekuwa ikiwataka wale wote wanaotajwa ni mafisadi au kuhusishwa na kashfa ya ufisadi kujiuzulu wenyewe kabla hawajafukuzwa, akishangaa kwa nini Rais Jakaya Kikwete asijiuzulu kwa kuwanadi watu hao majimboni kwao kuwa watu safi.
Alisema wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana, Rais Kikwete alizunguka kwenye majimbo ya watuhumiwa hao na kuwanyanya mikono kila mmoja kwa wati wake aakiwataka wananchi wawachague kwa kuwa ni watu wazuri, na tegemea la chama, iweje leo waibuke na kusema hao si wasafi.
Bw. Mpendazoe aliyewania ubunge katika Jimbo la Segerea na kushindwa na Bw. Makongoro Mahanga, alihoji, "Kama kweli wanaotajwa kuhusika na tuhuma mbalimbali wanatakiwa wajivue gamba, iweje Rais Kikwete naye asijiuzulu kwa kuwa naye alitajwa katika orodha ya Mwembeyanga?"
Alisema ulipochaguliwa na wananchi na kupewa madaraka ya kuwaongoza si lazima ang'ang'anie hadi miaka mitano imalizike, ni vema akamwaga unga kwa kuwa nchi imemshinda wazi na hata mawaziri wake wamefikia hatua ya kukinzana na maagizo yake.
"Ukiona familia yako inakupinga hadharani ujue una kasoro, ndivyo ilivyo kwa Rais Kikwete anapingwa na mawaziri wake hadharani tena ndani ya bunge na kwenye majimbo yao," alisema.
JK alivyonukuliwa
Mwaka jana wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, akiwa mgombea wa CCM, Rais Kikwete alifika katika majimbo ya Monduli na Igunga, ambako kote aliwanadi waliokuwa wagombea ubunge, Bw. Lowassa na Bw. Aziz, huku mkewe, Mama Salma Kikwete akienda katika Jimbo la Bariadi Magharibi kumpigia kampeni Bw. Andrew Chenge.
Akiwa jimboni Monduli, Rais Kikwete alinukuliwa akimsifia Bw. Lowassa kuwa ni mchapakazi na kuwa tuhuma dhidi yake zilikuwa ni za uongo na kupakaziwa. Kauli ambayo iliibua mjadala mkubwa miongoni mwa jamii, ikidaiwa kulidharau bunge ambalo liliridhia kujiuzulu kwake ubunge, kutokana na kashfa ya Richmond.
Akiendelea na kampeni zake za kuwania urais, Rais Kikwete akiwa jimboni Igunga, alimnadi aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM, Bw. Aziz, ambaye pamoja na kuandamwa na tuhuma kadhaa, ikiwemo ya Richmond na Dowans, alifananisha uwezo wake sawa na timu nzima ya mpira iliyokamilika.
Katika kampeni hizo hizo, Rais Kikwete pia alinukuliwa akimsifia Bw. Basil Mramba anayekabiliwa na mashtaka ya kutumia madaraka vibaya, kuwa ni sawa na shoka la zamani lisiloisha makali.
Katika mkutano huo, chama hicho kiliwahamasisha mamia ya wananchi wa Jimbo la Segerea kushika vichwa na ikiwa ni ishara ya kuilaani serikali ya CCM kwa kushindwa kutimiza ahadi za zake.
Mkutano huo ulitawaliwa na ulinzi mkali wa polisi ukiwa wa kwanza kufanyika katika jimbo hilo tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010
Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa Kata ya Kiwalani, Bw. Gervas Barandaje alisema kuwa moja ya matatizo yanayowakabili wananchi ni kutokuwa na shule ya kata, miundombinu mibovu ya barabara.
Naye aliyekuwa mgombea wa jimbo la Segerea, Bw. Fred Mpendazoe alisema kuwa vitendo vya kubebana kwa CCM vimeanza kuwagonganisha vichwa wenyewe kwa wenyewe na kusababisha serikali nzima kuyumba na kukosa mwelekeo kwa wananchi waliokuwa na matumaini.
Bw. Mpendazoe alisema mwisho wa Dkt. Mahanga kupata ubunge ilikuwa mwaka jana kwa kuwa serikali iliyopo madarakani ni ya kubebana kwa kuchakachua matokeo ya uchaguzi.
"Ninavyomfahamu Dkt. Mahanga hawezi kupata ubunge ndani ya Tanzania hii, mwaka jana ulikuwa mwisho wake wake wa kusimama kwenye majukwaa na kuomba nafasi hiyo," alisema.
Bw. Mpendazoe aliwataka wananchi kununua kitabu chake cha 'Tutashinda' ambacho kinaelezea hali ya ufisadi nchini, mwenendo wa CCM, nchi inakotoka na inakokwenda pamoja na jinsi CCJ ilivyoanzishwa na vigogo wa CCM, akiwemo aliyekuwa Spika wa Bunge Bw. Samuel Sitta.
Alisema kuwa hivi sasa wananchi wamefanywa wakishangilia umeme unapokatika na kuwafananisha na watoto wa vijijini wanaoshangilia mbio za mwenge unapopita katika maeneo yao.
Pia alilaani kitendo cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. David Jairo kkupewa likizo ya malipo ili achunguzwe badala ya kumtimua kazi.
Mkutano huo ulitarajiwa kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Willibrod Slaa ambaye aliwakilishwa na Mkurugenzi Oganizasheni ya Mafunzo Makao Makuu, Bw. Benson Singo ambaye alisema kuwa hivi sasa Watanzania wanaishi kama kuku wa kienyeji wanaohangaika kujitafutia mlo wao wa siku.
Bw. Singo alisema kuwa serikali imeshindwa kuwaondolea matatizo walimu kwa sababu fedha nyingi zilikuwa zikitengwa kuwahonga wabunge ili kupitisha bajeti katika wizara mbalimbali ambazo hazina tija kwa wananchi.
Alisema kuwa msimamo wao juu suala la umeme ni kutaka bajeti yote ya serikali ianzwe upya ili vipaumbele viangaliwe upya.
Hata hivyo, aliwataka wananchi wasitoa malalamiko yao juu ya maisha kuwa magumu kwa sababu ni mavuno yao kwa kile walichokipanda mwaka jana wakati wa uchaguzi na kuwataka iwe fundisho la kubadili mwelekeo ifikapo mwaka 2014 kuanzia chaguzi za serikali za mitaa hadi kwa diwani, wabunge na rais.
Katika mkutano huo vijana 230 walijitokeza kuchukua kadi za uanachama chama hicho na kuahidi kuwa mabalozi katika maeneo yao huku wengine wakirudisha kadi za CCM.
HIVI MPENDAZOE WEWE NI MWANASIASA AU MPIGA DOMO?
ReplyDeleteKoma wee, Mpendazoe kavaa kanga ya mama yako hivyo muheshimu shwaini wee!
ReplyDeleteNa mama yako kavaa kanga ya nani? ni malaya tu. HAWA WANASIASA UCHWARA NDIO WALIOLETA BALAA LA UMEME NA RICHMOND HIYO NDIYO NDIYO INAYOOKOA TAIFA SAA HIZI VINGINEVYO NCHI INGEKUWA KIZANI. HUYO NI MNAFIKI KAISHA,MBONA HAKWENDA KWAO KUGOMBEA?
ReplyDeleteNinamshangaa sana huyu mtu anayebeza hizo hoja za Mpendazoe.Kwani lipi alilodanganya mbona unakuwa kama litoto,kuzomea tu mambo ya ajabu?Hata kama wewe nikipofu ni kiziwi pia?Nakwambia hii inchi lazima ikombolewe kutoka mikononi mwawanyang'anyi kwa hali yoyote ile. BONY
ReplyDelete