Na Mariam Mziwanda
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania (Bara), Philip Mangula
ameshangazwa na chama hicho kuwa na ‘jeshi’ kubwa la wanachama, lakini
linazidiwa nguvu na jeshi dogo la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
hatua ambayo imemfanya aamke na kusoma alama za nyakati kwa kuwarudia wananchi.
Akizungumza na
Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Dar es
Salaam pamoja na waandishi wa habari jana kabla ya
kuanza ziara yake jijini, Mangula alisema;
“CCM ina jeshi
kubwa la wanachama lakini linashindwa na jeshi dogo la CHADEMA ambalo halina
hata anuani... hivyo nimeona ipo haja kurudi kwenu kuanzia ngazi ya chini
kupitia matawi, shina na wananchi mnieleze tatizo ni nini?”
Alisema ili
kufikia wananchi nkoani Dar es Salaam, atafanya ziara katika wilaya zote za
mkoa huo na kukutana na watendaji, wanachama na wananchi kwani kila mwana CCM
ni askari wa mstari wa mbele, lakini anashangazwa na nguvu ndogo iliyopo sasa.
“Chama kikiwa
na nguvu ndipo na Serikali inavyokuwa na nguvu, umefika wakati tuelewe kuwa ni muhimu
chama kiwasemee watu na si viongozi wa chama wakisemee; hivyo uhai wa chama ni
jambo muhimu kwa wana CCM,” alisema
Alieleza kuwa
makundi yaliyotokana na uchaguzi wa 2010 ndani ya chama hicho, bado yapo na
yanaendelea kwa kasi, hali iliyoathiri zaidi Chama mpaka kufikia mwaka 2012,
hivyo mkakati wa kujua vipi yaondolewe pasipo kuathiri zaidi 2014 mpaka 2015
unahitaji kuwepo na mipango imara.
Mangula alisema
katika ziara yake hiyo ya mafunzo ambayo imetokana na kutambua kuwa nguvu ya
chama ni uwepo wa wanachama, atatenga muda mwingi kuzungumzia changamoto
zinazowakabili na kuwagawa wana CCM.
Alisema kwa kufanya hivyo atapata sababu
zinazokwamisha maendeleo ya chama hicho. Alihimiza wana CCM kuelewa kuwa katika
wiki ya maadhimisho ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius
Nyerere, ipo haja kuenzi harakati zake kwa kukiongezea nguvu chama.
Mangula alisema
kujenga chama kunahitaji kujitoa hata kufikia kuacha nafasi ya madaraka kama alivyofanya Mwalimu Nyerere.
“Wakati wa wiki ya Kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere ni muhimu kuwa na chama chenye nguvu na kujitoa kwani Mwalimu
aliacha hata nafasi ya Uwaziri Mkuu na k umuachia Mzee Rashid Kawawa kwa lengo
la kurudi katika kazi za ujenzi wa chama na pia tukumbuke Mwalimu aliacha kazi
ya Urais mwaka 1985 na nafasi yake kuchukuliwa na Rais Mwinyi, ambapo yeye
alirudi tena kufanya kazi za chama hivyo kukijenga chama kunahitaji kujitoa ili
kiweze kuwa na nguvu kubwa,” alisema
sasa tangia Mwalimu Nyerere achie madaraka na kujenga chama atuambie mwengine nani alie fanya hivyo.nadhani Bw Mangula sababu ya kuanguka kwa CCM ni ulevi wa madaraka ulioigupika CCM pamoja na UFISADI unaolindwa.
ReplyDeleteKINACHOTAKIWA NA KILA CHAMA NI KUFANYA CHAGUZI KUANZIA NGAZI YA KATA HADI TAIFA ILI KUPATA UWAKILISHI HALALI NA WA KIDEMOKRASIA KINYUME CHAKE MAKUNDI YA KIHUNI TU NI SAWA NA KUWAPA SERIKALI WAHUNI WA LIBYA NA MISRI MPAKA LEO HAKUNA AMANI WALA UTENGAMANO ILA MATAIFA YA MAGHARIBI WANAFURAHIA KWANI FURSA NZURI YA KUIBA RASILIMSALI ZA AFRIKA NI VEMA KUWACHUNGUZA VIBARAKA WA NDANI KAMA AKINA CHANGIRAI WA ZIMBABWE MBONA KAANGUKIA PUA SIKU ZA MNAFIKI NI CHACHE KILA MBUNGE ATATOA HESABU 2015 NI NANI ALIYEPANDA MBEGU NA NINANI ALIYEPANDA UPEPO
ReplyDeleteKutoa hesabu ni kwa wote haijalishi uko tawala ama upinzani. Ueleze umehamasisha vipi maendeleo katika jimbo lako. Sio umahamasisha maandamano na na chuki vipi katika taifa lako
Deletehivi bado kunawatu wanatumia kichwa kufugia nywele nili na wapi na nani uliona kafanya maandamiano ya chuki au yasiyo na tija kojoa ukale.
ReplyDelete