Na Daud Magesa, MWANZA
WIZARA
ya Maliasili na Utalii, imesema mwaka jana hadi Juni, mwaka huu watu 27
waliuawa na fi si na wanne kujeruhiwa na wanyama hao. Pia fi si 22 wanaodaiwa
kujeruhi na kuua watu waliuawa mkoani Geita katika kipindi cha mwaka jana hadi
Juni mwaka huu. Kutokana na matukio hayo,
Wizara hiyo kupitia wataalamu wake,
iliamua kutoa elimu kwa wananchi katika vijiji mbalimbali vya Mikoa ya Mwanza na
Geita vinavyokabiliwa na changamoto hiyo. Katika mkakati huo vijiji saba vya
Senga, Burigi, Katoma, Nyaboge, Sungusira, Igate na Lwenzera vilivyoko mkoani
Geita vimenufaika na elimu hiyo ya kujikinga na wanyama hao.
Akizungumza na wakazi wa vijiji hivyo jana na juzi, mwakilishi wa
Wizara ya Maliasili na Utalii, Uenezi Makao Makuu, Twaha Twaibu alisema elimu kama hiyo imetolewa katika vijiji vya Wilaya za Magu na
Ilemela mkoani Mwanza. Twaha, alisema familia 93 za waliopata madhara baada ya
kujeruhiwa na wanyama wakali wakiwemo fisi walilipwa na Serikali fidia ya sh. Milioni
49,200,000 katika kipindi cha mwaka 2012/2013 kwa mujibu wa kifungu cha 71 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na.5 ya mwaka
2009.
Alisema elimu hiyo kwa wananchi inatolewa kwa njia ya mikutano ya hadhara
na sinema za kuonesha tabia za wanyama na inalenga kubaini chanzo cha tatizo, ambapo watoto wengi hawamfahamu fi si na
wanafananisha na mbwa, kitu ambacho si kweli. Benjamini Kijika, ambaye ni Mkuu
wa Kikosi ya ujangili Mwanza na Samweli Nyakonga, Ofisa wanyamapori wa Wilaya
ya Geita kwa nyakati tofauti waliwaeleza wananchi wa vijiji hivyo kuwa taarifa
zilizopo zinaonesha kuongezeka kwa matukio ya wanyamapori ya kushambulia na kuua
binadamu hasa watoto.
Alisema Wizara kwa kuliona tatizo hili imeamua kuwaelimisha wananchi
jinsi ya kujikinga na wanyama hao na tabia zao ambao huwinda nyakati za usiku na
kuwatahadharisha wananchi wazingatie elimu inayotolewa.Twaha alisema wananchi wanapaswa
waone umuhimu wa kuwalinda wanyamapori na mazingira yake hasa wanapokuwa hawaleti
madhara,na kuonya vitendo vya ujangili vinavyofanywa na baadhi ya wananchi
kuwinda kama swala na wengineo huwakosesha fisi kitoweo na matokeo yake kuvamia
mifugo na binadamu chakula mbadala Kuhusu suala la fi si kuhusishwa na
ushirikina, Twaha alisema ëJambo hili amelisikia siku nyingi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, hata hivyo hakuweza kulizungumzia kwani
hana ushahidi wa suala hili.Kijika aliwaeleza wananchi wa vijiji hivyo kuwa
suala la kusaka fi si limekuwa na vikwazo,yeye kama
mtaalamu ameshindwa kuelewa na kuhisi kuna masuala ya ushirikina kuhusu fi si
hao.
No comments:
Post a Comment