Neema Rajab na Flora
Nkya (TUDARCO)
KATIBU
Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Uledi Musa, amelitaka Shirika la Viwanda
Vidogo Vidogo nchini (SIDO) na kampuni binafsi za biashara kushirikiana na
Shirika la Viwango vya Tanzania (TBS) ili kuwahamasisha matumizi ya viwango vya
ubora vya kimataifa
.Kauli hiyo
ilitolewa Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu huyo, kwa niaba ya Waziri wa
Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda, wakati akifungua semina ya siku moja
iliyoshirikisha wadau mbalimbali kuhusu jinsi ya kutumia kiwango cha Shirika la
Viwango la Kimataifa (ISO) 26,000 cha Uwajibika wa Kijamii nchini Tanzania.
Lengo la semina
hiyo lililenga kueleza kampuni husika kuwa karibu na jamii wakati zinapotoa
maamuzi na kuchukulia umuhimu wa kutunza mazingira, namna ya kufanya kazi na
jamii, utii wa sheria bila shuruti ili kuwa na jamii ya Watanzania iliyo
endelevu.Alizitaka
kampuni na mashirika mbalimbali kujali jamii ambayo ndiyo wanunuzi wakuu wa
bidhaa zao na si kujali uzalishaji wao peke yake, japo yote mawili yana mantiki
kuongeza mapato.
Aliwaambia
washirika wa semina hiyo kuwa zipo faida mbalimbali za wao kushirikiana na TBS
na ISO wakati wa uzalishaji wa bidhaa zao, kwani hatua hiyo itawasaidia
kutambulika kimataifa na kijipatia soko la bidhaa zao.
"Ma k amp u n i b i n a f s i n a
mashirika ya serikali yanakabiliwa na changamoto ya kufilisika na kushindwa
kuendeleza huduma zao kwa jamii kutokana na umaskini na mabadiliko ya hali ya
hewa, lakini kwa kushirikiana na TBS na ISO ni rahisi kukabiliana na changamoto
hizo kwani lengo ni kuisaidia jamii," alisema Kaimu Mkurugenzi wa
Uendelezaji Viwango wa TBS, Theresia Kessy kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa
TBS, Joseph Masikitiko.
Taasisi ambazo zimeshajiunga kutumia
kiwango hicho ni Vodacom Tanzania,Benki ya CRDB, Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA), Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM).
Kwa upande wake Ofisa Viwango wa
TBS,Geofrey Thomas, alisema lengo la semina hiyo ilikuwa ni kueleza kampuni
umuhimu wa kuwa karibu na jamii wakati wa kufanya maamuzi. "Watanzania
wabadilishe mtazamo kuhusiana na jinsi ya kuhamisha matatizo yanayowazunguka
ndani ya jamii na kuyaweka katika biashara yako," alisema.Alisema
kiwango hicho namba 26000 kimeanza kutumiwa na makampuni matano nchini na
kwamba kwa nchi za Afrika Mashariki kinatumika nchi za Tanzania, Uganda na
Kenya.
No comments:
Post a Comment