Na Omari Moyo, Arusha
UKWEPAJI wa kodi unaofanywa na
wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu katika halmashauri ya jiji la Arusha
kunachangia manispaa hiyo kupata hati chafu mara kwa mara.Kauli hiyo
ilitolewa na Mkurugenzi wa Jiji, Sipora Liana, wakati akizungumza na waandishi
wa habari. Alisema kuwa mianya yote iliyokuwa ikichangia kuingiwa kwa mikataba
'feki' katika miradi ya jiji hilo na ambayo imeiletea jiji hilo hasara kubwa
pamoja na ukwepaji kodi itazibwa.
"Nimejichagua
mwenyewe kuwa mwenyekiti wa kamati ya mapato ya halmashauri ili kufuatilia kila
mahali tunapostahili kulipwa na tumeanza kuona mafanikio; tulikuwa tukipata sh.
milioni 400 kwa mwezi; miezi miwili tu iliyopita tumefikia sh. milioni 800 na
tunaendelea," alisema Liana.
Aliongeza
kwamba, hakutakuwa tena na mikataba ambayo haifuati kanuni wala taratibu na
hivyo tenda yoyote na mradi wowote wa halmashauri ya jiji la Arusha haitatolewa
kwa kufahamiana wala umaarufu wa mtu wala kupindishwa kwa sheria.
Kutokana na
kuongezeka kwa mapato hayo, watajenga mdarasa 39, ya shule za sekondari ili
wanafunzi wa mwakani wasikose madarasa ya kusomea pia watanunua magari ya
kubebea takataka pamoja na magari makubwa ya ujenzi barabara.Alisema
kuwa, yeye madiwani na watendaji wengine wa jiji la Arusha wamejipanga vilivyo
kuhakikisha maendeleo katika jiji hilo yanakua kwa kasi ya aina yake.
No comments:
Post a Comment