30 July 2013

ZIMAMOTO KUBORESHA HUDUMA DAR



JESHI la Zimamoto nchini linafanya maandalizi ya ujenzi wa vituo vya Zimamoto vya kikanda katika Jiji la Dar es Salaam ili kusogeza huduma kwa wananchi, anaripoti Charles Lucas. 
 Akizungumza wakati wa hafla ya kuwapandisha vyeo baadhi ya maofisa wa jeshi hilo, Dar es Salaam jana Naibu Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Luteni Kanali Saimon Mgumba alisema ili kuboresha huduma kwa wananchi watajenga vituo visivyopungua vitano jijini.

Kamishna huyo alisema, kwa kuanzia utekelezaji wa mpango huo maeneo yaliyopangwa kujengwa ni Mbagala, Lugalo, Gongolamboto, Mwenge, Kigamboni na Mabibo na siku zijazo vituo vitajengwa katika maeneo mengi zaidi.
Pia aliwaomba wananchi ushirikiano yanapotokea majanga ya moto ili kazi ya kuudhibiti kuwa rahisi na kuonya baadhi ya watu wenye tabia ya kupiga simu katika jeshi hilo na kutoa lugha za matusi na kejeli kuwa kuanzia sasa watachukuliwa hatua za kisheria.
“Tumekuwa na wakati mgumu katika utendaji tunapigiwa simu zaidi ya matukio 20 ‘hewa’ ni hasara kwa taifa tunatumia fedha kufika maeneo ambayo hakuna tukio, hivyo tumefunga mitambo ya kutambua watu wanaofanya mchezo huo mchafu,” alisema.
Upandishaji wa vyeo kwa maofisa hao wanaotoka mikoa mbalimbali ni mwendelezo wa maboresho ya jeshi hilo linalojetegemea katika utendaji wake zaidi ya maofisa 500 wamepandishwa vyeo hivi karibun

No comments:

Post a Comment