Na Fatuma Mshamu
MAMLAK
Ay aMapatoTanza ni a(TRA ),im et angazakua nzakw amfumompyawaulipajiwa adaz
amagari kwa mwakakwanjiaya mt andaoutakaoa nzakutumika Agosti Mosi mwakahuu .Hayoyame ele
zwajanajijini Dar es S alaamnaMku rugen zi waHudumana Elimu kw aMlipakodi
Richard Kayomboa lipokuwaaki elezamabor eshoy amfumowakielek tronikiamba om
amlaka hiyo inaendelea kufanya ikiwa ni juhudi za kuboresha huduma kwa
walipakodi.
Alisema mfumo
huo utatumika kulipa ada za mwaka za magari ambapo mlipakodi anaweza kupata
taarifa ya kiasi cha kodi anachotakiwa kulipa. “Mfumo huu ni
rahisi kutumia na utapunguza misongamano isiyo ya lazima katika mamlaka ya
mapato na mabenki na hivyo kumwezesha mlipakodi kulipa ada ya gari lake akiwa
mahali popote nchini pia mfumo huu unapanua wigo wa njia za kulipa kodi na
mlipaji yuko huru kuchagua njia aipendayo”, alisema kayombo.
Alisema malipo haya yanaweza kufanyika
kwa njia ya M-pesa, Tigopesa, Airtel Money na kwa wakala wa Maxmalipo ambapo
hurahisisha kazi katika ofisi yoyote ya TRA kwa kupewa stika ya kuonyesha namba
ya kumbukumbu iliyotumika kufanya malipo.
“Ili kuweza kuchukua kadi ya gari,
mlipa kodi anatakiwa kuwa na leseni ya udereva au hati ya kusafiria, pia mfumo
huu ni muendelezo wa maboresho ya mfumo wa kulipa kodi kwa mtandao (revenue
gateway) uliobuniwa na TRA kwa kushirikiana na Benki Kuu (BoT),” alisema
Kayombo.Aliongeza
kuwa, wananchi wote wanaolipa ada za magari huitumia fursa hiyo ya kulipa kodi
kwa njia ya mtandao ili waweze kuendelea vema na shughuli za ujenzi wa Taifa
badala ya kutumia muda mwingi katika misururu kwenye mabenki.
Sasa wale "vishoka" wa pale TRA - Moshi wataishije? Na wale wafanyakazi wa TRA - Moshi waliowajiri "vishoka" hao nao wataponea wapi? Au wataishia kubuni mbinu nyingine nini!! Hebu tusubiri; yetu macho kwani mvunja nchi ni mwananchi!!!!!
ReplyDelete