08 January 2013

Majaji,mahakimu watakiwa kufuata maadili ya kazi



Na Grace Ndossa

JAJI Mkuu Othuman Chande amewataka majaji na mahakimu kufuata maadili na miiko ya kazi ili kurudisha imani kwa wananchi.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana alipokuwa anafungua mkutano wa mwaka  pamoja na kuzindua kitabu cha sheria chenye mrundikano wa kesi mbalimbali pamoja na majarida yenye makala za sheria zilizoandaliwa na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA)

Alisema majaji pamoja na mahakimu wanatakiwa kufuata maadili ya kazi kwani hiyo ni suala muhimu sana katika mahakama ili kurudisha imani kwa wananchi

"Mahakama ni chombo muhimu sana kinachosimamia haki na kutoa maamuzi hivyo majaji mahakamu na watumishi wengine wa mahakama lazima wazingatie miiko na maadili ya kazi,"alisema Bw. Chande.

Pia alisema kuwa kuzinduliwa kwa vitabu hivyo vyenye kesi mbalimbali kutasaidia kupunguza uhaba wa vitabu vya sheria hapa nchini na katika vyuo mbalimbali kutokana na vitabu vingi hutoka nje ya nchi.

Hata hivyo alisema kuwa vitasaidia majaji wengine kuvisoma  na mahakimu kuangali ni kwa jinsi gani nchi nyingine wanaendesha kesi na kutolea maamuzi.

Naye Mwenyekiti wa(TAWJA) Jaji Hengera Kileo alisema kuwa kitabu walichozindua  cha sheria kinamrundikano wa kesi mbalimbali  na kutoka nchi nyingine hivyo kitasaidi mahakimu pamoja na wanasheria kujifunza sheria mbali mbali.

Pia alisema kila wanapokutana lazima wazungumzie suala la maadili kwa majaji na viongozi wengine wa mahakama kwani ndiyo chombo kinachoto haki kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment