31 July 2012
Wizara yajipanga kuzuia ugonjwa wa Ebora
Na Grace Ndossa
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii, imesema tayari imejipanga kukabiliana na ugonjwa wa Ebola ambao umeibuka nchini Uganda na kuua watu 14.
Akizungumza na Majira, Msemaji wa Wizara hiyo, Bw. Nsachriss Mwamwaja, alisema tayari wamefanya mawasiliano na mikoa yote nchini pamoja na Wilaya ili wajipange kukabilina na ugonjwa huo.
Alisema habari za kuibuka ugonjwa huo nchini Uganda, zinadai watu 20 ndio wameugua ugonjwa huo lakini 14 wamefariki dunia hivyo Serikali ya inajipanga kuandaa vifaa vya kutosha ili kuwahudumia wagonjwa kama utaingia nchini.
“Wizara ilipopata taarifa hizi, iliwasiliana na kitengo cha dharura na kutoa taarifa katika mikoa na Wilaya zote nchini ili zichukue tahadhari za kukabiliana nao,” alisema Bw. Mwamwaja.
Aliongeza kuwa, mikoa pamoja na Wilaya wametakiwa kutumia vipeperushi vya zamani kutoa elimu kwa wananchi juu ya ugonjwa huo jinsi unavyosambaa ili waweze kuchukua tahadhari.
Alisema tiba ya ugonjwa huo inahusisha vifaa maalumu ambapo hivi sasa, kitengo cha dharura kimeanza kuviandaa na kuviweka tayari.
Bw. Mwamwaja alisema mikoa iliyopo mipakani na viwanja vya ndege, inapaswa kuhakikisha watu wanaotoka na kuingia nchini, kupimwa ili kama akigundulika waana ugonjwa huo, hatua zichukuliwe mapema za kuwapatia matibabu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment