26 July 2012
Wassira kufungua kituo cha kimataifa kupunguza umaskini
Na Grace Ndossa
WAZIRI wa Nchi Mahusiano na Utaratibu Bw. Stephen Wassira, leo anatarajia kuzindua Kituo cha Kimataifa cha Kupunguza Umaskini nchini ambacho kimejengwa na Serikali ya China.
Katika uzinduzi huo, Bw. Wassira atakuwa na Waziri Ofisi wa Serikali ya Jamhuri ya china Bw. Fan Xiaojian ambapo taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, ilisema Mawaziri hao watatilian saini kama ishara ya ushirikiano.
Taarifa hiyo ambayo imesainiwa na Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais Tume ya Mipango, Dkt. Philipo Mpango, ilisema kuazishwa kwa kituo hicho, kutaiwezesha Tanzania kufaidika na maeneo mbalimbali pamoja na kushirikiana kwenye tafiti zinazohusu masuala ya maendeleo.
“Kituo hiki ambacho kwa kifupi kinaitwa IPRCC, ni ishara ya ushirikiano katika nyanja za maendeleo na kupunguza umaskini, ushirikiano huu utakuwa katika tafiti za masuala ya maendeleo, kupunguza umaskini, kubadilishana na kuongeza uzoefu katika masuala haya,” alisema.
Alisema pia watafanya ziara za mafunzo, kubadilishana utaalam na fursa za masomo kwa muda mfupi na mrefu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment