31 July 2012
Mshtakiwa amtaja Bilal kesi ya EPA
Na Rehema Mohamed
MSHTAKIWA wanne katika kesi ya wizi wa zaidi ya sh. bilioni 3.9 katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), Bw. Imani Mwakosya (54), ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Bw. Daudi Balali, alipitisha fedha hizo zilipwe kwa Kampuni ya Mibare Farm kwa kuwa ilionekana ni deni halali.
Bw. Mwakosya aliyasema hayo wakati akitoa utetezi wake mbele ya jopo la Mahakimu watatu wanaosikiliza kesi hiyo Bw. Samuel Kalua, Bi. Beatrice Mutungi na Bw. Ilvin Mugeta, akiongozwa na wakili wa utetezi Bw. Majula Magafu.
Mshtakiwa huyo ambaye alikuwa kifanya kazi Idara ya Madeni katika Benki Kuu, alidai vielelezo mbalimbali vilivyowasilishwa BoT na kampuni hiyo wakati ikiomba kulipwa fedha hizo, vilionekana halali baada ya kupitiwa na maofisa mbalimbali.
Alitaja baadhi ya vielelezo hivyo ni pamoja na hati ya makabidhiano ya deni hilo kati ya Kampuni ya Mibare Farm na Lackshim Textile Mills Ltd ya nchini India.
Alidai deni hilo pia lilionekana katika mtandao wa BoT, taarifa zake na vielelezo ambavyo viliwasilishwa na Kampuni ya Mibare Farm wakati wakidai deni hilo.
“Malipo yalifanyika kihalali kwa sababu vithibitisho vyote ambavyo vilivyotakiwa kuthibitisha deni husika vililetwa BoT na kuonekana halali ndipo gavana alipitisha malipo hayo,” alisema na kudai kuwa, katika mchakato wa ulipwaji wa deni hilo, yeye aliwahi kuandika dokezo la kulipwa kwenda kwa gavana.
Aliongeza kuwa, Kampuni ya Lackshmi Textile Mills Ltd ya India, ilikuwa inaidai Serikali ya Tanzania sh. milioni 307,595,400 na fedha za India rupia milioni 29,220,686.92 sawa na zaidi ya sh. bilioni 3.8.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kada wa CCM Bw. Rajabu Maranda, Bw. Farijala Hussein, Bw. Ajay Somani, Bi. Ester Komu na Bi. Sophia Kalika.
Katika kesi hiyo, washtakiwa hao wanadaiwa kula njama, kugushi na kuiba zaidi ya sh. bilioni 3 .8 kutoka BoT, baada kudanganya kuwa Kampuni ya Mibare Farm imepewa deni na Kampuni ya Lackshim Textile Mills Ltd ya India na kujipatia ingizo hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
thanks for good sharing
ReplyDeleteI like it this blog information
ReplyDelete