28 June 2012
Tunalaani unyama aliofanyiwa Ulimboka
WAKATI Serikali ikiendelea na jitihada za kuupatia ufumbuzi mgomo madaktari, ili umalizike bila kuathiri zaidi hali ya utoaji huduma katika hospitali zetu, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dkt. Steven Ulimboka, amejeruhiwa vibaya baada ya kutekwa nyara usiku wa kuamkia jana katika mazingira ya kutatanisha, jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo la kikatili, linadaiwa kufanywa na watu wasiojulikana, ambao baada ya kufanya unyama huo, walimtelekeza Dkt. Ulimboka katika Msitu wa Mabwepande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Taarifa za kutekwa na kushambuliwa kwa Dkt. Ulimboka, zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alipozungumza na waandishi.
Kamanda Kova alisema, tayari jalada la upelelezi wa shambulio limefunguliwa kwenye Kituo cha Wazo Hill, lenye namba WH/IR/6707/2012.
Alisema Dkt. Ulimbokwa aliokotwa katika msitu huo na mtu mmoja (bila kumtaja jina), ambaye alimbeba katika gari yake na kumpeleka Kituo cha Polisi Bunju, akizungumza kwa sauti ya chini kutokana na kipigo alichopata kwa watu hao.
Kimsingi tukio hili limetusikitisha na kuungana kwa nguvu zote wanaolaani waliohusika na tukio hilo. Ni wazi kuwa Watanzania wengi wana shauku ya kujua ni nini kilichomsibu Dkt. Ulimboka hatua ambayo itasaidia kuepusha taarifa za upotoshaji ambazo zinaweza kuenezwa wakati huu, iwapo ukweli utachelewa kujulikana.
Kwa msingi huo ni imani yetu kuwa wakati leo Serikali ikiratarajia kutoa msimamo wake juu ya mgomo unaoendelea, itatoa ufafanuzi wa kina kuhusu hatua zitakazochukuliwa kuhakikisha wahusika wa unyama huo, wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Tunaungana na Watanzania wengine kulaani na kukemea vikali unyama wa aina hiyo kwani si sehemu ya utamaduni wa Watanzania. Tunasisitiza hivyo kwani tunafahamu kwamba kwa namna moja kitendo alichofanyiwa Dkt. Ulimboka kinaweza kuchochea mgomo huo.
Kwa msingi huo tunatoa mwito kwa Serikali kuchukua hatua stahiki kuhakikisha waliohusika wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Tunahisi Serikali itekeleze hili ikiwa na dhamira kuwa waliomfanyia Dkt. Ulimboka unyama ule walilenga kusiganisha madaktari wetu na Serikali yao.
Ndiyo maana tunatoa mwito kwa Serikali wahuni wote waliohusika na unyama huu wakamatwe ili sheria ichukue mkondo wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
na unyama anaoufanya yeye na madaktari wenzie ni wa kupongezwa. NI BORA WANGEMUUA KABISA. WATU WANAKUFA MAHOSPITALINI KUTOKANA NA MGOMO WA MADAKTARI NA HUYU BWANA ULIMBOKA NDIYE KINARA,TUNASIKIA AANALIPWA MAPESA MENGI NA CHADEMA ILI AIMALIZE SERIKALI ILIYOKO MADARAKANI. MMEWAKUTA WATANZANIA NI WAJINGA,MGONJWA WANGU ANAKUFA HAPO NA DAKTARI ANAMUANGALIA TU,NA MIMI NAMUUA DAKTARI ALIYE KARIBU YANGU. NYIE MADATARI MLIOGOMA MSIMTIBU NA HUYO AONE MACHUNGU YA MGOMO ANAOUSHABIKIA.
ReplyDeleteMADAKARI WOTE WALIOSUKUMA GARI LA ULIMBOKA NA KUMHUDUMIA NI VIZURI KUWACHUNGUZA NYENDO ZAO WATAFUTWE HUKO BAR NA KUWASHUGHULIKIA KAMA DAKTARI WAO WAGONJWA MUWE WAANGALIFU NA HAO WAUAJI WANAWEZA KUPIGWA SINDANO ZA SUMU
ReplyDelete